HAJI MWINYI: Ajiandaa na Maisha Nje ya YANGA

Beki Haji Mwinyi ni miongoni mwa wachezaji wa Yanga ambao mikataba yao inamalizika baada ya mchezo wa mwisho wa ligi

Beki huyo aliyeitumikia Yanga kwa zaidi ya miaka minne, atakuwa huru baada ya Yanga kuumana na Azam Fc wiki ijayo

Amezikaribisha timu zinazohitaji huduma yake kwa ajili ya msimu ujao

“Mkataba wangu na Yanga unamalizika msimu huu. Baada ya hapo nitakuwa huru”

“Nakaribisha klabu yeyote inayohitaji huduma yangu kwa msimu ujao waje tukae mezani tuzungumze, lakini kuhusiana na ofa nilizonazo mezani hadi sasa siwezi kuweka wazi hadi hapo nitakapomaliza msimu wangu kwa michezo miwili iliyobaki,” Mwinyi aliiambia Mwanaspoti

“Sikuwa na namba kikosi cha kwanza, lakini hiyo haina maana kwamba kiwango changu kimeshuka, nipo vizuri na nina uwezo wa kupambana. Kutokana na uzoefu nilionao na naweza kucheza timu yeyote”

Haji Mwinyi hakuwa na wakati mzuri msimu huu katika kikosi cha Zahera akishindwa kutamba mbele ya Gadiel Michael aliyekuwa chaguo la kwanza

Yanga imepanga kutowaongezea mikataba wachezaji ambao hawakucheza angalau nusu ya michezo ya ligi kuu msimu huu

USAJILI: Klabu ya Raja Casablanca ya Morocco 🇲🇦 Imethibitisha kukamilisha Usajili wa kiungo fundi, Fabrice Luamba Ngoma

OFFICIAL! – Klabu ya Raja Casablanca ya Morocco 🇲🇦 Imethibitisha kukamilisha Usajili wa kiungo fundi, Fabrice Luamba Ngoma kutoka Miamba wa Kinshasa, Klabu ya AS Vita Club 🇨🇩.
.
– Kiungo huyo wa Kimataifa wa DR Congo, amesaini Mkataba wa Miaka Mitatu kuwatumikia Miamba hao Baada ya kudumu Kinshasa kwa Misimu miwili.
#transfers

ZAHERAC: Amlilia AJIBU Kwenda TP MAZEMBE

Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera amemwambia nahodha na mshambuliaji wa klabu hiyo Ibrahim Ajibu kufikilia mara mbili kuhusu kuihama klabu hiyo mwisho wa msimu huu. Imeelezwa.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Zahera amedai Ajibu ni kiongozi wa wenzake na hapaswi kuwa na mawazo ya kuondoka Yanga na kuwaacha wenzake.

Mkataba wa Ajibu na Yanga unaisha mwisho wa msimu huu na inadaiwa kuwa atajiunga na klabu ya Simba baada ya mkataba wake kuisha na Yanga.

Taarifa za Ajibu kuondoka Yanga zimeanza muda mrefu uliopita na kuleta sintofahamu kwa wapenzi na mashabiki wa timu hiyo kutokana na namna mwenendo wa klabu ulivyo.

Zahera amemuomba Ajibu afikirie zaidi ya mara moja kuhusiana na kuondoka kwake kwa manufaa ya Yanga maana anaheshimu mchango wake.

AJIBU Kutimkia TP MAZEMBE

TP Mazembe itamsajili kiungo wa Yanga Ibrahim Ajib Migomba akitarajiwa kujiunga na timu hiyo Julai 01 2019

TP Mazembe imeiandikia barua Yanga kuitaarifu juu ya nia ya kutaka kumsajili kiungo huyo.

Mazembe itamsajili Ajib baada ya kumaliza mkataba na Yanga

Aidha TP Mazembe imeiomba Yanga impe ruhusa ya siku tatu wiki hii ili aweze kwenda Congo kukamilisha taratibu za usajili

Hii ni habari njema kwa Ajib ambaye msimu huu umekuwa mzuri sana kwake

Ajib ameifungia Yanga mabao sita na kutengeneza mabao 17 kwenye ligi kuu ya Tanzania Bara inayoelekea ukingoni

IBRAHIM AJIBU AMALIZANA NA TP MAZEMBE.

