BREAKING NEWS: REGINALD MENGI AFARIKI DUNIA

Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP , Dkt Reginald Abraham Mengi (75) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.

Dk Mengi amefariki dunia akiwa jijini Dubai, Falme za Kiarabu (UAE).

Dk Mengi alikuwa ni mfanyabiashara mkubwa barani Afrika, ambapo sehemu ya utajir wake aliuelekeza kwa jamii kwa kutoa misaada mbalimbali.

Kwa mujibu wa jarida la Forbes mwaka 2014, utajiri wa bilione huyo ulitajwa kuwa ni TZS trilioni 1.3 ($560 milioni).

Enzi za uwahi wake na katika shughuli zake aliweza kushinda tuzo mbalimbali za kitaifa na kimataifa, pamoa na kuandika kitabu chake cha I Can, I Must, I will.

Mungu Ailaze Roho yake Mahali Pema Peponi. Amina

Yanga kuikabili Tanzania Prisons uwanja wa Uhuru kesho

Ligi Kuu ya Tanzania Bara inaendelea kesho ambapo vinara wa ligi hiyo Yanga watakuwa uwanja wa Uhuru kupepetana na Tanzania Prisons

Baada ya juzi kuichapa Azam Fc bao 1-0, Yanga itakuwa na nafasi ya kuzidi kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi kama itaibuka na ushindi kwenye mchezo huo

Mabingwa hao wa kihistoria wamesalia na michezo mitano kabla ya kumalizika kwa ligi, kama watashinda yote watafikisha alama 92

Bado Yanga haiwezi kuondolewa katika mbio za ubingwa kwani wapinzani wao Simba bado watahitaji kupata matokeo katika michezo yao10 iliyobaki ili waweze kutete ubingwa

Baada ya mchezo wa kesho Yanga itaelekea mkoani Iringa tayari kwa mchezo wa nusu fainali kombe la FA dhidi ya Lipuli Fc utakaopigwa May 06 2019

Ajib ajumuishwa kikosi cha Stars

Hatimaye kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Emmanuel Amunike amemjumuisha nahodha wa Yanga Ibrahim Ajib kwenye kikosi cha timu ya Taifa kitakachoshiriki michuano ya AFCON itakayofanyika mwezi ujao nchini Misri pamoja na michuano ya CHAN inayohusisha wachezaji wa ndani

Kikosi hicho chenye wachezaji 39 pia kimewajumuisha Gadiel Michael, Kelvin Yondani na Feisal Salum kutoka klabu ya Yanga

Simba kushirikiana na Porto FC

Mwekezaji wa klabu ya Simba Bilionea Mohammed Dewji ‘Mo’ akiwa nchini Ureno alitembelea kitua cha kulelea vipaji cha klabu ya Porto Fc

Ziara yake hiyo ilikuwa mahsusi kwa ajili ya kutafuta fursa ya ushirikiano baina ya klabu ya Porto Fc na Simba

“Jana nilipata nafasi nzuri ya kujifunza nilipoitembelea @FCPorto ambapo niliweza kujua fursa za ushirikiano kwa kituo cha kukuzia vipaji cha Simba huko mbeleni,” amebainisha Mo

“Tuna mengi ya kujifunza na kupata kutokana na uzoefu wa Porto FC. Natarajia kuimarisha mazungumzo yetu hivi karibuni”

Hii ni habari njema kwa Simba ambayo ina mipango ya kujenga mifumo imara itakayoinufaisha klabu hiyo siku za mbeleni

Zana aipa mtihani Simba

Licha ya ubora wake hasa wakati timu ikishambulia, beki wa kulia wa Simba Zana Coulibaly ameonesha kuwa na mapungufu hasa wakati timu inapokuwa inashambuliwa
Katika michezo ya hivi karibuni, Zana aliyetua Simba wakati wa usajili wa dirisha dogo, ameonekana kutotimiza vyema majukumu yake katika ulinzi

Na hiyo imekuwa sababu ya mashabiki wengi wa Simba kuulizia hali ya Shomari Kapombe ambaye licha ya kuanza mazoezi mepesi, kuna uwezekano mdogo kwake kurejea dimbani msimu huu kutokana na muda uliobaki kuwa mdogo kabla ya ligi kumalizika

Katika mchezo dhidi ya JKT Tanzania, kocha Patrick Aussems alilazimika kumfanyia mabadiliko Zana kwenye kipindi cha pili nafasi yake kuchukuliwa na Nicholas Gyan

Inaelezwa Zana alipata majeraha ya goti

Zana alisajiliwa kuongeza nguzu pembeni baada ya Kapombe kupata majeraha wakati akitimiza majukumu ya timu ya Taifa nchini Afrika Kusini

