SASA RASMI TANZANIA KUINGIZIA TIMU 4 KIMATAIFA

-Baada ya Jana klabu ya Gor Mahia kutolewa na RS Berkane ya Morocco sasa ni rasmi nchi ya Tanzania itaingiza timu 4 kwenye michuano ya Caf msimu wa 2020/21 ikiwa timu 2 kwenye michuano ya Caf Champions League na timu 2 kwenye michuano ya Caf Confederation Cup.

-Mafanikio ya Simba msimu huu ya kufika robo fainali imeifanya nchi ya Tanzania kupanda kutoka nafasi ya 24 hadi ya 12 watu wanauliza hesabu ya Pointi inahesabiwa vip? Iko hivi twende pamoja

-Pointi ni Perfomance ya vilabu vya nchi husika katika miaka mitano ya nyuma mfano pointi za msimu wa 2020/21 ni kwa miaka mitano ya nyuma yaani 2018/19, 2018, 2017, 2016, na 2015 unazidisha na coeffient namba ya kila mwaka
2018/19 5
2018 4
2017 3
2016 2
2015 1

-kila hatua kwenye michuano ya klabu bingwa ya klabu bingwa Afrika (Caf Champions League) na kombe la Shirikisho (Caf Confederation Cup) kuna pointi zake kama ifuatavyo

Kwenye Caf Champions League
-Bingwa 6
-Mshindi wa pili 5
-Waliofika nusu fainali 4
-Waliofika robo fainali 3
-Walishika nafasi ya tatu kwenye kundi 2
-Walioshika nafasi ya nne kwenye kundi 1

Kwenye Caf Confederation Cup
-Bingwa 5
-Mshindi wa pili 4
-Walioingia nusu fainali 3
-Walioingia robo fainali 2
-Waliomaliza nafasi ya tatu kwenye kundi 1
-Waliomaliza nafasi ya nne kwenye kundi 0.5

-Rank ya 2020/21 unachukua code namba ya mwaka husika kwa miaka mitano ya nyuma unazidisha na Performance ya kila timu kutoka nchi yako na unajumla zote kwa pamoja.

-Mataifa 12 ambayo yanaongoza kwa kuwa na pointi nyingi kwa msimu 2020/21 ni

1-Morocco = ≥143
2-Tunisia = ≥139
3-Misri = ≥110.5
4-Algeria = 92
5-DR Congo= ≥ 87
6-Afrika Kusini = ≥76.5
7-Zambia = 40.5
8-Sudani = ≥35
9-Nigeria = 32.5
10- Guinea = 30
11-Angola = 21.5
12-Tanzania = 18

-Timu zenye alama ya ≥ kubwa kuliko au sawa bado zina timu kwenye mashindano hayo maana yake zinaweza kuongeza pointi au kuishia hapo hapo timu ambazo hazina symbol ya ≥ maana yake mpaka sasa timu zao zimetolewa kwenye mashindano ya Caf Champions League na Caf Confederation Cup

-Tuangalie pointi 18 za Tanzania zimepatikana hivi pointi 15 ni mafanikio ya Simba msimu huu kuingia robo fainali na pointi 3 ni mafanikio ya Yanga kucheza hatua ya makundi ya kombe la Caf Confederationa Cup kwa miaka ya 2018 na 2016

-Hesabu iko hivi mwaka 2016 Klabu ya Yanga iliishia nafasi ya nne kwenye kundi la Kombe la Shirikisho na kuwa na kupata alama 0.5 chukua 0.5 zidisha na Code ya mwaka 2016 ambayo ni 2 (0.5×2=1) kwa mwaka 2018 pia ilishika nafasi ya nne kwenye msimamo wa kundi kwenye michuano ya Caf Confederation Cup chukua Alama 0.5 zidisha na Code ya mwaka 2018 ambayo ni 4 (0.5×4=2)

-Ukichukua 1+2=3 ndio alama ambazo zimetafutwa na klabu ya Yanga pointi 15 za Simba iko hivi imeishia hatua ya robo fainali ya Caf Champions League ambayo alama ya robo fainali ni 3 chukua 3 zidisha na code ya msimu 2018/19 ambayo ni 5 (3×5=15) chukua 3 za Yanga jumlisha 15 za Simba (3+15 =18) ndio point ambazo inazo Tanzania kama nchi.

Ongera Yanga
Ongera Simba
Ongera Tanzania

@yossima Sitta Jr.

