
Mchezo huo utapigwa Jumapili May 05 katika uwanja wa Sokoine




Mchezo huo utapigwa Jumapili May 05 katika uwanja wa Sokoine



Esperance leo imeilazimisha TP Mazembe suluhu ya bila kufungana katika mchezo uliopigwa dimba la Mazembe, Lubumbashi huku ikitoka kushinda bao 1-0 kwenye mchezo wa kwanza
Mamelodi Sundowns pia imeshindwa kupindua matokeo ya 2-1 iliyofungwa na Wydad Casablanca kwenye mchezo wa kwanza baada ya kulazimishwa suluhu ya bila kufungana
Esperance imetinga fainali kwa msimu wa pili mfululizo sasa itachuana na Wydad Casablanca michezo miwili ya fainali itakayopigwa mwishoni mwa mwsi huu

Yanga ina alama 80 na imebakiwa na michezo minne ambayo hata kama wakishinda yote watafikisha alama 92
Simba yenye alama 75 ikishinda michezo sita itafikisha alama 93 ambazo hazitafikiwa na timu nyingine yoyote
kesho Simba itarejea uwanja wa Sokoine kusaka alama nyingine tatu kati ya 18 zinazohitajika ili kutetea ubingwa katika mchezo dhidi ya Tanzania Prisons
Habari njema ni kwamba baada ya mchezo huo, Simba itarejea jijini Dar es salaam ambako itacheza michezo sita
Ushindi katika michezo hiyo itakayopigwa uwanja wa Taifa/Uhuru, utawahakikishia mabingwa hao kuubakisha ubingwa Msimbazi mapema tu hata kabla ya tarehe ya mwisho ya kufunga msimu

Licha ya changamoto ya ukaribu wa michezo yake, Nyoni amesema wataendelea kujituma ili kupata matokeo yatakayo-wahakikishia kutetea ubingwa waliotwaa msimu uliopita
Baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City jana, kesho Jumapili Simba itarudi tena uwanja wa Sokoine kuikabili Tanzania Prisons
Simba itahitaji kuwa katika ubora wake ili kuondoka na ushindi dhidi ya Prisons iliyoimarisha kiwango chake tangu ilipoanza kunolewa na kocha Adolph Richard
Aidha mazingira ya uwanja wa Sokoine yanaweza kuchangia kuharibu burudani kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha mkoani humo
Hata hivyo Nyoni amesema kama walifanikiwa kupata ushindi dhidi ya Mbeya City kwenye uwanja huo, basi watahakikisha wanashinda mchezo dhidi ya Prisons
“Hali ya uwanja hatuwezi kuikwepa lakini jambo la msingi kwetu tutahakikisha tunapambana. Tunawaahidi mashabiki wetu kuwa tumedhamiria kushinda mchezo huo,” amesema

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Mbeya leo, Manara amesema uongozi wa timu hiyo uliamua kukaa kimya kwa kuwa haukuona umuhimu wa kuwajibu wanaoropoka
Hata hivyo amesema ukimya huo haumaanishi kuwa wanazifurahia kauli hizo
Amesema Simba ni taasisi kubwa na ametaka taasisi hiyo iheshimiwe, isiingizwe katika tuhuma ambazo hazina ukweli wowote
“Tunawataka wote wanaotuhusisha na masuala ya rushwa waache mara moja na kama wana usahidi wapeleke kwa vyombo husika,” amesema
“Simba sio klabu dhaifu, Simba sio klabu nyonge isifike mahali Simba ikafanywa kuwa ni timu dhaifu. Simba ni taasisi kubwa, tunaomba iheshimiwe”
“Mafanikio tunayopata yanatokana na ubora wa timu yetu. Msimu huu tumefika robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa, mtu anasemaje kuwa kiwango cha soka Tanzania hakijapanda?”
“Huku ni kuikosea heshima nchi yetu”

MATOKEO YA MECHI ZA LEO
FT: Mbeya City 1-2 Simba SC (Naldo 22’ : Mkude 68’, Kagere 85’)
.
.
FT: Singida United 1-1 Mtibwa Sugar (Habib Kyombo 32’ : Ismail Aidan 45’+1)
.
.
FT: Ruvu Shooting 3-1 JKT Tanzania (Musa Said 48’, Emmanuel Martin 59’, Fully Maganga 79’: Ally Bilaly 44’)
.
.
FT: Alliance FC 2-2 Kagera Sugar (Birimana Blaise 39’, Dickson Ambundo 90’+5 : Ramadhan Kapera 53’, Peter Mwalyanzi 71’)
.
.
#TanzaniaPremierLeague

Mabao mawili yaliyoiwezesha Simba kupata ushindi wa 2-1 dhidi ya Mbeya City leo, yameifanya timu hiyo iwe imefunga mabao 60
Meddie Kagere sasa ndiye kinara wa kuzifumania nyavu akiwa ametupia kambani mabao 17 akiwaacha washindani wake Salum Aiyee (16) na Heritier Makambo (16)
Katika mabao 60 yaliyofungwa mpaka sasa, Kagere, Okwi na Bocco wamechangia mabao 41
Kagere (17), Okwi (10) na Bocco (14)
Lakini pia Simba ndio timu iliyoruhusu mabao machache zaidi mpaka sasa ikiwa imefungwa mabao 12 tu. Azam Fc inafuatia ikiwa imeruhusu mabao 19
Simba inakaribia kutetea ubingwa wake ikihitaji kushinda michezo sita kati ya tisa iliyobaki
Baada ya mchezo dhidi ya Tanzania Prisons keshokutwa, Simba itarejea jijini Dar es salaam ambako itacheza michezo sita katika dimba la Taifa/Uhuru
Huenda ikatangaza ubingwa kupitia michezo hiyo
Tayari vikosi vimeshaingia uwanja, mchezo ukitarajiwa kuanza punde


Mchezo huo uliathiriwa na mazingira ya uwanja uliojaa maji baada ya mvua kunyesha muda mchache kabla ya mchezo kuanza
Mbeya City ilitangulia kufunga bao katika dakika ya 22 kupitia kwa Iddi Selemani Naddo
Hata hivyo Simba ilirejea ikiwa imara kwenye kipindi cha pili na kusawazisha bao hilo kupitia kwa Jonas Mkude kwenye dakika ya 68 kabla Meddie Kagere hajaihakikishia Simba alama tatu muhimu kwa kufunga bao la ushindi kwenye dakika ya 85

Ushindi huo umeifanya Simba ifikishe alama 75, ikiendelea kushika nafasi ya pili kwa tofauti ya alama tano dhidi ya Yanga
Itacheza mchezo mwingine dhidi ya Tanzania Prisons keshokutwa Jumapili hapohapo dimba la Sokoine

