SAKATA La Beno KAKOLANYA

Mlinda lango Beno Kakolanya hakusafiri na kikosi cha Yanga mkoani Mbeya ikielezwa ana matatizo ya kifamilia.

Hata hivyo taarifa nyingine zinadai kuwa Kakolanya amegoma kucheza na anataka kuvunja mkataba wake akiidai klabu hiyo malimbikizo ya mishahara ya miezi mitano

Wengi wamekuwa wakijiuliza ni kweli Yanga imeshindwa kumlipa mchezaji huyo hadi kufikia hatua ya kutaka kuvunja mkataba wake?

Hivi karibuni kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera alitoa ushauri kwa viongozi wa timu hiyo kuwa ni vyema wakamalizana na wachezaji wenye madai kuliko kusajili wachezaji wapya ambao hakuna uhakika wa kulipa mishahara.

Taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii leo zinadai Kakolanya tayari amevunja mkataba wake na sasa ni mchezaji huru.

Simba inahusishwa kutaka kumsajili mlinda lango huyo aliyeonyesha ubora wa hali ya juu msimu huu.

Viongozi wa Yanga watakuwa na majibu sahihi juu kinachoendelea kumuhusu mlinda lango Beno Kakolanya.

NGASSA : Azidi kung’ara Yanga

Mrisho Ngasa ni kama amezaliwa upyaaaa kwani mambo anayofanya dimbani sio ya kawaida. Leo amefunga bao lake la nne msimu huu akitupia katika michezo miwili mfululizo.

Anachokifanya Ngasa sasa ni kuwapa majibu ‘mbashara’ wale wote waliokuwa wanam-beza na kusema umri umemtupa mkono.

Amekuwa na ushirikiano mzuri sana na Heritier Makambo ambaye kasi yake ya kupachika mabao tayari imeanza kuwatia hofu upande wa pili

Amefikisha mabao saba na inaonekana atafunga sana msimu huu.

Makambo ni mshambuliaji aliyekamilika, amedhihirisha hilo na anao uwezo wa kufunga aina zote za mabao.

Kwa hakika kikosi cha Yanga sasa kimeiva.

Licha ya changamoto za nje ya uwanja, wachezaji wa Yanga wamekuwa wakicheza kwa kujituma, Na sasa kuna kitu kingine kimeongezeka, WANAJIAMINI

Ile burudani ya ‘kampa-kampatena’ imeanza kurejea. Sasa Yanga inapata ushindi huku pia ikicheza mpira ‘mwingi’ tofauti na ilivyokuwa mwanzoni mwa msimu

Yanga hii itawashangaza wengi msimu huu..

Yanga 3-0 JKT Tanzania

Yanga imeendeleza ubabe katika ligi kuu ya Tanzania Bara baada ya leo kuwafumua maafande wa JKT Tanzania kwa mabao 3-0 kwenye mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa

Vijana wa Mwinyi Zahera wamekwea kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 35 na kuipita Azam Fc yenye alama 33 huku kila timu ikiwa imeshuka dimbani mara 13.

Ushindi huo pia umeifanya Yanga izidi kuitimulia vumbi Simba iliyo katika nafasi ya tatu ikiwa na alama 27 sasa ikiwa imeachwa kwa alama nane.

Alikuwa ni Heritier Makambo aliyeanza kuifungia Yanga bao la kuongoza kwenye dakika ya 30.

Mcongomani huyo ameendeleza rekodi yake ya kupasia nyavu sasa akifunga kwenye mchezo wa tatu mfululizo leo akitumia vyema makosa ya safu ya ulinzi ya JKT Tanzania.

Hilo lilikuwa bao lake la saba msimu huu ambapo amewafikia Okwi na Kagere wote wakiwa nyuma ya Eliud Ambokile wa Mbeya City mwenye mabao nane.

Mabao mengine ya Yanga yalipatikana kwenye kipindi cha pili yakifungwa na ‘Uncle’ Ngasa (54′) na Ibrahim Ajib (79′) kupitia mkwaju wa penati baada mlinzi wa JKT Tanzania kuzuia kwa mkono shuti la Thabani Kamusoko

Ngasa na Ajib wamefikisha mabao manne kila mmoja wakizidi kupanda juu kwenye orodha ya vinara wa mabao msimu huu.

