Kikosi ambacho kitaanza leo dhidi ya Sevilla. #NguvuMoja #SportPesaChallenge #TukutaneMei23 #SimbaVSSevilla


Kikosi ambacho kitaanza leo dhidi ya Sevilla. #NguvuMoja #SportPesaChallenge #TukutaneMei23 #SimbaVSSevilla


Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mnghwira, ameeleza kuwa amepokea kwa masikitiko ajali ya moto iliyotokea leo Mei 23, kwenye Shule ya Sekondari ya wasichana ya Ashira iliyopo Marangu Mkoani Kilimanjaro.
Mkuu huyo akiongea muda mfupi baada ya moto huo uliounguza mabweni amesema bado hajapata tathmini kamili ya ajali, lakini Kamanda wa Polisi mkoani humo ambaye amewahi eneo la tukio, amemweleza kuna uwezekano mkubwa kuwa hakukuwa na mwanafunzi bwenini.
”Shule ya Ashira ni miongoni mwa shule kongwe ambazo zipo kwenye mpango wa kufanyiwa marekebisho na niliitembelea hivi karibuni, lakini nasikitika leo imeungua upande wa mabweni. Baadaye tutapata tathmini maana Kamanda yupo kule na RAS naye amekwenda”, ameeleza.
Katibu Mkuu wa zamani wa Yanga Charles Mkwasa anaamini timu hiyo inahitaji maboresha katika baadhi ya nafasi ili iweze kuchuana na Simba msimu ujao katika kuwania ubingwa wa ligi kuu
Mkwasa aliyejiuzulu uongozi Yanga mwaka jana baada ya kupata maradhi ya moyo, amesema lazima Yanga iimarishwe ili iweze kurudisha makali yake ya zamani
Mkwasa ametaka kusajiliwa kwa wachezaji ambao watarudisha utamaduni wa timu hiyo ambao ni kushambulia kupitia pembeni akimtaja Simon Msuva kuwa aliondoka na makali yake
Tangu kuondoka kwa Simon Msuva, Yanga haikuweza kuziba pengo lake na hivyo kujikuta ikikosa makali ya kushambulia kupitia pembeni
Mabao mengi ya Yanga msimu huu yamefungwa kupitia krosi au mipira iliyokufa, kiungo Ibrahim Ajib akihusika kutengeneza mabao 17 huku mwenyewe akifunga mabao sita
“Yanga inahitaji kusajili washambuliaji wa pembeni waliokuwa na uwezo kama wa Msuva au zaidi,” amesema
Mkwasa pia amependekeza maboresho kwenye safu ya ulinzi akiamini timu hiyo inahitaji angalau walinzi wawili wapya watakaoboresha eneo hilo
Eneo la mlindalango pia limempa mashaka nahodha huyo wa zamani wa Yanga ambapo amependekeza kusajiliwa kipa mwengine mwenye ubora zaidi ya waliopo
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema wako katika mazungumzo na wachezaji wengi wanaotarajiwa kusajiliwa na timu hiyo
Zahera amesema kabla ya wiki ijayo kukamilika, watakamilisha usajili wa wachezaji nane
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amefichua kuwa aliwasiliana na viongozi wa TP Mazembe wiki tatu zilizopita kuhusu usajili wa kiungo Ibrahim Ajib
Zahera amesema kwa uwezo alioonyesha kwenye kikosi cha Yanga, Ajib anaweza kufanikiwa kukipiga TP Mazembe lakini ni lazima abadilike
“Nilisimulia na TP Mazembe wiki tatu zilizopita juu ya Ajib,” amesema Zahera
“Sina wasiwasi na yeye kusajiliwa TP Mazembe sababu nafahamu ni mchezaji mzuri sana”
“Lakini inafaa akajitume sana ili kuweza kupata namba TP Mazembe”
“Mpira wa TP Mazembe ni mpira wa nguvu mingi, yafaa akatumike sana ili aweze kucheza”
Mshambuliaji wa Yanga Heritier Makambo jana aliwashukuru mashabiki wa timu hiyo kwa kumuunga mkono katika kipindi chote alichokuwa hapa nchini
Makambo aliyefunga bao pekee la Yanga katika mchezo dhidi ya Mbeya City, anatarajiwa kuondoka mwishoni mwa msimu kujiunga na Horoya AC
“Nawashukuru mashabiki kwa kuniunga mkono. Ligi haikuwa rahisi kwetu lakini mashabiki walikuwa nasi kwa kipindi chote,” amesema Makambo
“Tayari nimeshakamilisha kila kitu na Horoya hivyo nasubiri ligi imalizike nielekee Guinea nikaanze changamoto mpya”