Nahodha wa Klabu ya Yanga SC, Ibrahim Ajib anatarajia kujiunga na Mabingwa wa DR Congo, Miamba wa Lubumbashi Klabu ya TP Mazembe kwa uhamisho huru Baada ya Mkataba wake na Klabu yake ya Jangwani kufikia tamati mwishoni mwa mwezi Ujao.. 👏👏👏.
#transfers
.

Klabu ya TP Mazembe imeiandikia barua Yanga kuwaeleza kuwa wamefanya makubaliano ya kuingia mkataba na Ibrahim Ajibu utakaoanza rasmi Julai 1.

Hiyo ni baada ya Mazembe kujiridhisha kuwa mkataba wa mchezaji huyo na Yanga unaisha Juni 30.

Taarifa hii inaua matumaini ya Wanajangwani hao kuendelea kuwa na fundi huyo wa mpira msimu ujao huku ikizima tetesi za kurejea Simba.

#TransferUpdates

TSHISHIMBI: Aipotezea Azam Fc

Wakati mkataba wake ukielekea ukingoni, kiungo Papi Kabamba Tshishimbi amesema hafikiri kujiunga na timu nyingine Tanzania kama atashindwa kufikia makubaliano na Yanga

Tshishimbi aliyetua Yanga miaka miwili iliyopita akitokea Mbabane Swallows ya eSwatini, amekuwa akihusishwa kuwaniwa na Azam Fc

Hata hivyo amesisitiza Yanga ndio timu pekee ambayo atachezea kwa hapa Tanzania

“Mimi ni mchezaji wa Yanga na hata mkataba utakapomalizika timu nitakayofanya nayo mazungumzo ni Yanga,” amesema

“Ni kweli zipo timu zimewasilisha ofa, lakini nitazungumza na Yanga kwanza kama tukishindwana basi nitazipa kipaumbele ofa za nje ya Tanzania”

Kwa siku za hivi karibuni Tshishimbi amekuwa katika kiwango bora akiwa amefunga mabao manne kwenye ligi kuu ya Tanzania Bara

Hakuna shaka atakuwa miongoni mwa wachezaji watakaopewa mikataba mipya katika kikosi cha Yanga

TETESI ZA USAJILI SIMBA LEO JUMANNE

Tetesi za usajili Simba leo 21 May 2019

Kikosi cha Simba leo huenda kikatangaza ubingwa kikicheza kwenye ardhi ya Singida katika uwanja wa Namfua, Simba inahitaji walau sare tu ili kuweza kutangaza Ubingwa mbele ya Singida United wanaohitaji ushindi ili kujihakikishia kuendelea kusalia ligi kuu.

Ukiachana na hayo ya Simba kushinda inaelezwa kuwa kikosi cha Simba kinaendelea kutafuta wachezaji wakuimarisha kikosi chao kwaajili ya msimu ujao.

Kama ulijisahaulisha, mchezaji Vitalis Mayanga wa Ndanda inaelezwa kuwa ni suala la muda tu kutua Simba kwani Simba na Ndanda walishamalizana muda tu na kijana anasubiri ligi iishe waweze kumjumuisha kikosini.

Vitalis Mayanga licha ya kuwa akitajwa kuwaniwa na baadhi ya vilabu nchini Tanzania Yanga ikitajwa lakini imebainika ni mchezaji halali wa Simba anayesubiria ligi iishe aungane na mabingwa hao wa soka nchini.
Credit: Kwataunit

KENNY ALLY: Huru Kutua Jangwani #YANGA

Kiungo wa Singida United Kenny Ally ni miongoni mwa wachezaji wanaotajwa kuwaniwa na Yanga kwa ajili ya msimu ujao

Kenny anaweza kutua Yanga akiwa mchezaji huru kwani mkataba wake na Singida United unamalizika mwishoni mwa msimu huu

Uongozi wa Singida United umesema hauna pingamizi kwa kiungo huyo kama atapenda kujiunga na Yanga kwa kuwa maamuzi ni yake, mkataba wake uko ukingoni

“Kenny atakuwa huru kujiunga na timu yeyote baada ya ligi kumalizika, hivyo kama Yanga wanamuhitaji wazungumze nae,” amesema Cales Katemana ambaye ni msemaji wa Singida United

Yanga imedhamiria kuunda kikosi cha ushindani kwa ajili ya msimu ujao

Tayari michakato ya usajili imeanza kimyakimya