Bodi ya Wakurugenzi Simba yakutana Dar

Bodi ya Wakurugenzi ya Simba imekutana leo kwenye kikao cha kawaida jijini Dar es salaam

Kikao hicho kilichoongozwa na Mwekezaji Mohammed Dewji ambaye ndiye Mwenyekiti wa Bodi hiyo, kilikuwa maalum kwa ajili ya kutathmini ushiriki wa Simba kwenye michuano ya ligi ya mabingwa pia kujadili maendeleo ya klabu hiyo

Serikali yafuta viingilio AFCON U17

Wakati wa ufunguzi wa michuano ya AFCON U17 jana, Waziri Mkuu Mh Kassim Majaliwa alitangaza kufuta viingilio kwenye michuano hiyo inayofanyika nchini kwa mara ya kwanza

Katika mchezo wa ufunguzi kati ya Serengeti Boyz dhidi ya Nigeria idadi ya mashabiki waliojitokeza hawakuwa wengi hali iliyopelekea Serikali kuchukua uamuzi huo

Michezo yote inayopigwa kuanzia leo haitakuwa na viingilio hivyo Watanzania wameaswa kujitokeza kwa wingi kushuhudia michuano hiyo inayofanyika katika viwanja vya Taifa na Azam Complex

Mkongwe Yanga awapa somo wanachama kuelekea uchaguzi

Maamuzi ya Yanga kufanya uchaguzi mkuu Mei 5, yanatajwa ni mapinduzi mapya ya kiuchumi, kimtazamo na mawazo ndani ya klabu hiyo, tofauti na hali ambayo wanapitia kwa sasa.

Mchezaji wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Bakari Malima ‘Jembe Ulaya’ alisema uchaguzi huo ulenge kuwapata watu sahihi ambao, watakuwa na nia ya kuipeleka Yanga kwenye ushindani wa kimataifa.

“Simba imara inahitaji Yanga imara kwa sababu klabu hizi mbili ni kioo cha soka la Tanzania huo ndio ukweli, uchaguzi utakaofanyika Mei 5 kwa Yanga uwe wa mapinduzi ya kuleta vitu tofauti na vyenye tija sio kama miaka iliopita.

“Natamani ziingie sura mpya na sio wale ambao walikuwepo kwenye uongozi wa nyuma kwani, hawakuweza kufanya kitu chochote.

“Yanga tunahitaji ifike mbali na sio ilivyo kwa sasa mpaka inafikia mahali tunachangishana, klabu hiyo ni tajiri hapa vije vichwa vya kufanya mambo.

“Wanaochagua viongozi waache tamaa za kuchukua posho za wagombea, hilo limewahi kunikuta uchaguzi uliopita niligombea ujumbe watu wanataka niwape pesa natoa wapi sasa. nilipata kura 577, hivyo sikupita kwani walitakiwa 10 tu mimi nilikuwa wa 11.

“Uchumi ndio kikwazo cha wachezaji wa zamani tushindwe kwenda kuchukua fomu ili kusaidia klabu kuwa na soka la mfano, lakini yote kwa yote waje watu makini ambao, wana uwezo wa kubuni mikakati mipya ili kuhakikisha Yanga inafika mbali tofauti na mambo yalivyo sasa”

Mwanaspoti

Simba kuifuata Coastal Union Jumatatu

Msafara wa kikosi cha Simba unatarajiwa kuondoka jijini Dar es salaam kesho Jumatatu kuelekea mkoani Tanga kuikabili Coastal Union kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara

Mchezo huo wa kwanza baina ya timu hizo msimu huu, utapigwa siku ya Jumatano, April 17 kwenye uwanja wa Mkwakwani

Baada ya kumaliza majukumu ya michuano ya CAF, Simba imedhamiria kutetea ubingwa wake kuhakikisha inapata nafasi ya kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa msimu ujao

Simba imerejea nchini usiku wa kuamkia leo ikitokea DR Congo ambako iliondoshwa na TP Mazembe kwenye michuano ya ligi ya mabingwa hatua ya robo fainali

Serengeti Boyz yapoteza mchezo wa kwanza AFCON U17

Timu ya Taifa ya vijana umri chini ya miaka 17 Serengeti Boyz, imeanza vibaya michuano ya AFCON U17 inyofanyika nchini baada ya kukubali kipigo cha mabao 5-4 kutoka kwa Nigeria katika mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa

Licha ya kupoteza mchezo huo, Serengeti Boyz ilicheza vizuri na hakika hawapaswi kulaumiwa

Edmund John aliifungia Serengeti Boyz mabao mawili moja likiwa la mkwaju wa penati huku mengine mawili yakifungwa na Kelvin John ‘Mbappe’ na Morice Abraham (p)

Vijana wa Nigeria walifunga mabao yao kupitia kwa Olatomi, Ubani aliyefunga mabao mawili, Amoo na Abraheem

Mchezo unaofuata wa Serengeti Boyz ni April 17 dhidi ya Angola kabla ya kumaliza hatua ya makundi kwa kuchuana na Uganda April 20