Wachezaji wa Zimbabwe wakubali kucheza mechi yao dhidi ya Egypt leo

credit: @sokawaytz…

– Wachezaji wa timu ya taifa ya Zimbabwe πŸ‡ΏπŸ‡Ό wamekubali kucheza mchezo wao wa Ufunguzi wa fainali za AFCON 2019 dhidi ya Misri πŸ‡ͺπŸ‡¬ kesho usiku baada ya kukutana na Viongozi wa Soka wa nchini Zimbabwe.

:

– The Warriors walikatisha ghafla mazoezi yao jioni ya leo Sababu ya kutolipwa Posho zao na Bonasi ambazo walitakiwa kuanza kupewa tangu walipo ingia kambini na timu yao ya taifa… Walitishia kutocheza game ya kesho lakini Sasa mambo Shwarii πŸ‘πŸ»πŸ‘πŸ»..

#TotalAFCON2019

@Sokawaytz

Beki wa Kati wa azam mwantika amerudishwa nchini misri Kuziba pengo la agrey Moris alieumia

credit: @sokawaytz…

– Beki wa Klabu ya Azam FC, David Mwantika (Kushoto) amerudishwa nchini Misri tayari kuungana na kikosi cha Taifa Stars kuzipa pengo la Aggrey Morris aliyeumia katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Misri… Mwantika ni miongoni mwa wachezaji waliokatwa katika kikosi cha Awali kilichotajwa na kocha Emmanuel Amunike kujiandaa na Michuano ya AFCON..

#TotalAFCON2019

Misri yaichakaza stars 1-0

credit: @sokawaytz…

FULL-TIME; Kutoka Dimba La Borg El Arab.. Wenyeji Misri wanaibuka na Ushindi Mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Tanzania.. Ulikuwa ni Mchezo wa kutest Mitambo, game nzuri imemalizika salamaa… Taifa Stars kabla ya kuanza kibarua cha AFCON watacheza game nyingine ya kirafiki dhidi ya Zimbabwe..

:

Misri πŸ‡ͺπŸ‡¬ 1-0 Tanzania πŸ‡ΉπŸ‡Ώ

#PreAfcon #TotalAFCON2019 #EGYTAN

Stars yaanza na Senegal Afcon

credit: @sokawaytz…

– Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Emmanuel Amunike, amesema kuwa anaamini kuwa kushinda mechi ya ufunguzi katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika “AFCON” zitasababisha mafanikio kwenye Mashindano hayo kwani kutakuwa na nguvu ya kushinda mechi zinazofuata.

.

– Taifa Stars Imepangwa kuanza na Senegal katika Mchezo wa kwanza wa Kundi la C na legend huyo wa Nigeria anaamini matokeo ya ushindu yataamua muendelezo wa timu katika mashindano huko Misri.

:

πŸ—£ “Tutafungua kampeni yetu ya AFCON dhidi ya Senegal. Kwangu mimi, Senegal ni timu bora Afrika hadi sasa ina wachezaji wengi wazuri, lakini bado tuna wachezaji wetu wazuri ambao wanaweza kuleta matokeo yaliyoridhisha”.

.

πŸ—£ “Unapoingia katika mashindano haya, unapaswa kupata matokeo mazuri ya kwanza ili upate na hakika ya kufanya vizuri na hivyo ndio tutakavyolenga dhidi ya Senegal, kushinda mechi yako ya kwanza katika Mashindano yoyote husaidia sana kuimarisha timu mbele ya mechi nyingine zinazokuja” Amunike aliwaambia Waandishi wa Habari kambini jijini Aleksandria..

#Updates

@Sokawaytz