Aston Villa yarudi ligi kuu ya uingereza

– Aston Villa imefanikiwa kupanda Ligi Kuu Nchini Uingereza “Premier League” Baada ya ushindi wa Magoli 2-1 dhidi ya Derby Country mapema siku ya jana, katika Mafanikio hayo waliyopata kwa Mara ya kwanza takribani miaka Mitatu kwa Kiasi kikubwa imechangiwa na Wachezaji kutoka Bara La Afrika.

.

– Mfungaji bora wao Tammy Abraham licha tu ya kuichezea timu ya taifa ya England U21 lakini Nigeria wameendelea kumshawishi kurejea nyumbani kabla ya kuanza kucheza Senior team Moja kwa Moja, Mshambuliaji Anwar El Ghazi licha tu ya kuichezea timu ya taifa ya Uholanzi U21 Morocco hawajaacha kumshawishi kurejea nyumbani, Beki na nahodha wa Misri, Ahmed Elmohamady, Albert Adomah wa Ghana wa Nyota wa Ivory Coast, Jonathan Kodjia wameisaidia Aston Villa kwa kiasi chake kuhakikisha imerejea Ligi Kuu… Baada ya wao kupanda wanahitimisha Timu tatu Baada ya Mbili kutangulia ambazo ni Norwich City na Sheffield United.

.

– Magoli kutoka Kwa, Anwar El Ghazi na John McGinn yaliweza kutosha na kuwapandisha PL vijana hao wa kocha Dean Smith katika Dimba la Wembley, Martin Waghorn aliwafuta machozi Derby kwa Goli lake Dakika 10 za Mwisho wa Mchezo huo..

#Updates

@Sokawaytz

credit: @sokawaytz

Jorome Boateng atakiwa kuondoka Bayern Munich

Rais wa Klabu ya Bayern Munich Uli Hoeness amemwambia beki wa kati wa klabu hiyo Jérôme Boateng kuwa muda wa kucheza Bayern umeisha hivyo angependa kumshauri atafute klabu nyingine. (DW SPORTS) .

.

Mpaka sasa klabu za Arsenal pamoja na Manchester United zimeonyesha nia ya kumhitaji.

credit: @sokaonline_

Daniel Alves apewa unahodha timu ya taifa ya Brazil

– Imethibitisha Rasmi, Dani Alves ndiye nahodha mpya wa timu ya taifa ya Brazil katika Michuano ijayo ya Copa América, Kocha Tite kampiga chini Staa wao, Neymar Jr ambaye alimpa kitambaa hicho mwaka jana kuwa nahodha wa Brazil.

:

Brazil wanatarajia kuwa wenyeji wa Copa America, Mabingwa hao Mara Nane Mara ya mwisho mwaka 2016 walifanya vibaya lakini mwaka huu wakiwa kundi A pamoja na Bolivia , Peru na Venezuela watajaribu kufanya vema zaidi, Brazil game yao ya kwanza katika Michuano hii wataanza na Bolivia ndani ya Sao Paulo siku ya June 14..

#Updates

@Sokawaytz

credit: @sokawaytz

Mshambuliaji wa Chelsea Edin Hazard ashinda Tuzo ya mchezaji bora wa EPL msimu huu 2018-2019

– Mshambuliaji wa Klabu ya Chelsea, Eden Hazard ametwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa msimu wa Premier league 2018/19 kwa upande wa Mashabiki (PFA Fans Player of the Year); Hazard katika msimu huo Akiwa na The Blues kafunga magoli 16 na kutoa Assist 15:

:

✋🏻 Mpaka Sasa tuzo alizokusanya Hazard msimu huu.

🎯 Mchezaji mwenye Assist nyingi zaidi katika msimu ndani ya Premier League.

🥇 Mchezaji Bora wa Mwaka wa Mashabiki ndani ya Premier league.

🥇Mchezaji bora wa Mwaka wa Chelsea.

🥇Mchezaji Bora wa Mwaka wa Wachezaji ndani ya Chelsea.

🥇 Goli Bora la mwaka ndani ya Chelsea.

✋💷 £130m Dau La Chelsea kwa Klabu inayotaka Kumnunua..

#premierleague #chelsea

@Sokawaytz

credit: @sokawaytz

Mshambuliaji Mwenye uraia wa Tanzania Adi Yusuf Aachana na timu yake Solhull moors fc ya uingereza daraja la 5

– Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania, Adi Yussuf Rasmi Amethibitisha kuachana na Klabu aliyokuwa akiichezea, Solihull Moors FC ya National League nchini Uingereza (Daraja La tano) Baada ya kutofikia muhafaka wa Mkataba mpya kwa ajili ya msimu ujao.

.

– Adi mwenye umri wa miaka 26, Alijiunga na klabu hiyo January 25,2018 kwa Mkataba wa mwaka Mmoja na Nusu Baada ya kumaliza Mkataba wake na Klabu ya Barrow nayo ya National League akiichezea mwaka mmoja tu tangu ajiunge nao Julai 29, 2017.

.

– Katika Game yake ya kwanza tu akiwa na Solihull alifunga Magoli mawili katika Dakika mbili dhidi ya  Dagenham akicheza Dakika 70.. Tangu hapo kacheza game zaidi ya 50 na kufunga Magoli zaidi ya 20..@adiyussuf anajiandaa kutua Nchini tayari kujiunga na kambi ya @taifastars_ kujiandaa na Maandalizi ya AFCON 2019.

#Tanzania #TotalAFCON2019

@Sokawaytz

credit: @sokawaytz

Stock city yamtema mshambuliaji wa Burundi saida Beraino

– Klabu ya Stoke City Inayoshiriki Championship nchini England, Imethibitisha kusitisha Mkataba na Mshambuliaji wake, Saido Berahino; Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ambaye alikutwa na kosa La Ulevi akiwa anaendesha gari mwezi huu na kufungiwa kuendesha vyombo vya Moto Uingereza, na kupigwa faini ya £75,000 na Mahakama ya Highbury Corner Magistrates.

:

– Mnamo Januari 2017, Berahino alijiunga na Stoke kutokea West Bromwich Albion kwa ada ya uhamisho £12m na alisaini Mkataba wa miaka Mitano, Amecheza michezo 51 ya ligi akifunga magoli matatu; Tangu akutwe na Makosa ya Ulevi hajawahi tena kupangwa katika kikosi cha timu yake mpaka walipotoa taarifa ya kuvunja Mkataba uliokuwa umalizike 2022.

:

– Mwezi ujao, Berahino atatarajiwa kuwa sehemu ya Kikosi cha Burundi katika Mechi za Mataifa ya Afrika AFCON 2019 nchini Misri..Vijana hao wa kocha Olivier Niyungeko wamepangwa kundi B, ambapo watacheza na Nigeria Juni 22 kabla ya kucheza Madagascar siku tano baadaye na kumaliza na Guinea siku ya Juni 30..

#Updates

@Sokawaytz

credit: @sokawaytz