Gormahia yachukua wawili kutoka tanzania

credit: @sokawaytz_…

– Mabingwa wa Ligi Kuu Nchini Kenya, Klabu ya GOR Mahia imevamia Tanzania na Kukamilisha usajili wa Nyota wawili wa Tanzania.. yatua Alliance na Singida United.

.

– K’Ogalo Imethibitisha Rasmi Kumsajili Mlinda lango David Kisu kwa Mkataba wa Miaka Mitatu akitokea Klabu ya Singida United ya mkoani Singida. Kisu mwenye umri wa Miaka 23 pia kabla ya kutua Singada amewahi kuzichezea Simba SC na Toto Africans zote za Tanzania kwa Kipindi tofauti tofauti.

.

– Wakati huo huo, Mshambuliaji wa Klabu ya Alliance FC ya Jijini Mwanza, Dickson Ambundo nae amejiunga na Mabingwa hao wa Keny kwa Mkataba wa Mkopo wa Mmoja..

#TransferNewsUpdates

@Sokawaytz_

Ajibu atoa mazito kwa mashabiki wa yanga

credit: @sokawaytz_…

– Aliyekuwa Kiungo Mshambuliaji wa Klabu ya Yanga SC, Ibrahim Ajibu amewashukuru Mashabiki na Viongozi na Benchi la Ufundi la Klabu hiyo Baada ya kukamilisha usajili wake wa kujiunga na Watani zao, @simbasctanzania, Ajibu ameandika katika Mtandao wake wa kijamii wa Instagram.

:

##Repost

Hakika Ilikua miaka miwili bora sana kwangu, ndani na nje ya uwanja, Yanga ilikua sehemu ya familia yangu.

Nitoe shukrani zangu za dhati kwa viongozi, benchi la ufundi, wachezaji na mashabiki wote, kwa kuniamini na kuniunga mkono katika kila jambo.

Ni mengi nimejifunza na nina amini yatanisaidia kunijenga zaidi kama mchezaji. Asanteni sana.

Hadi wakati mwingine tena, WananchiπŸ™πŸ»

Francis Kahata atua simba sports club

credit: @sokawaytz_…

OFFICIAL | Haijalala!! Mara Moja Baada ya kuwasili Nchini jioni hii, Kiungo wa Kimataifa wa Kenya Francis Kahata Amesaini Mkataba wa Miaka Miwili kuitumikia Klabu ya Simba SC.

.

– Kahata mwenye umri wa Miaka 27; Ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa wa kucheza eneo la kiungo, kwasasa akiwa sehemu ya wachezaji wanaounda kikosi cha timu ya Taifa ya Kenya, msimu ujao atavaa jezi ya Mabingwa hao Tanzania Bara.

.

– Amejiunga Msimbazi akitokea Gor Mahia ya Kenya ambapo akiwa kwenye klabu hiyo alishinda Kombe la Ligi Kuu mara tatu, kiungo bora wa mwaka wa Ligi Kuu ya Kenya mara mbili na mchezaji bora wa msimu 2018/2019 wa Gor Mahia.

#TPLTransferUpdates

Uganda warejea tena mazoezini baada ya kugoma

credit: @sokawaytz_…

– Baada ya Majadiliano ya Takribani Masaa Manne ya Viongozi wa Soka wa Uganda na Wachezaji wa timu hiyo ya taifa @ugandacranes, hatimae wamefikia Makubaliano na Wachezaji wamerejea kuanza Mazoezi ya kujiandaa na Mchezo wa hatua ya 16 ya AFCON dhidi ya Senegal.

:

– Wachezaji hao waligoma kufanya mazoezi kwa kile kilichoripotiwa kuwa wanadai posho zao, hivi Sasa mambo yapo shwari kocha Sebastien Desabre anaongoza Maziezi ya kuwavaa Senegal kesho Ijumaa Usiku.

#AFCONUpdates #TotalAFCON2019 #UgandaCranes

Afcon yazidi kua tamu

credit: @sokawaytz_…

FULL-TIME | New Suez Stadium & Ismailia Stadium.

Mauritania πŸ‡²πŸ‡· 0-0 πŸ‡ΉπŸ‡³ Tunisia

Angola πŸ‡¦πŸ‡΄ 0-1 πŸ‡²πŸ‡± Mali

[Amadou Haidara]

:

✍🏻 Kwa Matokeo hayo Sasa ni kwamba, timu ya taifa ya Mali inafuzu 16 bora Kama kinara wa kundi E kwa pointi zao Saba, nafasi ya pili ni Tunisia nao wanafuzu Baada ya kufikisha pointi zao tatu. Angola na Mauritania wote Kila mmoja wana pointi mbili kwa pamoja Safari yao katika AFCON 2019 imeishia hapa..

#TotalAFCON2019 #MTNTUN #ANGMLI