SEVILA YAWASILI BONGO

Kikosi cha Sevilla kimewasili jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo tayari kwa mchezo wa Kimataifa wa kirafiki dhidi ya mabingwa wa Tanzania Bara Simba

Sevilla ilikaribishwa nchini kwa burudani ya Msanii maarufu Mrisho Mpoto ‘Mjomba’ aliyetumbuiza uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakati timu hiyo ilipowasili

Wapinzani wao Simba wanatarajiwa kurejea leo Dar kutoka mkoani Singida ambako jana walitwaa ubingwa wa ligi kuu kwa msimu wa pili mfululizo baada ya kuifunga Singida United mabao 2-0

Baada ya mchezo jana, Simba ilielekea mkoani Dodoma ambako leo inatarajiwa kuunganisha kwa usafiri wa Ndege kurudi jijini Dar es salaam

IBRAHIM AJIBU AMALIZANA NA TP MAZEMBE.

Nahodha wa Klabu ya Yanga SC, Ibrahim Ajib anatarajia kujiunga na Mabingwa wa DR Congo, Miamba wa Lubumbashi Klabu ya TP Mazembe kwa uhamisho huru Baada ya Mkataba wake na Klabu yake ya Jangwani kufikia tamati mwishoni mwa mwezi Ujao.. 👏👏👏.
#transfers
.

Klabu ya TP Mazembe imeiandikia barua Yanga kuwaeleza kuwa wamefanya makubaliano ya kuingia mkataba na Ibrahim Ajibu utakaoanza rasmi Julai 1.

Hiyo ni baada ya Mazembe kujiridhisha kuwa mkataba wa mchezaji huyo na Yanga unaisha Juni 30.

Taarifa hii inaua matumaini ya Wanajangwani hao kuendelea kuwa na fundi huyo wa mpira msimu ujao huku ikizima tetesi za kurejea Simba.

#TransferUpdates

NIYONZIMA: Azidi Kuweka REKODI

– Kiungo wa Kimataifa wa Rwanda na Klabu ya @simbasctanzania ameendelea kuweka rekodi zake ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara kuwa Mchezaji wa kigeni kutwaa Makombe mengi zaidi ya Ligi Kuu Tanzania Bara; Baada ya kunyakua Ubingwa wa msimu huu 2018/19, Niyonzima Sasa kabeba Ubingwa Mara tano mfululizo Pia kwa jumla ni Mara ya Sita anatesa Ubingwa wa Tanzania 🇹🇿 akiwa na vilabu viwili tofauti na vikongwe nchini.
🏆2012/13 (Yanga)
🏆2014/15 (Yanga)
🏆 2015/16 (Yanga).
🏆 2016/17 (Yanga).
🏆 2017/18 (Simba).
🏆 2018/19 (Simba).
.
– Licha ya Bongo tu, Niyonzima Ana medali tatu za Ubingwa wa Kwao Rwanda 🏆 2008/9, 🏆 2009/10, 🏆 2010/11… Medali tatu za Ubingwa wa Kombe La FA kwao Rwanda 🏆 2007/8, 🏆 2009/10, 🏆 2010/11 na Medali Moja ya Ubingwa wa Kombe La FA nchini 🏆 2015/16.
#LigiKuuTanzaniaBara #TPL
@Sokawaytz

YANGA: Kuisimamisha DAR June 15

Harambee kubwa ya kuichangia Yanga itafanyika Juni 15 katika ukumbi wa Diamond Jubelee jijini Dar es salaam

Siku hiyo ndio itakuwa kileleni cha kampeni ya kuichangia Yanga iliyoanza takribani miezi miwili iliyopita

Wananchi wa kawaida, Wasanii, Wanamuziki, Wabunge, viongozi wa Serikali,Taasisi Binafsi na Mashirika watahudhuria hafla hiyo ambayo Kamati ya Hamasa inakusudia kukusanya zaidi ya Tsh Milioni 500

Mwana Jangwani weka kumbukumbu ya tarehe hiyo….!

TSHISHIMBI: Aipotezea Azam Fc

Wakati mkataba wake ukielekea ukingoni, kiungo Papi Kabamba Tshishimbi amesema hafikiri kujiunga na timu nyingine Tanzania kama atashindwa kufikia makubaliano na Yanga

Tshishimbi aliyetua Yanga miaka miwili iliyopita akitokea Mbabane Swallows ya eSwatini, amekuwa akihusishwa kuwaniwa na Azam Fc

Hata hivyo amesisitiza Yanga ndio timu pekee ambayo atachezea kwa hapa Tanzania

“Mimi ni mchezaji wa Yanga na hata mkataba utakapomalizika timu nitakayofanya nayo mazungumzo ni Yanga,” amesema

“Ni kweli zipo timu zimewasilisha ofa, lakini nitazungumza na Yanga kwanza kama tukishindwana basi nitazipa kipaumbele ofa za nje ya Tanzania”

Kwa siku za hivi karibuni Tshishimbi amekuwa katika kiwango bora akiwa amefunga mabao manne kwenye ligi kuu ya Tanzania Bara

Hakuna shaka atakuwa miongoni mwa wachezaji watakaopewa mikataba mipya katika kikosi cha Yanga

YANGA : Wachezaji wagonjwa

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema wachezaji saba wa kikosi cha Yanga hawataweza kucheza kesho mchezo dhidi ya Mbeya City baada ya kukumbwa na Malaria

Wachezaji hao ambao hawakufika kufanya mazoezi yaliyofanyika uwanja wa Uhuru leo ni pamoja na Abdallah Shaibu, Andrew Vicent, Juma Abdul, Haji Mwinyi, Said Makapu, Mohammed Issa na Paulo Godfrey

“Nadhani timu yetu imekumbwa na janga la Malaria, tuna wachezaji karibu saba ambao wanaugua Malari,” amesema Zahera

“Sijui ni kama walikula nini sijui”

Akizungumzia mchezo wa kesho, Zahera amesema hautakuwa mwepesi kutokana na ubora wa kikosi cha Mbeya City

“Tuliwafunga mchezo wa kwanza, lakini wachezaji ilibidi wajitume sana kuweza kupata matokeo,” amesema

“Kesho pia mchezo hautakuwa tofauti lakini nafurahi wachezaji wangu wamepata muda mrefu wa kupumzika hivyo watakuwa ‘fresh'”

“Kwa wale watakaocheza lengo letu ni moja, tumalize mechi mbili zilizobaki kwa kuibuka na ushindi”