Category: simba
Kila kheri Simba, kila la kheri wawakilishi wa nchi

Simba ina nafasi ya kutinga nusu fainali ya michuano hiyo kama itaibuka na ushindi au kutoka sare yoyote ya mabao
Simba ilitua Lubumbashi mapema jana Ijumaa na jioni kupata nafasi ya kufanya mazoezi katika uwanja wa Mazembe ambao utatumika baadae
Kocha Patrick Aussems amesema kikosi chake kiko tayari kuelekea mchezo huo na amewataka wapenzi, mashabiki wa Simba na Watanzania wote kwa ujumla kuwaombea dua ili waweze kuibuka na ushindi
Ushindi wa Simba leo ni faida kwa Tanzania kwani matokeo hayo yataisaidia Tanzania kuongezewa timu za kushiriki michuano ya CAF kuanzia msimu ujao
Simba tayari imedhihirisha kuwa inaweza kupambana na timu yoyote barani Afrika, mchezo wa leo utadhihirisha mara dufu uimara wa Simba
Kila la kheri Simba, kila la kheri mabingwa wa nchi, kila la kheri wawakilishi wa Tanzania..
MAKUNDI AFCON 2019
MAKUNDI YOTE SITA: #AFCON2019
Kundi A
Misri
DR Congo
Uganda
Zimbabwe
Kundi B
Nigeria
Guinea
Madagascar
Burundi
Kundi C
Senegal
Algeria
Kenya
Tanzania
Kundi D
Morocco
Ivory Coast
South Africa,
Namibia
Kundi E
Tunisia
Mali
Mauritania,
Angola
Kundi F
Cameroon
Ghana
Benin,
Guinea-Bissau



Simba yawasili Lubumbashi

Kesho Jumamosi Simba itashuka dimba la Mazembe kuwakabili wenyeji wao katika mchezo wa pili wa robo fainali michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Simba imetumia usafiri wa Ndege Maalum ya kukodi na wataitumia Ndege hiyo kurejea nchini kesho baada ya mchezo
Mabingwa hao wa Tanzania leo jioni wanatarajia kujifua katika uwanja wa Mazembe ambao utatumika kwenye mchezo wa kesho


Aussems aahidi Simba tofauti Lubumbashi
KIKOSI Cha SIMBA kinachoondoka Kuifuata TO MAZEMBE
Makamanda ambao wanaondoka kesho asubuhi kwenda Lubumbashi, DR Congo kuwakabili TP Mazembe. #CAFCL #NguvuMoja


Ni mchezo wa jasho na damu – Manara

Manara amesema Simba inakwenda Congo kupambana na watahakikisha wanaiwakilisha vyema nchi kwa kupata matokeo mazuri katika mchezo huo utakaopigwa keshokutwa Jumamosi kwenye uwanja wa TP Mazembe
Amesema wachezaji wa Simba wako tayari kuandika historia nje ya nchi
“Tunakwenda kesho kibingwa tukiwa hatuna cha kupoteza ila tunawaahidi jasho jingi litamwagika kuipigania Simba na nchi Jumamosi,” amesema Manara
“Hatuogopi lolote toka Mazembe pamoja na kuwapa heshima yao kama klabu kubwa”
“Wachezaji wetu wapo tayari kuionyesha Afrika ubora wao na ukubwa wa Simba. Tuombeeni tufike salama na turejee salama kifua mbele”
Simba inakwenda Congo kwa usafiri wa ndege maalum ya kukodi na itarejea nchini Jumamosi jioni baada ya mchezo
SIMBA: Mazoezi ya mwisho kabla ya safari ya Lubumbashi

Mchezo dhidi ya TP Mazembe utapigwa keshokutwa Jumamosi, saa kumi jioni
Simba itaondoka nchini kesho Ijumaa, April 12 2019





Viporo vya Simba kupangiwa ratiba maalum

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Wambura alisema ratiba ya michezo ya Simba imekuwa na changamoto kutokana na ushiriki wa timu hiyo kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Msimu wa Ligi Kuu 2018/19 unatarajiwa kumalizika May 26 2019 huku Simba, mabingwa watetezi wakiwa bado na michezo 16 ambayo watalazimika kuicheza katika kipindi cha mwezi mmoja na siku kadhaa
“Tutafanyia kazi ratiba ya Simba ili kuhakikisha haiathiri kalenda yetu,” alisema Wambura
“Tutaandaa ratiba maalum kwa klabu ya Simba ili kuhakikisha wanamaliza michezo yao yote bila kuathiri kalenda ya TFF ambapo ligi inapaswa kumalizika mwezi Mei”
Juzi Bodi ya ligi ilisogeza mbele mchezo wa Simba dhidi ya Biashara United ili kuwapa nafasi wawakilishi hao wa nchi wafanye maandalizi ya mchezo wa pili wa robo fainali dhidi ya TP Mazembe
Simba inatarajiwa kuondoka kesho Ijumaa kuelekea DR Congo tayari kwa mchezo huo utakaopigwa uwanja wa TP Mazembe keshokutwa, April 13 2019
FT: Simba U20 1-1 Cameroon U17
Timu ya vijana leo imetoka sare ya goli 1-1 na timu ya Taifa ya Cameroon U-17 katika mchezo wa kirafiki ambao umepigwa kwenye viwanja vya JK Youth Park. #NguvuMoja









