Yanga wasaini chombo kingine

credit: @sokawaytz…

– Mlinda lango wa timu ya taifa ya Tanzania, Metacha Mnata 20″ amejiunga na Klabu ya Yanga SC kwa Kusaini Mkataba wa miaka miwili, Nyada huyo kajiunga na Yanga akitokea kuitumikia Klabu ya Mbao FC kwa mkopo ambapo Sasa kamaliza Mkataba wake na Azam FC..

.

– Usajili mwingine tena Jangwani, Mshambuliaji wa Kimataifa, Maybin Kalengo 20″ nae amesinyaa rasmi Mkataba wa Miaka Miwili kuwatumikia miamba hao msimu ujao.. Kalengo katoka kuitumikia Klabu ya ZESCO United ya kwao Zambia..

#transfers

@Sokawaytz

Bakambo aondoka rasmi yanga

credit: @sokawaytz…

MAKAMBO AONDOKA RASMI YANGA

Straika Heritier Makambo ameaga na kuondoka rasmi nchini tayari kujiunga na timu yake mpya ya Horoya AC ya nchini Guinea huku uongozi wa Yanga ukimpa Baraka zake.

.

.

“Tunakutakia kila lakheri Heritier Makambo kwenye majukumu yako mapya huko uendako tunatambua na tunathamini sana mchango wako kwenye klabu yetu” – Yanga.

@heritier_ebenezer @yangasc @horoyaac

Zahera simuachi yondani ng’oo

— “Mimi na Yondani mbona tuna mawasiliano mazuri kabisa, akiwa na matatizo yake ananiambia na tunajua tunafanyeje hata hayo anayosema kwamba anagoma kiukweli mimi sifahamu”.

— “Iko hivi mchezaji huyu hawezi kuondoka na nawaambia atazeekea hapa hapa, kwahiyo hayo maneno ya mtaani wala msiyasikilize,”.

👉 Kocha Mkuu wa Yanga SC akiweka wazi kuwa beki kisi wa Klabu hiyo, Kelvin Yondani atacheza Yanga mpaka yeye mwenyewe atakapoamua kusema basi amechoka na anahitaji kupumzika katika Masuala ya Soka.

#Updates

credit: @sokawaytz

Yanga wanasa chuma kingine Rwanda

– Klabu ya Yanga SC imefikia Makubaliano ya kuingia Mkataba wa Miaka Miwili na Mshambuliaji wa Kimataifa wa Rwanda, Issa Bigirimana.

.

– Bigirimana Mzaliwa wa Burundi lakini anaitumikia timu ya taifa ya Rwanda, amemwaga wino wa Mkataba wa Miaka Miwili kuwatumikia Miamba wa Mitaa ya Jangwani akitokea katika Klabu ya APR FC ya Ligi Kuu Nchini kwao Rwanda.

.

– Bigirimana 23, anakuwa Mchezaji wa Pili kusinyaa Baada ya Jana, Kiungo Ambaye Pia ni wa Rwanda kutoka Klabu ya Mukura Victory, Patrick Sibomana kumwaga wino.. Haya yote ni kuijenga Yanga mpya ya Ushindani kwa msimu ujao 2019/20..

#transfers #Updates

@Sokawaytz

credit: @sokawaytz

Yanga yakamilisha usajili wa kiungo mnyaruanda Patrick papy sibomana

✍🏻 Kumekucha Jangwani, Klabu ya Yanga SC Imekamilisha Usajili wa kiungo wa Kimataifa wa Rwanda, Patrick Papy Sibomana kwa Mkataba wa Miaka Miwili akitokea Klabu ya kwao Rwanda, Mukura Victory.

:

✍🏼 Sibomana 22, Aliwahi kuitumikia Klabu ya APR FC ya kwao Rwanda, mwaka 2017 akasaini Mkataba wa kuitumikia Klabu ya Shakhtyor Soligorsk ya Nchini Belarus kisha kurejea Rwanda mwaka huu na kutua Mukura na kisha Sasa Yanga SC ya Tanzania.

