ZAHERA AMPA ZA USO HAJI MANARA

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amemtaka Ofisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara kutofuatilia mambo yasiyomhusu.

Kauli ya Zahera imekuja kufuatia Manara kumsema kocha huyo kuwa amekuwa akiishutumu bodi ya ligi na TFF kuwa inafanya mpango wa kuiwezesha Simba kuchukua ubingwa wa ligi.

Ameeleza kwa kumtaka Manara ni vema akafuatilia mambo yanayomhusu na kuachana na kumzunguzia yeye kwani anaona anachokifanya ni sahihi.

Zahera amesema kamwe hatoweza kukaa kimya kwani kila anachokisema ni sahihi kwake na hataweza kufumbia macho madudu ya TFF.

Amefunguka kwa kusema kama TFF wanaona anakiuka taratibu wamfungie lakini hatoacha kuzungumza mpaka pale uongozi wa Shirikisho hilo utakapobadilika.

Kipigo cha Simba chafufua matumaini ya ubingwa Yanga

Baada ya Simba kupoteza mchezo dhidi ya Kagera Sugar kwa kuchapwa mabao 2-1, matokeo hayo yamefufua matumaini ya ubingwa kwa Yanga ambayo inaomba wapinzani wao hao wapoteze michezo zaidi

Aidha matokeo hayo yametoa taswira kuwa haitakuwa kazi rahisi kwa Simba kushinda michezo yote iliyobaki

Kama Yanga itashinda michezo yote sita iliyobaki itafikisha alama 92 huku wapinzani wao wakiwa na mzigo wa kupata matokeo kwenye michezo 14 ndani ya mwezi mmoja

Yanga imeendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa imejikusanyia alama 74 ikifuatiwa na Azam Fc yenye alama 66

Simba ni ya tatu ikiwa na alama 60

Azam na Yanga zimeshuka dimbani mara 32 wakati Simba imeshuka dimbani mara 24

Simba inakabiliwa na ratiba ngumu ya michezo ya viporo ambapo katika kipindi cha siku 15 itashuka dimbani mara sita

Simba yaelekea Mwanza

Baada ya mchezo dhidi ya Kagera Sugar, kikosi cha Simba kimeondoka leo Jumapili asubuhi mkoani Kagera kuelekea Mwanza tayari kwa michezo miwili ya viporo itakayopigwa jijini humo

Keshokutwa April 23 Simba itashuka uwanja wa CCM Kirumba kuchuana na Alliance Fc na siku mbili baadae, April 25 Simba itarejea kwenye uwanja huo kuchuana na KMC kisha kikosi cha mabingwa hao watetezi kitaelekea mkoani Mara kuikabili Biashara United April 28

FT : Kagera Sugar 2-1 Simba

Mabingwa watetezi ligi kuu ya Tanzania Bara Simba leo wamepoteza mchezo wa pili msimu huu baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Kagera Sugar

Kagera Sugar ilikuwa bora zaidi kwenye kipindi cha kwanza ambapo ilipachika mabao yake mawili yaliyofungwa na Kassim Khamis na Ramadhani Kapera

Simba ilikuja juu kwenye kipindi cha pili na kufanikiwa kufunga bao lake kupitia kwa Emmanuel Okwi kwenye dakika ya 64

Wekundu wa Msimbazi walikosa nafasi kadhaa ambazo zingewawezesha kuondoka na angalau alama moja dhidi ya Kagera Sugar ambayo kwa mara nyingine imedhihirisha umwamba wake dhidi ya Simba

Simba haikuwa katika kiwango bora leo, pengine uchovu uliosababishwa na timu kucheza mfululizo umechangia kukosa matokeo muhimu

Baada ya mchezo huo Simba inaelekea mkoani Mwanza ambapo Jumanne, April 23 itacheza na Alliance Fc

Heri ya sikukuu ya Pasaka kwa Wanamsimbazi

Wakristo nchini, leo wanaungana na wenzao duniani kusherehekea Sikukuu ya Pasaka ya kukumbuka ufufuko wa Yesu Kristo zaidi ya miaka 2,000 iliyopita.

Maadhimisho hayo yatakwenda sambamba na ibada kwenye makanisa mbalimbali nchini pamoja na burudani zitakazofanyika kumbi tofauti za starehe, fukwe za bahari na sehemu nyingine.

Sherehe hii ambayo kwa Wakristo huwakumbusha upendo, inatakiwa kusherehekewa katika hali ya amani na utulivu.

Tunawatakia Wanamsimbazi na Watanzania wote Pasaka Njema.

Aussems ataja kilichoiponza Simba mchezo dhidi ya Kagera Sugar

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema timu yake haikucheza vizuri kwenye kipindi cha kwanza katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar ambao Simba ilipoteza kwa mara ya pili msimu huu kwa kufungwa mabao 2-1

“Nawapongeza Kagera Sugar kwa sababu walikuwa na mchezo mzuri katika kipindi cha kwanza, sisi hatukuwa bora,” alizungumza Aussems baada ya mchezo jana

“Walitumia udhaifu wetu kuweza kufunga mabao mawili ambayo kwetu haikuwa rahisi kuyarejesha yote kwenye kipindi cha pili licha ya kurekebisha makosa tuliyofanya kwenye kipindi cha kwanza”

“Wachezaji wangu walicheza dakika 45 za kipindi cha pili na kufanikiwa kufunga bao moja na kutengeneza nafasi nyingine ambao tulishindwa kuzitumia. Hata hivyo mchezo ni dakika 90”

Baada ya mapumziko ya Pasaka, Simba itaelekea mkoani Mwanza kuikabili Alliance Fc kwenye mchezo mwingine wa ligi utakaopigwa keshokutwa April 23 katika dimba la CCM Kirumba

SIMBA YANYUKWA NA KAGERA SUGAR BAO 2-1