Viongozi hakikisheni Yanga inamaliza msimu salama

Mpaka hapa ilipofika Yanga hata kama haitatwaa ubingwa wa ligi kuu, msimu huu utabaki kuwa wa mafanikio kwa mabingwa hao wa kihistoria

Licha ya kukabiliwa na changamoto za kiuchumi, wachezaji wa timu hiyo wamepambana na kuweza kufanya vizuri kwenye ligi huku wakitinga nusu fainali ya michuano ya kombe la Azam (ASFC)

Mwanzoni mwa msimu hakuna aliyeipa Yanga nafasi ya kufanya vizuri kutokana na kushindwa kufanya usajili ‘mkubwa’ ukilinganisha na wapinzani wake Simba na Azam Fc

Bila shaka mgomo waliofanya wachezaji juzi umewasikitisha wengi, ni faraja kusikia uongozi wa timu hiyo umechukua hatua haraka kuirejesha timu katika hali ya kawaida

Wachezaji na benchi la ufundi wamefanya kazi kubwa katika mazingira magumu, litakuwa jambo la kusikitisha kama walichokifanya wakati wa shida kitaharibiwa dakika hizi za majeruhi

Naamini viongozi wameyasikia malalamiko ya wachezaji, wayapatie ufumbuzi mapema ili wamalize msimu kwa moyo mmoja

Yanga bado inawania mataji mawili, wakati huu inapaswa fikra za wachezaji ziwe katika kumaliza msimu kwa nguvu ili washinde angalau taji moja kuliko kufikiria mambo mengine

Niyonzima aomba radhi

Kiungo fundi Haruna Niyonzima amewaomba radhi kwa uongozi wa klabu ya Simba pamoja na mashabiki wa timu hiyo kufuatia kadi nyekundu aliyopewa kwenye mchezo wa jana dhidi ya Biashara United, mchezo ambao Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-0

Niyonzima amesema anajutia tukio alilofanya ambalo lilisababisha apewe kadi nyekundu

“Ulikua mchezo wenye presha kubwa sana ukizingatia tulihitaji sana matokeo kuliko chochote,” amesema

“Iliniumiza sana kutoka uwanjani nikiacha timu yangu pungufu. Niombe radhi kwa klabu yangu mashabiki zetu waliosafiri mpaka Mara na pia wale wote mliokua majumbani mkitizama kupitia televisheni”

“Nilichofanya hakikuwa bora kwa ustawi wa mpira wetu samahani wote mliokwazika, tutapambana mpaka tone la mwisho kwajili ya ubingwa”

Mashabiki wa Simba Mara ‘mmetisha’

Mapokezi na sapoti iliyopata Simba mkoani Mara ni ya kipekee na hakika watu wa Musoma wanastahili pongezi kwa ‘vibe’ la maana waliloonyesha leo

Simba haikuwa imefika Mara katika kipindi cha miaka 15 kutokana na mkoa huo kukosa timu ya ligi kuu, makaribisho iliyopata yanadhihirisha ukubwa wa Simba nchini Tanzania kwa sasa

Baada ya mchezo wa leo kikosi cha Simba kinatarajiwa kuondoka kesho kurejea jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo unaofuata dhidi ya JKT Tanzania

FT : Biashara United 0-2 Simba

Simba imeendeleza umwamba wake kwenye ligi kuu ya Tanzania Bara baada ya leo kuifumua Biashara United mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Karume, Mara

Simba imefikisha alama 69 sasa ikitofautiana na Yanga kwa tofauti ya alama tano tu huku kibindoni ikiwa na michezo mitano ya viporo

Shukrani za kipekee zimwendee nahodha John Bocco aliyefunga mabao yote mawili kwenye kipindi cha kwanza na kuihakikishia Simba alama tatu muhimu

Bocco amefikisha mabao 14 akichupa mpaka nafasi ya tatu kwenye orodha ya vinara wa mabao nyuma ya Makambo mwenye mabao 15

Aidha Bocco amefikisha idadi ya mabao aliyofunga msimu uiliopita

Katika mchezo huo Simba ilipata pigo baada ya kiungo wake Haruna Niyonzima kutolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumtolea maneno machafu mwamuzi

Simba imemaliza michezo ya kanda ya ziwa na sasa inarejea jijini Dar es salaam ambapo Jumanne itachuana na JKT Tanzania, mchezo utakaopigwa uwanja wa Uhuru

Mashabiki mapemaa uwanja wa Karume

Leo saa kumi kamili jioni mabingwa wa nchi Simba watashuka kwenye uwanja wa Karume kuchuana na Biashara United katika mchezo wa kiporo wa ligi kuu ya Tanzania

Simba ilipowasili mkoani Mara jana, shamrashamra za mashabiki zilikuwa kubwa hali hiyo imeendelea mpaka leo ambapo mashabiki walianza kuingia uwanjani tangu saa tatu asubuhi

Mpaka kufika saa 10 jioni huenda mashabiki ambao watachelewa wakalazimika kurudi nyumbani kuushuhudia mchezo huo runingani kwani mpaka sasa uwanja wa Karume unaelekea kujaa

Mashabiki wana shauku ya kuishuhudia Simba ambayo imetua mkoani Mara kwa mara ya kwanza baada ya kupita miaka 15

Simba yasaka alama tatu dhidi ya Biashara United leo

Kikosi cha mabingwa watetezi ligi kuu ya Tanzania Bara Simba kiko mkoani Mara ambapo leo kitashuka kwenye uwanja wa Karume kupepetana na wenyeji wao Biashara United

Baada ya ushindi dhidi ya Alliance na KMC, Simba imeingia Mara ikiwa na shauku yas kupata alama nyingine tatu ili kujisogeza zaidi kileleni mwa msimamo wa ligi

Biashara United imeweka hadharani viingilio vya mchezo huo ambapo VIP ni Tsh 20,000/- Mzunguuko Tsh 5,000/- huku watoto wakiwekewa kiingilio cha Tsh 3,000/-

Mchezo utapigwa kuanzia saa kumi kamili jioni

Kila la kheri mabingwa wa nchi…!

Mchazaji Neymar Afungiwa Mechi 3 Kutokana na Alichoandika Instagram

Shirikisho la Soka Barani Ulaya(UEFA) limemfungia mshambuliaji huyo wa Paris Saint-Germain baada ya kuandika maneno ya dharau na kejeli kufuatia timu yake kutolewa na Manchester United katika mchezo wa Klabu Bingwa Ulaya

Mbrazili huyo, aliweka bandiko katika ukurasa wake wa mtandao wa Kijamii wa Instagram lenye kuonesha hasira baada ya Man. Utd kupata penati ndani ya dakika nne za nyongeza wakati shuti lililopigwa na Diogo Dalot lilipomgonga Presnel Kimpembe mkononi

-l

Marcus Rashford alitumia nafasi hiyo aliyopewa na Muamuzi Damir Skomina aliyetoa penati hiyo baada ya kujishauri kutumia mfumo wa uamuzi wa runinga(VAR), kufunga goli na kufanya Manchester United kufuzu kucheza hatua ya robo fainali

Neyma aliandika “Hii ni aibu, wameweka watu wanne wasiojua chochote kuhusu soka kutoa maamuzi baada ya kuangalia marudio ya tukio kupitia VAR. Hakukua na penati. Panawezaje kuwa na penati wakati mpira umempiga mgogoni!” Kisha akatuna