:

✍🏼 Nyota huyu ni Miongoni mwaka Wachezaji wanaounda timu ya taifa ya Rwanda “Amavubi” akiichezea timu hiyo tangu mwaka 2013 mpaka Sasa, Kafunga Magoli mawili na Moja ya Goli lake aliifunga Taifa Stars katika Mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki Tanzania ikipoteza 2-0 mwaka 2015 ndani ya Dimba La Amahoro Stadium, Kigali..

#Updates #transfers

@Sokawaytz

credit: @sokawaytz

YONDANI: Amtibua ZAHERA

Kikosi cha Yanga leo kimeendelea na mazoezi kwenye uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo wa mwisho wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Azam Fc utakaopigwa Jumanne, May 28 dimba la Uhuru

Kocha Mkuu wa mabingwa hao wa kihistoria Mwinyi Zahera amesema baadhi ya wachezaji waliokuwa wagonjwa wameanza kurejea kikosini

“Paul Godfrey alikuwa mgonjwa lakini leo ameanza mazoezi. Dante, Abdul, Ngasa, Banka, Jaffar na Ajib bado wagonjwa,” amesema

Katika hatua nyingine Zahera amemuagiza Meneja wa Yanga Nadir Haroub kumsaka beki wa timu hiyo Kelvin Yondani ambaye haonekani mazoezini

Zahera amesema hana taarifa kama Yondani ni mgonjwa, amejaribu kumpigia simu bila ya mafanikio

“Sina taarifa za Yondani, nimejaribu kumpigia simu lakini hapokei, tumemtuma Meneja (Nadir) aende akamtafute kwake anipe mrejesho kabla sijafanya maamuzi,” Zahera aliiambia eFM

KAMUSOKO -:Aaga wachezajinyanga

Kiungo mkongwe Thabani Kamusoko yuko Zimbabwe na kikosi cha timu ya Taifa kinachojiandaa na fainali za AFCON 2019 zitakazofanyika mwezi ujao nchini Misri

Ni kama kiungo huyo hatarejea tena Yanga baada ya jana kuwaaga wachezaji wenzake wa kikosi cha Yanga

“Nimewakumbuka sana rafiki zangu, sina neno jingine la kusema zaidi kwani mlikua zaidi ya marafiki,” ameandika Kamusoko ukurasa wake wa Instagram

Kamusoko ni miongoni mwa wachezaji ambao mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu, hatma yake ikibaki mikononi mwa kocha Mwinyi Zahera

Keshokutwa Jumanne baada ya mchezo dhidi ya Azam Fc, Yanga itatangaza majina ya wachezaji ambao wameachwa pamoja na wale ambao tayari wamesajiliwa na timu hiyo

Zahera amesema kuna wachezaji nane ambayo tayari wamesajiliwa na timu hiyo, sita wa Kimataifa na wawili wazawa

Sitaingilia Majukumu ya Zahera – Dk Msolla

Licha ya kuwa na taaluma ya ukocha Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amemuhakikishia kocha Mwinyi Zahera kuwa hatamuingilia kwenye majukumu yake

Dk Msolla ana taaluma ya ukocha na aliwahi kuinoa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’

“Nimezungumza na kocha kuhusu hili. Nimemuhakikishia awe huru kutekeleza majukumu yake,” amesema

“Nitajikita zaidi katika uongozi kuhakikisha yale niliyoyaahidi wakati wa kampeni tunayatekeleza”

“Tutampa Zahera ushirikiano wote atakaohitaji, na kama atahitaji ushauri wa kiufundi kutoka kwangu basi nitampatia”

Katika hatua nyingine Dk Msolla amesema wameanza mkakati wa kuongeza wanachama kwa kuanzisha matawi mapya

“Tunataka tuhamasishe sana uanzishwaji wa matawi mapya nchi nzima,” amesema

“Tutaigawa mikoa kwenye kanda ambapo kila kanda tutapeleka Mjumbe mmoja wa kamati ya utendaji, mchezaji mmoja wa zamani na mchezaji mmoja anayecheza sasa”

“Tutahakikisha wanapita kina kona ya nchi kushawishi mashabiki wawe wanachama”

Aidha Dk Msolla amesema wataongeza ushiriki wa wanachama katika kufanya maamuzi ya timu hiyo kupitia teknolojia kwa kuwashirikisha hukohuko waliko

Utaratibu wa sasa unawapa zaidi fursa wanachama wa jijini Dar es salaam