Kwa mara nyingine Yanga imedhihirisha uimara wake kwani JKT Tanzania ni moja ya timu ngumu sana kwenye ligi msimu huu

ZAHERA: Awatahadharisha watakao sajiliwa na Yanga

Yanga ilitarajiwa kurejea jijini Dar es Salaam jana Jumatatu kutoka Bukoba baada ya kumaliza mechi zake za Kanda ya Ziwa kibabe kwa kuvuna alama zote sita ilizozifuata, lakini Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera ameamua kutoa masharti mazito.

Kocha huyo kutoka DR Congo, ameamua kuwarahisishia kazi Kamati ya Usajili ya klabu hiyo kwa kulegeza masharti ya kuwaacha wachezaji wa kigeni dirisha dogo ili kuhakikisha inawanasa wachezaji wazawa ambao anaamini wataibeba timu.

Lakini katikati ya masharti hayo kwa mabosi wake, Zahera ametoa tahadhari mapema kwa nyota wapya wanaotamani kuichezea Yanga ama watakaosajiliwa, ni lazima wawe watu wa mazoezi kwelikweli kwani hataki wavivu.

Zahera alisema usajili wa nyota wazawa utasaidia pia kuipunguzia klabu gharama, lakini amebaini ni vijana wenye vipaji vya soka isipokuwa wanaangushwa na tabia za uvivu hasa wa mazoezi.

Kocha huyo aliyeiongoza Yanga katika mechi 12 za msimu huu ikishinda 10 na kutoka sare mbili, alimtolea mfano Ibrahim Ajib ‘Kadabra’ kwa kusema awali alikuwa anampa nafasi kwa kuwa alikuwa anaonyesha jitihada kuanzia mazoezini, lakini baada ya kuanza kutegea ameamua kumkalisha benchi.

“Yanga kwa sasa imeyumba, lazima mchezaji anayekuja atambue hali ya klabu na awe tayari kustahimili, isije ikawa kama alivyofanya Obrey Chirwa kutukimbia tukiwa na uhitaji na huduma yake kisa Yanga haina pesa,” alisema Zahera.

Kauli ya Zahera imekuja huku kukiwa na taarifa, mabosi wa klabu hiyo wamekuwa katika mchakato wa kuwanasa mastraika wakali, Eliud Ambokile anayekipiga Mbeya City, Sixtus Sabilo na Bigirimana Blaise wa Stand United.

Kama kweli wachezaji hao wanahamu ya kutua Jangwani, lazima wajiandae kutii masharti ya Zahera, kwani amesisitiza anataka wapambanaji atakaowapa nafasi.

Zahera alisema amesikia nyota wengi wakihusishwa kutua Yanga katika dirisha hili la usajili, ila kwake analowaambia ni kuhakikisha wanafuata kile anachokitaka ili wapate nafasi ya kucheza katika kikosi chake akiamini mchezaji yeyote wa timu ya Ligi Kuu ana uwezo wa kukipiga Jangwani.

“Mchezaji hadi asajiliwe kikosi kinachoshiriki ligi basi huyo ni mchezaji haswa na anayejitambua, hivyo kwa upande wangu yeyote anayejituma hasa mazoezini ndiye anayepata nafasi ya kucheza siangalii majina,” alisema Zahera.

“Kuna muda watu wananiletea mapenzi, sijui kwa nini fulani sijampanga katika kikosi cha kwanza. Huwa siwasikilizi naangalia mchezaji anayefanya vizuri mazoezini, nategemea kile alichokionyesha ndicho kitakachozaa matokeo mazuri hata kwenye mchezo huwezi ukampanga mvivu wa mazoezi ukategemea katika mapambano atacheza kwa nguvu, sio kweli, huo ndio msimamo wangu,” alisema.

Mwanaspoti

USAJILI: Yanga mbioni Kumnasa mchezaji Huyu

Uongozi wa klabu ya Yanga uko mbioni kumalizana na Lipuli Fc ili kukamilisha usajili wa nahodha wa timu hiyo ambaye ni mlinzi anayemudu nafasi za beki wa kati na pembeni, Ally Sonso.

Sonso amekuwa katika kiwango bora msimu huu akiwa miongoni mwa wachezaji walioitwa na Emmanuel Amunike kuunda kikosi cha timu ya Taifa mwezi uliopita.

Sonso amethiboitisha kumalizana na Yanga akiwa tayari kuelekea Jangwani lakini akisubiri viongozi wa Lipuli Fc wamalizane na wenzao wa Yanga.

Sonso anakuwa mchezaji wa pili kuwaniwa na Yanga katika kipindi cha miezi sita baada ya mabingwa hao wa kihistoiria kumkosa Adam Salamba aliyetua Simba mwishoni mwa msimu uliopita.

