Mshambuliaji wa Azam Fc Obrey Chirwa amegoma kusaini mkataba mpya kunako klabu hiyo mpaka mwishoni mwa msimu
Azam Fc imekuja na utaratibu tofauti wa kuwaongezea mikataba wachezaji wake kabla ya mikataba yao ya awali kumalizika
Timu hiyo tayari imewapa mikataba wachezaji wake waandamizi isipokuwa Chirwa aliyejiunga na timu hiyo kwa mkataba wa miezi sita wakati wa dirisha dogo la usajili
Hivi karibuni kocha Mwinyi Zahera alieleza kuvutiwa na kiwango cha mshambuliaji huyo raia wa Zambia
Zahera alisema Chirwa ni bonge la mchezaji, lakini alikataa kuweka wazi kama anaweza kumrejesha tena kikosini kwa ajili ya msimu ujao
Alitaja hali ngumu ya kiuchumi Yanga ilikuwa sababu ya yeye kukataa asisajiliwe aliporejea kutoka Misri mwishoni mwa mwaka jana
“Chirwa ni mchezaji mkubwa na anapambana sana katika uchezaji wake hata kwa mechi nilizomuona ana kitu ambacho wengine hawana, ila nilimkataa kwa kuwa hawezi kuvumilia matatizo,” alisema
Streka wa PSG na Ufaransa Kylian Mbappe, 20, amebainisha kuwa anaweza kuihama klabu yake katika kipindi hiki cha usajili. Kauli hiyo inatarajiwa kuziamsha klabu kongwe na tajiri kama Real Madrid, Barcelona na Manchester City kumgombea. (Express)
Kiungo raia wa Ujerumani Ilkay Gundogan, 28, anataka kurudi mezani na klabu yake ya Manchester City kwa malengo ya kusalia klabuni hapo zaidi ya mwezi Juni 2020 ambapo mkataba wake wa sasa unaishia. (Mail)
Kocha Pep Guardiola atapewa fursa ya kusalia klabuni Manchester City walau kwa miaka mitano ijayo huku kipato chake kikifikia pauni milioni 100, baada ya mshahara wake kwa mwaka kuchupa toka pauni milioni 15 mpaka milioni 20. (Sun)
Kiungo wa kimataifa wa Ubelgiji Yannick Carrasco, 25, ambaye anakipiga kwenye ligi kuu ya Uchina, klabu ya Dalian Yifang, anataka kuhamia katika ligi ya Primia na Arsenal wanatarajiwa kumnyemelea, klabu hiyo ilikaribia kumsajili katika dirisha dogo la usajili la Januari. (Sun)
Arsenal pia wanamnyemelea beki wa kati na kinda wa timu ya Saint-Etienne na timu ya taifa ya chini ya miaka 19 ya Ufaransa, William Saliba, 18. (Goal.com)
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionSanchez amekuwa na wakati mgumu na United tofauti na alipokuwa Arsenal
Mshambuliaji aliyepoteza kiwango wa Manchester United na Chile Alexis Sanchez, 30, anatarajiwa kukatiza mapumziko yake ya mwisho wa msimu na kurudi klabuni ili kujifua na kujihakikishia nafasi katika kikosi cha United. (Sun)
Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane amemwonesha dalili za wazi winga raia wa Wales Gareth Bale, 29, kuwa muda wake katika klabu hiyo umefikia tamati, baada ya kusema kuwa asingemuingiza mchezoni kutoka benchi walipofungwa Jumapili na Real Betis hata kama kungekuwa na fursa ya kuingiza wachezaji wanne. (Eurosport)
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionBale ‘agoma’ kuhama Real Madrid mpaka mkataba wake utakapoisha
Bale hata hivyo amewaambia wachezaji wenzake kuwa anapanga kusalia klabuni hapo mpaka kwisha kwa mkataba wake na takuwa mwenye furaha kucheza gofu endapo hatapangwa kucheza. (Radioestadio, via Mail)
Kiungo wa Chelsea na Ufaransa N’Golo Kante, 28, anapiga hessabu za kuikacha klabu yake na kujiunga na miamba ya Ligi ya Ufaransa PSG. (Talksport)
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Manchester United watarasimisha nia yao ya kumsajili kiungo wa Lyon, Tanguy Ndombele, 22, pale tu mustakabali wa kiungo wao Paul Pogba, 26, utakapokuwa wazi. (Manchester Evening News)
Kocha wa Lille, Christophe Galtier amethibitisha kuwa winga raia wa Ivory Coast winger Nicolas Pepe, 23, ataihama klabu hiyo hivi karibuni. Mcezaji huyo anahusishwa na uhamisho na klabu kongwe za Manchester United, Arsenal na Bayern Munich. (Manchester Evening News)
KUNA kila dalii kwamba, endapo straika Heritier Makambo wa Yanga atakamilisha dili lake la kujiunga na klabu ya Horoya FC ya nchini Guinea, basi mkali mwingine raia wa Ghana ataziba nafasi yake.
