Simba yampa mtihani Meddie Kagere avunje rekodi ya Abdallah Juma kwa ufungaji msimbazi

“Amekuwa na msimu mzuri na anapambana muda wote, nadhani ataweza kufunga mabao mawili katika mchezo uliobaki na kuifikia rekodi ya Abdallah Juma nasi wachezaji tutamsaidia kwakua tunashirikiana sana,” Nahodha wa Simba, John Bocco akimzungumzia Meddie Kagere kuelekea kufikia rekodi ya ufungaji ya Abdallah Juma kwenye ligi kuu. Kwa sasa Kagere ana mabao 23.

credit: @simbamakini

Okwi awashitua mashabaki wa simba sc clubs

✋ Emmanuel Okwi juu ya Ujumbe wake katika mtandao wa Instagram uliozua sintofahamu kwa Mashabiki wake na Klabu yake ya @simbasctanzania kwamba je ni kweli ameaga kuachana Mabingwa hao.

:

👉 “Nimeweka ujumbe huo sikuwa na maana yoyote zaidi ya wimbo mmoja ambao naupenda na umejizolea umaarufu na wapenzi wa Simba wasiwe na wasiwasi wowote kuhusu hilo,” alisema Okwi.

.

– Okwi amekuwa akihusishwa kutimka ndani ya Klabu ya @simbasctanzania Kipindi hiki ambacho Mazungumzo ya Kusaini Mkataba mpya na Klabu yake yamepungua.. @kcfcofficial ya Afrika Kusini ndio Klabu inayotajwa kumuhitaji.

#simbasc #transfers

@Sokawaytz

credit: @sokawaytz

Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano ya castle lager msimu huu

Michuano ya #CastleLager #Africa5s imerejea tena kwa msimu wa pili na mwaka huu inafanyika hapa hapa nchini Tanzania.

•••

USIKOSE siku ya uzinduzi wa michuano hiyo Tarehe 8/6 Ndani ya Uwanja wa Uhuru Jijini Dar Es Salaam ambapo Gwiji wa Soka Duniani Samuel Etoo atakuwepo.

•••

Burudani ya Muziki itakuwepo kutoka kwa @officialalikiba @harmonize_tz na @officialnandy

•••

Kiingilio kitakuwa ni ‘BURE ‘

….

Ratiba ya uzinduzi.

🏆: #CastleLager #Africa5s.

🕤: Kuanzia Saa 4:00 Asubuhi.

🏟: Uwanja wa Uhuru.

🎤: @officialalikiba @harmonize_tz @officialnandy

💵: BURE.

@castlelagertz #CastleLager #Africa5s #kfs #Kitaakimetuamini

credit: @tv1tanzania

Man United walia na Ajax kuipata saini ya beki na captain wao kisiki Matthijs de Ligt

– Kwa mujibu wa @skysports, Klabu ya Manchester United Imejitoa katika mbio za kumuwania Beki na nahodha wa Klabu ya Ajax, Matthijs de Ligt.

.

Kwa mujibu wa vyanzo, United ilikuwa tayari kutoa £65m kuinasa saini ya Beki huyo wa timu ya taifa ya Uholanzi mwenye umri wa miaka 19; United imejitoa rasmi kumuwania De Ligt, hivyo kuna uwezekana mkubwa kwa nyota huyo kujiunga na Mabingwa wa Hispania Klabu ya FC Barcelona..

#transfers

credit: @sokawaytz

YONDANI: Amtibua ZAHERA

Kikosi cha Yanga leo kimeendelea na mazoezi kwenye uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo wa mwisho wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Azam Fc utakaopigwa Jumanne, May 28 dimba la Uhuru

Kocha Mkuu wa mabingwa hao wa kihistoria Mwinyi Zahera amesema baadhi ya wachezaji waliokuwa wagonjwa wameanza kurejea kikosini

“Paul Godfrey alikuwa mgonjwa lakini leo ameanza mazoezi. Dante, Abdul, Ngasa, Banka, Jaffar na Ajib bado wagonjwa,” amesema

Katika hatua nyingine Zahera amemuagiza Meneja wa Yanga Nadir Haroub kumsaka beki wa timu hiyo Kelvin Yondani ambaye haonekani mazoezini

Zahera amesema hana taarifa kama Yondani ni mgonjwa, amejaribu kumpigia simu bila ya mafanikio

“Sina taarifa za Yondani, nimejaribu kumpigia simu lakini hapokei, tumemtuma Meneja (Nadir) aende akamtafute kwake anipe mrejesho kabla sijafanya maamuzi,” Zahera aliiambia eFM