Full Time: Yanga 2-1 Kagera Sugar

Mabingwa wa kihistoria wa Tanzania, Yanga leo wameendeleza rekodi ya ushindi ugenini kwa asilimia 100 baada ya kuichapa Kagera Sugar mabao 2-1 kwenye mchezo Mabingwa wa kihistoria wa Tanzania, Yanga leo wameendeleza rekodi ya ushindi ugenini kwa asilimia 100 baada ya kuichapa Kagera Sugar mabao 2-1 kwenye mchezo uliopigwa dimba la Kaitaba.

Haritier Makambo ambaye amerejesha makali yake ya kupachika mabao, aliitanguliza Yanga kwenye dakika ya 21 kwa bao safi la kichwa baada ya kuunganisha krosi ya Haji Mwinyi.

Kagera Sugar walisawazisha bao hilo kwenye dakika ya 32 kupitia mkwaju wa penati uliopigwa na Ramadhani Kapera baada ya mshambuliaji huyo kufanyiwa madhambi ndani ya eneo la hatari

Katika kipindi cha pili ni Yanga iliyorejea ikiwa na kasi ya kusaka bao la ushindi.

Yanga iliongeza kasi zaidi baada ya mabadiliko yaliyofanywa na kocha Mwinyi Zahera aliyewatoa Makamnbo aliyepata majeraha na nafasi yake kuchukuliwa na Ibrahim Ajib, Maka aliyetoka kumpisha Raphael Daudi na Haji Mwinyi aliyempisha Deus Kaseke.

Alikuwa ni Lothi aliyeihakikishia Yanga alama tatu muhimu kwenye dakika ya 74 alipounganisha kwa kichwa mpira aliotengenezewa na Deus Kaseke kutoka krosi ya Paulo Godfrey ‘Boxer’ aliyekuwa na mchezo mzuri sana.

Mlinda lango Ramadhani Kabwili leo ameonyesha ukomavu na kudhihirisha kuwa yeye ni chaguo sahihi la kulinda lango mbele na Klaus Kindoki baada ya kuokoa mashambuliz ya hatari wakati mchezo huo ukielekea ukingoni

Matokeo hayo yameikita Yanga kwenye nafasi ya pili katika msimamo wa ligi ikiwa imefikisha alama 32, alama tano mbele ya Simba mabayo iko nafasi ya tatu ikiwa na alama 27 huku timu zote zikiwa zimeshuka dimbani mara 12.

Yanga pia iko nyuma ya Azam Fc kwa alama moja tu huku pia ikiwa na mchezo mmoja mkononi.

Ushindi kwenye mchezo ujao dhidi ya JKT Tanzania utakaopigwa kwenye uwanja wa Taifa utaipeleka Yanga kileleni.uliopigwa dimba la Kaitaba.

Haritier Makambo ambaye amerejesha makali yake ya kupachika mabao, aliitanguliza Yanga kwenye dakika ya 21 kwa bao safi la kichwa baada ya kuunganisha krosi ya Haji Mwinyi.


Kagera Sugar walisawazisha bao hilo kwenye dakika ya 32 kupitia mkwaju wa penati uliopigwa na Ramadhani Kapera baada ya mshambuliaji huyo kufanyiwa madhambi ndani ya eneo la hatari
Katika kipindi cha pili ni Yanga iliyorejea ikiwa na kasi ya kusaka bao la ushindi.
Yanga iliongeza kasi zaidi baada ya mabadiliko yaliyofanywa na kocha Mwinyi Zahera aliyewatoa Makamnbo aliyepata majeraha na nafasi yake kuchukuliwa na Ibrahim Ajib, Maka aliyetoka kumpisha Raphael Daudi na Haji Mwinyi aliyempisha Deus Kaseke.
Alikuwa ni Lothi aliyeihakikishia Yanga alama tatu muhimu kwenye dakika ya 74 alipounganisha kwa kichwa mpira aliotengenezewa na Deus Kaseke kutoka krosi ya Paulo Godfrey ‘Boxer’ aliyekuwa na mchezo mzuri sana.
Mlinda lango Ramadhani Kabwili leo ameonyesha ukomavu na kudhihirisha kuwa yeye ni chaguo sahihi la kulinda lango mbele na Klaus Kindoki baada ya kuokoa mashambuliz ya hatari wakati mchezo huo ukielekea ukingoni
Matokeo hayo yameikita Yanga kwenye nafasi ya pili katika msimamo wa ligi ikiwa imefikisha alama 32, alama tano mbele ya Simba mabayo iko nafasi ya tatu ikiwa na alama 27 huku timu zote zikiwa zimeshuka dimbani mara 12.
Yanga pia iko nyuma ya Azam Fc kwa alama moja tu huku pia ikiwa na mchezo mmoja mkononi.
Ushindi kwenye mchezo ujao dhidi ya JKT Tanzania utakaopigwa kwenye uwanja wa Taifa utaipeleka Yanga kileleni.

