
credit: @sokaonline_…
HII NI FUJO ISIYOUMIZA: Chukua hii. .
.
Justine Shonga ni jina linalozungumzwa sana katika soko la usajili wa vilabu barani Afrika kwasasa. .
.
Huyu ni mzambia anayekipiga katika klabu ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini. .
.
Ubora wake umefanya aingie kwenye kinyang’anyiro cha baadhi ya vilabu barani Afrika pamoja na baadhi ya vilabu vya ulaya. .
.
Taarifa kutoka Afrika Kusini zinadai Orlando Pirates wapo tayari kumuuza nyota huyo, wababe wa Misri Al Ahly wameonyesha nia ya kumhitaji fundi huyo mwenye udambwi udambwi katika eneo lake la kushambulia. .
.
Lakini zipo taarifa ambazo inasemekana klabu ya Simba nayo imeingia kwenye shindano la kuwania saini yake. Ikumbukwe Mo Dewji ambaye ndiye mwekezaji mkuu wa klabu ya Simba aliwahi kutamka kuwa klabu hiyo ina uwezo wa kushindana na klabu yoyote Afrika kwenye saini za wachezaji. .
.
Simba Sc katika orodha yake ya usajili wa wachezaji wa kigeni imebaki nafasi moja, Unafikiri wataweza kuipata saini yake mbele ya Al Ahly ? Tusubiri tuone. .
.
Takwimu za nyota huyo katika msimu uliopita ni kama zinavyosomeka hapo juu. .
.
