“Ssitaacha kuwakumbuka mashabiki, wachezaji wenzangu kocha na viongozi wa Yanga kwani tumeshirikiana vizuri”
Makambo tayari amesaini mkataba wa awali klabu ya Horoya AC kinachosubiriwa ni viongozi wa timu hiyo kuja nchini kumalizana na Yanga kabla ya ITC yake kuachiwa
Mwekezaji wa klabu ya Simba Bilionea Mohammed Dewji ‘Mo’ amesema hivi karibuni atatoa Bilioni 20 za uwekezaji wa klabu hiyo alizoahidi kuzitoa baada ya kushinda zabuni
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mo amesema changamoto ya urasimishaji wa mali za Simba imepelekea yeye kuchelewa kutoa fedha hizo
“Simba haikuwa na nyaraka halisi zake yakiwemo majengo na uwanja wa Bunju. Uongozi ulilazimika kufanya kazi ya ziada kupata hati halisi kwa mujibu wa sheria, ” alisema Mo
“Lakini pia Simba ilikuwa na madeni Mamlaka ya Mapato (TRA), klabu ilitakiwa kupeleka hesabu kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu. Kwa sasa zoezi hilo limekamilika na hata hati halisi za mali za klabu zimekamilika hivyo kukamilisha mchakato wa kufanikisha zoezi la uwekezaji”
Mo alisema anatarajia kuanza kutoa fedha zilizomo ndani ya mkataba wa uwekezaji muda mfupi ujao baada ya mchakato wa uwekezaji kukamilika
Tangu Simba ilipofanya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wake, Mo amekuwa akitoa fedha zote za kuiendesha timu hiyo ikiwemo kulipa mishahara ya wachezaji pamoja na mambo mengine yanayohusu fedha
Baada ya ligi kumalizika, Mo ameahidi kukiboresha kikosi cha Simba ambapo amesema fedha zitakazotumika kwenye usajili ni zaidi ya zile zilizotumika msimu uliopita
Msimu uliopita Simba ilitumia Tsh Bilioni 1.3 katika usajili
Ukiachilia mbali zawadi nyingi ambao uongozi wa klabu ya Simba utawapa wachezaji baada ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Tanzania Bara kwa msimu wa pili mfululizo, jana Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mohammed Dewji ‘Mo’ aliahidi kuwapa kila mchezaji Bodaboda yenye thamani ya Tsh Mil 2.4
Mo alisema zawadi hiyo itawasaidia wachezaji na familia zao kwani ni kitega uchumi kizuri
“Zawadi hii ya Bodaboda kwa kila mchezaji naitoa mimi mwenyewe. Nimewaambia wachezaji watumie Bodaboda hizo kama kitega uchumi na kuwapa ndugu zao ili kujiingizia kipato kila siku,” amesema Mo
“Wanaweza kuingia mikataba na ndugu zao ambao hawana kazi na kujipatia Tsh 15,000/- mpaka pale mikataba hiyo inapomaliza”
“Nimefarijika na mafanikio tuliyopata msimu huu. Umoja na Mshikamano baada ya kuanza uongozi mpya ni chachu ya mafanikio haya”
“Nimethamini kilichofanywa na wachezaji wetu msimu huu ndio maana nimeamua kuwapa zawadi hiyo kila mmoja”
Bilionea huyo amesema msimu ujao wamejipanga kupata mafanikio zaidi ambapo safari hii timu inatarajiwa kwenda kuweka kambi Ureno au Marekani
Simba inatarajiwa kuingia kambini mara tu baada ya kumalizika fainali za michuano ya AFCON 2019 inayofanyika nchini Misri
Wachezaji nane wa kikosi cha Simba wanatarajiwa kushiriki michuano hiyo
Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Boniface Wambura amesema Simba imetawazwa rasmi kuwa mabingwa wa Ligi Kuu baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Singida Uinted
Ushindi huo uliiwezesha Simba kufikisha alama 91, alama ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine
Wambura amesema Simba walikuwa na timu imara, walionekana kudhamiria kutwaa ubingwa huo tangu mwanzoni mwa msimu
Simba itakabidhiwa kombe keshokutwa Jumamosi, baada ya mchezo dhidi ya Biashara United utakaofanyika uwanja wa Uhuru