
Simba inakwenda Algeria kuumana na JS Saoura kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa raundi ya tano utakaopigwa Jumamosi March 09, saa nne usiku kwa saa za Afrika Mashariki

Simba inakwenda Algeria kuumana na JS Saoura kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa raundi ya tano utakaopigwa Jumamosi March 09, saa nne usiku kwa saa za Afrika Mashariki
Hali ya mshambuliaji hatari wa Simba Emmanuel Okwi imeshindwa kulishawishi benchi la ufundi ambapo ameondolewa katika kikosi cha wachezaji 20 kilichoondoka jioni ya leo Jumanne March 05 2019 kuelekea nchini Algeria
Pamoja na kuuguza jeraha la chini ya jicho, Okwi alipata maumivu ya goti kwenye mchezo dhidi ya Lipuli Fc na kulazimika kurudishwa jijini Dar es salaam kutibiwa wakati kikosi cha Simba kikielekea mkoani Shinyanga kuikabili Stand United
Hata hivyo yaonekana hali yake haikutengemaa na benchi la ufundi kulazimika kumuondoa kikosini
Kikosi kilichosafiri;
Aishi Manula,
Zana Coulibaly
Nicholas Gyan
Asante Kwasi
Mohammed Hussein
Pascal Wawa
Poul Bukaba
James Kotei
Jonas Mkude
Mzamiru Yassin
Hassan Dilunga
Cletus Chama
Rashid Juma
Abdul Selemani
John Bocco
Maddie Kagere
Adam Salamba
Deo Munishi
Asante Kwasi
Mohammed Ibrahim
Haruna Niyonzima.
Shomari Kapombe anatarajiwa kurejea Afrika Kusini wiki hii kwa ajili ya vipimo vya mwisho kabla ya kuruhusiwa kuanza mazoezi mepesi. Pichani Kapombe akizungumza na Afisa Mtendaji Mkuu Crescentius Magori. #NguvuMoja
Jumamosi ya wiki hii Simba itakuwa ugenini nchini Algeria ikichuana na JS Saoura katika mchezo ambao huenda ukaifanya Simba iandike historia nyingine barani Afrika
Kikosi cha Simba kinatarajiwa kuondoka baadae leo kuelekea Algeria ambapo Aussems amesema wanakwenda kusaka alama tatu
“Kwa nini tufikirie sare badala ya ushindi? tunaenda Algeria kupambana kupata ushindi ambao kwa kweli utakuwa umetuweka karibu kabisa na kufuzu hatua ya robo fainali ambayo ndio malengo yetu kwa sasa,” amesema Aussems.
Aussems amesema wapo tayari kwa mchezo huo kwani michezo waliyocheza karibuni katika ligi imewasaidia kujiimarisha zaidi
Baada ya mchezo dhidi ya JS Saoura ugenini, Simba itarejea nyumbani kujiandaa na mchezo wa mwisho dhidi ya AS Vita utakaochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Machi 19
Kama Simba itashinda mchezo huo utakaopigwa saa nne usiku halafu AS Vita Club ikashindwa kuifunga Al Ahly kwenye mchezo wa mapema utakaopigwa saa moja usiku, basi mabingwa hao wa Tanzania watajihakikishia kuwa miongoni mwa timu nane zitakazotinga robo fainali
Leo jioni kikosi kitaondoka kuelekea nchini Algeria kwa kupitia Dubai, UAE ambako kitacheza mchezo wa tano wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya JS Saoura, mchezo ambao utachezwa siku ya Jumamosi Machi 9, 2019. Tuikumbuke timu yetu kwenye dua ili ifike salama na ifanye vizuri katika mchezo huo muhimu. #NguvuMoja

Kagere amewataka mashabiki kuiombea na kuiunga mkono timu kwa hali na mali ili kuhakikisha inatinga robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa
“Nawaambia wote wenye mapenzi mema na Simba, wale wanaoamini kuwa tunaweza kutinga robo fainali, nusu fainali na hata fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa, waungane nasi kwa kutuombea ili tuweze kufanikiwa,” amesema Kagera katika ujumbe mfupi alioutuma kwa mashabiki wa Simba
Simba inatarajiwa kwenda Algeria siku chache zijazo tayari kwa mchezo huo dhidi ya JS Saoura utakaopigwa Jumamosi, March 09

Leo Meddie Kagere anatarajiwa kuiongoza safu ya ushambuliaji ya Simba kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Stand United utakaopigwa uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga
Kagere mwenye mabao 12, yuko katika kiwango bora cha upachikaji mabao, akifunga mfululizo kwenye michezo mitano iliyopita
“Kazi yangu mimi ni kufunga, hivyo nitaendelea kufanya hivyo kila ninapopata nafasi ili niisaidie timu yangu iweze kupata ushindi,” alisema Kagere baada ya mazoezi ya jana
Kagere ndiye mchezaji hatari zaidi katika ligi kuu ya Tanzania Bara kwa sasa kutokana na kuwa na wastani mzuri wa kufunga kulingana na uwiano wa michezo aliyocheza

Hiki hapa kikosi cha Simba kinachoanza;


Okwi alipata majeraha madogo kwenye mchezo dhidi ya Lipuli Fc. Lakini pia Okwi alicheza mchezo huo huku akiwa amefungwa bandeji chini ya jicho kutokana na jeraha la kuchanika alilopata kwenye mchezo dhidi ya Azam Fc
Baada ya mchezo wa Lipuli Fc, Okwi alirejeshwa jijini Dar es salaam kwa ajili ya matibabu zaidi
Hata hivyo taarifa za uhakika ni kuwa kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amempa mapumziko mshambuliaji huyo wa Kimataifa wa Uganda ili aweze kupona kabisa majeraha yake tayari kwa mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya JS Saoura
Baada ya mchezo dhidi ya Stand, Simba itasafiri kwenda Algeria kuikabili JS Saoura kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa hatua ya makundi, raundi ya tano utakaopigwa Jumamosi ijayo, March 09 2019
Simba inahitaji angalau pointi moja tu ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga robo fainali ya michuano hiyo
Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema timu yake imefuata alama tatu mkoani Shinyanga hivyo iko tayari kwa mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Stand United utakaopigwa kesho Jumapili kwenye uwanja wa CCM Kambarage
Simba iliweka kambi ya siku mbili mkoani Singida kabla ya kutua Shinyanga hapo jana
Aussems amesema anatambua mchezo huo hautakuwa mwepesi lakini kama walivyofanya katika michezo iliyopita, lengo lao ni kuondoka na alama zote tatu
Juzi kocha wa Stand United Athuman Bilali ‘Bilo’ alitamba kuwa timu yake itaibuka na ushindi katika mchezo huo ambapo alisema Simba ni timu ya kawaida kama zilivyo Ndanda Fc, Mwadui Fc na timu nyingine zinazoshiriki ligi kuu
“Tumewafuata Stand United, tunajua kila timu sasa inajiandaa kuonyesha ushindani itakapocheza na sisi, tunajua hilo, lakini mipango yangu ni kuhakikisha tunashinda mechi hii ya Jumapili, tuko tayari,” alisema Aussems jana baada ya kutua mkoani Shinyanga
Jana jioni kikosi cha Simba kilijifua mkoani Shinyanga kujiandaa na mchezo huo ambao ushindi utazidi kuisogeza Simba kileleni