Anayetajwa kuziba nafasi hiyo ni Mnamibia anayekipiga katika klabu ya Lusaka Dynamos ya Zambia, Petrus Shitembi, anayetajwa kuwa hatari katika nafasi ya kiungo mshambuliaji.
Kiungo huyo alisajiliwa na Lusaka Dynamos siku chake baada ya Clatous Chama kusajiliwa na Simba ili kuziba pengo lake kutokana na uwezo mkubwa alionao.
Simba walimsajili Chama kutoka klabu hiyo na kwa haraka nao hawakulaza damu, wakamchukua Shitembi ambaye naye ameingia kwenye rada za Yanga.
Kigogo mmoja wa Yanga amefunguka kuwa kiungo huyo ambaye ana uwezo mkubwa wa kutoa pasi za uhakika na kufunga mabao muhimu, ameshaingia kwenye 18 zao na kilichobakia ni kumalizana tu.
“Ni kweli Makambo ameondoka lakini hiyo haimaanishi kwamba Yanga inakufa. Tumeshaanza harakati za usajili na muda si mrefu tutamalizana na kiungo kutoka Namibia.
“Ni moja ya viungo wazuri na yeye hana tabu yoyote kuja Yanga. Nadhani ataungana na wachezaji wengine ambao tutawasajili kwani dhamira yetu ni kuisuka klabu yetu upya ili msimu unaokuja tuwakate kilimilimi wapinzani wetu,” alisema.
Alisema kiungo huyo ni moja ya wachezaji wanane wa kigeni ambao kocha wao mkuu, Mwinyi Zahera, alidai atawasajili, huku akisema kuna mastraika wengine watatu kutoka nchi tofauti.
“Wapo pia mastraika watatu tunaendelea na mazungumzo nao, hiyo kazi inafanywa na kocha wetu, nadhani baada ya kuondoka Makambo, tutashusha mashine nyingine hatari zaidi,” alisema.
Kiungo huyo alianza soka katika timu ya Rundu Chiefs ya nchini kwao Namibia kabla ya kwenda Afrika Kusini ambako alijiunga na University Of Pretoria na baadaye kwenda Ghana kuichezea Ashanti Gold kabla ya kurudi tena na kuzichezea Amazulu FC na Stellenbosch FC na baada ya kuondoka Chama akasajiliwa Lusaka Dynamos kuziba pengo lake.
Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema mchakato wa usajili wa mshambuliaji Heritier Makambo uko katika mikono salama
Aidha Mwakalebelea amesema Yanga imepokea ofa nyingi zinazomuhusu mshambuliaji huyo
Amesisitiza bado hakuna mkataba uliosainiwa upande wa Yanga, hivyo amewahakikishia Wanayanga kuwa Makambo bado ni mchezaji wao halali
“Suala la Makambo liko mikono salama, uongozi tunalifahamu na tulitoa baraka zetu kwake pamoja na Mwalimu kwenda Guinea ambako alitakiwa kwenda kufanyiwa vipimo vya afya,” amesema
“Ilikuwa ni lazima aende na Mwalimu kwa sababu kule wanaongea kifaransa”
“Lakini ifahamike Makambo ana ofa nyingi, sio Horoya Fc pekee wanaotaka kumsajili, Jumatatu tutakutana na wengine”
“Tunazipitia ofa zote na kufanya tathmini kabla ya kuamua. Hakuna mkataba ambao umeshasainiwa kwa upende wetu. Na kwa kawaida mkataba lazima uwe wa pande mbili”
“Mpira ni biashara, kama kutakuwa na ofa nzuri tutafanya biashara lakini kama itakuwa tofauti basi tutaendelea kubaki na mchezaji wetu”
Imeripotiwa kuwa uongozi wa klabu ya Azam FC ya Dar Es Salaam umesitisha mazungumzo ya mkataba mpya na nyota wake Obrey Chirwa.
.
.
Taarifa za awali kutoka ndani ya uongozi wa klabu hiyo zinasema watafanya uamuzi wa kuendelea au kutoendelea na Chirwa mara baada ya fainali ya kombe la shirikisho la ASFC.
