Mabingwa watetezi ligi kuu ya Tanzania Bara, Simba wanaelekea mkoani Mbeya kuwania alama nyingine sita katika mbio za kutetea ubingwa walioutwaa msimu uliopita
Simba inahitaji kushinda michezo 7 kati ya 10 iliyobaki ili kutetea ubingwa
Habari njema ni kuwa baada ya michezo ya mkoani Mbeya, Simba itarejea jijini Dar es salaam ambako itacheza michezo mitano mfululizo
May 03 itachuana na Mbeya City kwenye uwanja wa Sokoine kisha kurejea katika dimba hilo May 05 kuikabili Tanzania Prisons
Baada ya mchezo huo, Simba itarejea jijini Dar es salaam ambapo May 08 itashuka uwanja wa Uhuru kuikabili Coastal Union kisha kufuatiwa na michezo dhidi ya Kagera Sugar (May 10), Azam Fc (May 13), Mtibwa Sugar (May 16) na Ndanda Fc (May 19) michezo yote ikipigwa uwanja wa Uhuru/Taifa
Simba huenda ikatetea ubingwa wake katika michezo hii saba inayofuata kabla ya kuifuata Singida United May 22. Hata hivyo mchezo dhidi ya Singida huenda ukapangiwa tarehe nyingine kwani May 23 Simba itaecheza na Sevilla mchezo wa Kimataifa wa kirafiki
May 25 SImba itarudi jijini Dar es salaam kucheza na Biashara United kisha kumaliza msimu mkoani Morogoro kwa kuikabili Mtibwa Sugar