Mabingwa watetezi ligi kuu ya Tanzania Bara Simba leo wanashuka uwanja wa Sokoine kuikabili Tanzania Prisons katika mchezo wa ligi
Hiki hapa kikosi kinachoanza mchezo huo;
Hiki hapa kikosi kinachoanza mchezo huo;




Lakini asikwambie mtu, mzuka wa mashabiki wa timu hiyo mkoani Mbeya, unawafanya mabingwa hao wa Tanzania Bara kutojihisi kabisa kama wako ugenini
Katika mchezo dhidi ya Mbeya City ambao Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-1, mashabiki wa ‘Mnyama’ walifunika dimba la Sokoine.


Leo tena wameahidi kuwa sambamba na timu yao kuhakikisha alama zote tatu zinakwenda Msimbazi
Mchezo unatarajiwa kuanza saa kumi kamili jioni na tayari mashabiki wameanza kujisogeza uwanja wa Sokoine

Mchezo ambayo kama Simba itaibuka na ushindi, itasogea zaidi kileleni mwa msimamo wa kwani itabakisha alama mbili tu kuifikia Yanga
Meneja wa Simba Patrick Rweyemamu amesema wachezaji wa timu yake wako katika hali nzuri, wamejiandaa vyema kuweza kupata alama nyingine tatu leo
Tanzania Prisons ilitua mkoani Mbeya juzi ikitokea Dar es salaam ambako ilifungwa na Yanga mabao 2-1
Kocha Mkuu wa timu hiyo Adolph Richard amesema wanatarajia mchezo hautakuwa mwepesi lakini wamepania kupata matokeo ili kujiweka salama na hatari ya kuteremka daraja
Baada ya mchezo huo Simba itarejea jijini Dar es salaam ambako itakuwa na nafasi ya kutwaa ubingwa katika michezo sita itakayocheza uwanja wa Taifa/Uhuru

Uhakiki wa wanachama utaanza saa mbili mpaka saa nne na nusu asubuhi
Hii hapa Ratiba kamili;


Mchezo huo utapigwa Jumapili May 05 katika uwanja wa Sokoine



Esperance leo imeilazimisha TP Mazembe suluhu ya bila kufungana katika mchezo uliopigwa dimba la Mazembe, Lubumbashi huku ikitoka kushinda bao 1-0 kwenye mchezo wa kwanza
Mamelodi Sundowns pia imeshindwa kupindua matokeo ya 2-1 iliyofungwa na Wydad Casablanca kwenye mchezo wa kwanza baada ya kulazimishwa suluhu ya bila kufungana
Esperance imetinga fainali kwa msimu wa pili mfululizo sasa itachuana na Wydad Casablanca michezo miwili ya fainali itakayopigwa mwishoni mwa mwsi huu

Hafla hiyo sasa itafanyika May 18 Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam
Mwili wa Dk Mengi unatarajiwa kuwasili Jumatatu ambapo utahifadhiwa kwenye nyumba yake ya milele Jumamosi ya May 11, Machame mkoani Kilimanjaro

Inaelezwa Igangula ameamua kumuunga mkono Dk Mshindo Msolla ambaye sasa atachuana na Dk Jonas Tiboroha aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Yanga
Dk Msolla amepata uungwaji mkono mkubwa na anapewa nafasi kubwa ya kuibuka kidedea kwenye uchaguzi huo wa kesho

Wagombea walianza kunadi sera zao kwa Wanachama Jumanne iliyopita
Nafasi ya Mwenyekiti wa Yanga inawaniwa na wagombea watatu Barak Igangula, Dk Jonas Tiboroha na Dk Mshindo Msolla wakati nafasi ya Makamu Mwenyekiti inawaniwa na wagombea wanne ambao ni Fredrick Mwakalebela, Janeth Mbene, Titus Osoro na Yono Kevela
Aidha wagombea 21 wanawania nafasi nane za wajumbe wa Kamati ya Utendaji
Wanachama wa Yanga wametakiwa kutofanya makosa kwenye uchaguzi wa kesho kwa kuwachagua viongozi ambao wataweza kuipeleka Yanga mbele
Suala la Mabadiliko limekuwa kilio cha Wanayanga. Wagombea wote wameahidi kufanya mabadiliko, ni jukumu la Wanachama kujiridhisha na uwezo wao na ahadi walizotoa katika kutatua changamoto zinazoikabili Yanga
Wanachama wameaswa kutochagua viongozi kwa mazoea badala yake wachague viongozi ambao wana upeo mkubwa
Ni vyema kiongozi atakayechaguliwa awe na uwezo wa kutengeneza mikakati ya kuipeleka Yanga kule ambako kila mdau anahitaji kuona klabu ikielekea
Huu sio wakati wa kujaribu viongozi, Wanachama wawaweke madarakani ‘watu wa kazi’
Wanachama wasichague viongozi kwa papara, mihemko na makundi, kila mmoja afanye uamuzi kwa maslahi ya klabu kwa kuchagua viongozi wenye tija
Yanga ikipata viongozi wazuri, utakuwa mwanzo wa kutengeneza Yanga imara ambayo itagombewa na wawekezaji na kuifanya timu hiyo kongwe zaidi Tanzania kuondokana na dimbwi la ‘umasikini’