Simba tayari imeanza mchakato wa kuhuisha mikataba ya wachezaji wake ambayo inamalizika mwishoni mwa msimu
Baada ya kumalizana na nahodha John Bocco, inaelezwa mshambuliaji Emmanuel Okwi na Jonas Mkude wako katika mazungumzo na uongozi wa Simba ili kuhuisha mikataba yao
Wachezaji hao wanadaiwa kunyemelewa na timu nyingine hivyo kuulazimu uongozi wa Simba kuharakisha kuwapa mikataba mipya
Okwi amekuwa akihusishwa na timu kadhaa kutoka Afrika Kusini, ambapo mwezi Januari Kaizer Chiefs iliwasilisha ofa kwa klabu ya Simba lakini uongozi ‘ukaipiga chini’
Mkude anatajwa kuwaniwa na timu kadhaa kutoka Arabuni
Wachezaji wengine ambao wako katika mipango ya mwalimu na watasaini mikataba mipya pia
Aidha Simba huenda isifanye mabadiliko makubwa ya kikosi chake hasa kwa wachezaji wa ndani baada ya Aussems kuagiza waliopo waongezewe mikataba kwa kuwa nje ya Simba hakuna wachezaji wengi bora
Wachezaji wa ndani wanaotajwa kujiunga na Simba kwa ajili ya msimu ujao ni pamoja na Vitalis Mayanga kutoka Ndanda Fc.
Mayanga alisajiliwa kwa ajili ya michuano ya CAF lakini taarifa zake zikachelewa kutumwa
Wengine ni Ibrahim Ajib kutoka Yanga na Beno Kakolanya (huru)
✍🏼 Kujenga kikosi ndani ya Manchester United kumeanza, Miamba hao wa Old Trafford Rasmi imewasiliana na klabu ya Fulham mara moja juu ya kutaka kumsajili kinda wao, Ryan Sessegnon.
:
✍🏼 United itakutana na Upinzani kwani, Tottenham na Juventus pia wanavutiwa na kijana huyo, ambaye leo anatimiza umri wa miaka 19, lakini United ni timu pekee ambayo imetuma maombi yao kuwasiliana na Fulham hadi sasa.. Kwa mujibu wa chanzo makini @skysports.
:
✍🏼 Sessegnon inaeleweka kuwa hawezi kucheza msimu mwingine katika Championship kufuatia Fulham kushuka daraja ikiwa ni msimu mmoja tangu wapande Premier league, United wanataka kuongeza vipaji kwa kusajili wachezaji vijana katika kikosi cha kocha Ole Gunnar Solskjaer..
:
✍🏼 Fulham huenda wakakubali kufanya Biashara ya kumuuza Sessegnon kwa vilabu vinavyomtaka kwani kinda huyo kabakiza Mkataba wa Mwaka mmoja tu kuwatumikia watoto hao wa London..
#transfers #Updates #premierleague
@Sokawaytz
Mshambuliaji wa Chelsea aliyepo kwa mkopo Atletico Madrid Alvaro Morata amesema kuwa hafikirii kurejea Chelsea baada ya muda wake kumalizika badala yake atafanya kila aliwezalo ili aendelee kubaki Atletico Madrid kwa muda mrefu.
.
Baada ya kuondoka kwa Heritier Makambo, klabu ya Yanga Sc imeanza kuwania saini ya mshambuliaji wa Coastal Union Ayoub Lyanga ili kurithi mikoba Makambo.
.
Lyanga ameifungia mabao 10 klabu yake ya Coastal mpaka sasa kunako Ligi Kuu Tanzania Bara.
Klabu ya Simba inaendelea na mchakato wa kuhuisha mikataba ya wachezaji wake ambayo inamlizika na tayari imemalizana na nahodha wake John Bocco
Taarifa za uhakika ni kwamba Bocco amesaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kukipiga Msimbazi hadi mwaka 2021
Bocco aliyeifungia Simba mabao 15 kwenye ligi ya Tanzania Bara msimu huu, alikuwa akiwaniwa na timu yake ya zamani Azam FC
Azam Fc inadaiwa kuwashawishi Aishi Manula, Erasto Nyoni, John Bocco na Shomaria Kapombe wasaini kunako klabu hiyo waliyokuwa wakicheza kabla ya kusajiliwa na Simba mwaka juzi
Msimu uliopita Bocco aliibuka kuwa mchezaji bora wa Simba na msimu huu ameteuliwa kuwania tuzo hiyo sambamba na Meddie Kagere na Clatous Chama
Zoezi la kuchagua mchezaji bora wa msimu huu tayari limeanza, kura zinapigwa kupitia tovuti rasmi ya Mo Simba Awards
BonyezaHAPAkumpigia kura Bocco kama unadhani anastahili kuwa mchezaji bora wa Simba msimu huu