TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA LEO IJUMAA NOV 23, 2018.
1.ARSENAL inamnyatia nyota kinda wa As Roma Mturuki, Cengiz Under ambaye pia anatakiwa na Manchester City. (#Calciomercato).
2.ARSENAL pia inamtaka Kiungo wa Borussia Dortmund, Julian Weigl. (#SportsBild).
3.SEVILLA itamnunua jumla Mshambuliaji wa Ureno, Andre Silva kwa pauni €35m ambaye anaichezea kwa mkopo klabu hiyo kutoka Ac Milan.(#Goal).
4.JUVENTUS inataka huduma ya Kiungo Mshambuliaji wa Wolves, Ruben Neves. (#Tuttosport).
5.CHELSEA imeungana na Manchester United kuisaka saini ya Beki wa kati wa Inter Milan, Milan Skriniar mwenye thamani ya pauni £70m. (#TheSun).
6.MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Marcus Rashford ameripotiwa ataanza mazungumzo na Real Madrid ya kuhamia Santiago Bernabeu. #TheSun imeripoti.
7.HOFFENHEIM inamtaka Mshambuliaji wa Brighton, Aaron Connolly. (#SkySportNews).
8.PSG imeungana na Man City pamoja na Barcelona kuiwania saini ya Kiungo wa Ajax, Frenkie De Jong. (#Sport).
9.WEST HAM inataka kumsajili Mshambuliaji wa Bayern Munich, Sandro Wagner. (#TheSun).
10.KOCHA wa Man United, Jose Mourinho anawasaka Beki wa Atletico Madrid, Diego Godin, Gary Cahill na Kiungo wa As Roma, Lorenzo Pellegrin. Mreno huyo inadaiwa amepewa pauni£300m za usajili katika dirisha la January. (#DailyStar).
10.REAL MADRID itajaribu kuisaka saini ya Mshambuliaji wa Inter Milan, Mauro Icardi katika dirisha la January. (#OKdiario).
11.REAL MADRID imerudi tena ufaransa ikimtaka Fowadi wa PSG, Neymar huku Mbrazil huyo akifungua milango ya kurudi Barcelona. (#COPE).
12. REAL MADRID itamtoa Winga wake, Gareth Bale pamoja na pauni €100m kwa Chelsea kama chambo ya kumnasa Eden Hazard. (#OKDiario).
13.ARSENAL itamtumia Fowadi wake, Pierre Aubameyang ili amshawishi Winga wa Barcelona, Ousmane Dembele ajiunge Emirates. (#Sport).