Sababu za ZAHERA: Kutomtumia AJIBU

Kocha mkuu wa klabu ya @yangasc Mwinyi Zahera amefunguka kuhusiana na kutomtumia mshambuliaji wake Ibrahim Ajibu katika mchezo wa leo dhidi ya Mwadui Fc.
.
.
Kocha huyo amesema hakuridhishwa na mahudhurio ya nyota huyo wakati yeye akiwa kwenye majukumu ya kukinoa kikosi cha timu ya Taifa ya Congo akiwa kama kocha msaidizi.
.
.
Aliongeza kuwa kila siku kocha msaidizi wa Yanga alikuwa akimtumia majina ya wachezaji wote ambao walikuwa hawafiki mazoezini na Ajibu hakuhudhuria siku 4 hivyo ni bora afungwe akiwa ametumia wachezaji wanaofuata kile anachoagiza kuliko kucheza ambao hawana nidhamu. .
.
Mchezo huo umemalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 huku nyota wake muhimu Ibrahim Ajibu na Deus Kaseke wakishuhudia mechi hiyo Jukwaani
.
#sokaonlineUpdates

Yanga 2-1 Mwadui FC

Mabingwa wa kihistoria Tanzania Yanga leo wamedhihirisha kuwa kucheza nyumbani au ugenini hakuwezi kuwazuia kushinda baada ya kuichapa Mwadui Fc mabao 2-1 kwenye mchezo uliopigwa dimba la Kambarage mkoani Shinyanga.

Yanga iliuanza mchezo huo taratibu hata hivyo ilikuwa ya kwanza kupata bao la kuongoza mapema tu kwenye dakika ya 10 likiwekwa kambani na Mcongomani Heritier Makambo kwa shuti kali la mguu wa kushoto.

Kuingia kwa bao hilo kuliwaamsha Mwadui Fc waliopeleka mashambulizi mengi langoni kwa Yanga. Washambuliaji wa timu hiyo walikosa ufanisi katika umaliziaji.

Kwenye dakika ya 40 mlinda lango Klaus Kindoki alifanya makosa yale yale aliyofanya kwenye mchezo dhidi ya Stand United baada ya mpira aliokuwa ameudaka kumtoka mikononi na kutua mguuni kwa Salim Aiyee aliyeifungia Mwadui Fc bao la kusawazisha.

Makosa hayo yaligharimu nafasi ya Kindoki katika mchezo huo kwani kwenye kipindi cha pili kocha Mwinyi Zahera alimtoa na nafasi yake kuchukuliwa na ‘bwa mdogo’ Ramadhani Kabwili.

Zahera pia alimtoa Gadiel Michael na nafasi yake kuingia Matheo Anthony akifanya mabadiliko ya kiufundi kwa kumrudisha Jaffar Mohammed kucheza beki ya kushoto

Kwenye dakika ya 55 mpira wa adhabu uliopigwa na Feisal Salum uliwababatiza walinzi wa Mwadui Fc kabla haujatua mguuni kwa mkongwe Mrisho Ngasa aliyeutumbukiza kimiani kuihesabia Yanga bao la pili.

Hilo lilikuwa bao la tatu kwa Ngasa msimu huu.

Kwenye dakika ya 61 Zahera alifanya mabadiliko mengine kwa kumtoa Amisi Tambwe na kumuingiza kiungo Raphael Daudi mabadiliko ambayo yaliiongea uhai Yanga kwenye kipindi chote cha pili.

Matokeo hayo yameirudisha Yanga kwenye nafasi ya pili katika msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 29.

Kikosi cha Yanga vs Mwadui Fc

1. Klaus Kindoki
2. Paulo Godfrey
3. Gadiel Michael
4. Abdallah Shaibu
5. Andrew Vicent
6. Feisal Salum
7. Mrisho Ngasa
8. Maka Edward
9. Amissi Tambwe
10. Heritier Makambo
11. Jaffar Mohammed

SUB
Ramadhani Kabwili
Juma Abdul
Cleofas Sospeter
Raphael Daudi
Thabani Kamusoko
Yusuf Mhilu
Matheo Anthony