YANGA KUELEJEA MWANZA KESHO

Kikosi cha Yanga Sc kikiwa na wachezaji 20 pamoja na viongozi 8 kutoka bechi la ufundi, kesho asubuhi kitasafiri kwa ndege kuelekea Mwanza, tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya wenyeji @alliancefootballclub2011 utakaopigwa katika uwanja wa #ccmkirumba 2/3/2019 saa 10:00 jioni.
.
Nahodha @ibrahimajibu23 amesema Ni mchezo muhimu na mgumu, lakini maandalizi mazuri yaliyofanyika kikosini yataleta matokeo mazuri baada ya dakika 90 za mchezo.

R.I.P RUGE MUTAHABA

Tasnia ya Burudani nchini imepatwa na msiba mkubwa baada ya Mkurugenzi wa vipindi Clouds Media Group, Ruge Mutahaba kufariki dunia leo Jumanne, Februari 26 wakati akipatiwa matibabu nchini Afrika Kusini

Ruge atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa wa kukuza sanaa hasa muziki wa kizazi kipya

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli ni miongoni mwa walioguswa na kifo cha Ruge ambapo ametuma salamu za rambirambi

Mungu ailaze roho yake mahali pema, AMEN

FELIX MINZIRO Arejea Kikosini SINGIDA UTD

Klabu ya Singida United imemrejesha aliyekuwa kocha wake Fred Felix Minziro ili kusaidiana na Dragan Popadic kuhakikisha wanajiweka vizuri kunako Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.
.
Awali Minziro aliachwa baada ya kuipandisha Singida United Ligi Kuu mwaka 2017.
.
Kocha huyo miezi michache iliyopita aliondolewa kunako klabu ya Arusha United inayoshiriki Ligi daraja la kwanza kwa kile kilichodaiwa kuwa hakuwa na mwenendo mzuri na kikosi hicho

FT : Lipuli Fc 1-3 Simba

Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba leo wamewaadhibu vikali Lipuli Fc katika uwanja wao wa nyumbani kwa kuwafumua mabao 3-1 kwenye mchezo wa ligi kuu uliopigwa dimba la Samora

Baada ya Lipuli Fc kunusurika katika michezo mitatu iliyopita, leo Simba imepata matokeo stahili baada ya kuwabana vilivyo vijana hao wa Selemani Matola ambaye kabla ya mchezo alitamba kuwa hataki sare

Clatous Chama aliitanguliza Simba mapema tu kwenye dakika ya tano kwa kufunga bao safi kabla Lipuli Fc hawajasawazisha kupitia kwa Paul Nonga kwenye dakika ya 18

Chama tena akaongeza la pili dakika chache kabla ya kwenda mapumziko na Meddie Kagere aliye katika kiwango bora kabisa cha kupachika mabao , akafunga bao la tatu kwenye dakika ya 58

Ushindi huo umeendelea kuisogeza Simba kileleni baada ya kufikisha alama 48, sasa ikiwa nyuma ya Azam Fc kwa tofauti ya alama mbili

Kituo kinachofuata ni Shinyanga ambapo Jumapili, March 03 Simba itachuana na Stand United katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Kambarage

Nkana Fc yawasili Dar

Timu ya Nkana Fc kutoka Zambia imewasili nchini usiku wa kuamkia leo tayari kwa mchezo wa marudiano wa ligi ya mabingwa dhidi ya wenyeji wao Simba.

Mchezo huo utapigwa Jumapili Disemba 23, 2018 kwenye uwanja wa Taifa.

Nkana imekuja mapema kuliko ilivyotarajiwa viongozi wa timu hiyo wakidai wamefanya hivyo ili kupata muda wa kuzoea hali ya hewa ya joto katika jiji la Dar es salaam.

Wakati wapinzani wao wakiwasili, Simba leo inashuka katika dimba la Taifa kucheza na KMC kwenye mchezo wa kiporo wa ligi kuu ya Tanzania Bara.

Mchezo huo utapigwa saa 12 jioni