Hata hivyo Simba huenda ikalazimika kufanya uamuzi mgumu wakati wa usajili kwa kuachana na mmoja kati ya Zana au Gyan anayeonekana kupoteza nafasi katika kikosi cha kwanza

Sita Simba waitwa Stars kwa ajili ya AFCON na CHAN

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Emmanuel Amunike leo ametangaza majina ya wachezaji 40 wanaounda kikosi cha timu ya Taifa ambacho kitashirikia michuano ya AFCON 2019 itakayofanyika mwezi ujao nchini Misri pamoja na michuano ya CHAN inayohusisha wachezaji wa ndani

Katika kikosi hicho, wachezaji wa Simba Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohammed Hussein, Erasto Nyoni, Jonas Mkude na John Bocco wamejumuishwa

Kapombe aitwa Stars, yaelezwa atakuwa ‘fiti’ kucheza AFCON 2019

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania Emmanuel Amunike ameonyesha imani kwa beki wa Simba Shomari Kapombe baada ya kumjumuisha kwenye kikosi chake cha awali ambacho baadae kitatenganishwa kwa ajili michuano ya AFCON 2019 na michuano ya CHAN inayohusisha wachezaji wa ndani

Kapombe aliumia Afrika Kusini mwezi Novemba mwaka jana wakati akiitumikia timu Taifa.

Amekuwa nje kwa zaidi ya miezi mitano akiuguza majeraha ya goti ambayo yalihitaji kufanyiwa upasuaji

Baada ya kupona majeraha, Kapombe tayari ameanza mazoezi mepesi na inaelezwa ataweza kushiriki michuano ya AFCON itakayofanyika mwezi ujao nchini Misri

Hii ni habari njema kwa Simba ambayo huenda ikamtumia beki huyo mwenye uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya moja katika baadhi ya michezo yake ya kumaliza msimu

Hizi hapa mechi za ubingwa Simba

Mabingwa watetezi ligi kuu ya Tanzania Bara, Simba wanaelekea mkoani Mbeya kuwania alama nyingine sita katika mbio za kutetea ubingwa walioutwaa msimu uliopita

Simba inahitaji kushinda michezo 7 kati ya 10 iliyobaki ili kutetea ubingwa

Habari njema ni kuwa baada ya michezo ya mkoani Mbeya, Simba itarejea jijini Dar es salaam ambako itacheza michezo mitano mfululizo

May 03 itachuana na Mbeya City kwenye uwanja wa Sokoine kisha kurejea katika dimba hilo May 05 kuikabili Tanzania Prisons

Baada ya mchezo huo, Simba itarejea jijini Dar es salaam ambapo May 08 itashuka uwanja wa Uhuru kuikabili Coastal Union kisha kufuatiwa na michezo dhidi ya Kagera Sugar (May 10), Azam Fc (May 13), Mtibwa Sugar (May 16) na Ndanda Fc (May 19) michezo yote ikipigwa uwanja wa Uhuru/Taifa

Simba huenda ikatetea ubingwa wake katika michezo hii saba inayofuata kabla ya kuifuata Singida United May 22. Hata hivyo mchezo dhidi ya Singida huenda ukapangiwa tarehe nyingine kwani May 23 Simba itaecheza na Sevilla mchezo wa Kimataifa wa kirafiki

May 25 SImba itarudi jijini Dar es salaam kucheza na Biashara United kisha kumaliza msimu mkoani Morogoro kwa kuikabili Mtibwa Sugar

Simba na JKT Tanzania kupigwa uwanja wa Uhuru

Leo mabingwa watetezi ligi kuu ya Tanzania Bara Simba wanashuka kunako uwanja wa Uhuru kuwakabili maafande wa JKT Tanzania katika mchezo ambao utapigwa saa kumi kamili jioni

Mchezo huo awali ulipangwa kufanyika uwanja wa Taifa lakini umehamishwa ili kupisha ukarabati wa uwanja wa Taifa baada ya kumalizika mwa michuano ya AFCON U17

Simba inarejea uwanja wa Uhuru kwa mara ya kwanza msimu huu ikiwa na ‘mfalme’ Emmanuel Okwi ambaye msimu uliopita aliwea rekodi ya kupachika mabao mengi kwenye uwanja huo

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema wamedhamiria kushinda michezo yote iliyobaki, wanahitaji kushinda dhidi ya maafande

Katika mchezo wa kwanza uliozikutanisha timu hizo ambao ulipigwa jijini Tanga, Simba iliondoka na ushindi wa mabao 2-0