Kikosi kimewasili salama jijini Dar es Salaam. Kesho Alhamisi kitakuwa Uwanja wa Taifa kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya Sevilla FC. #NguvuMoja #SportPesaChallenge #TukutaneMei23




Kikosi kimewasili salama jijini Dar es Salaam. Kesho Alhamisi kitakuwa Uwanja wa Taifa kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya Sevilla FC. #NguvuMoja #SportPesaChallenge #TukutaneMei23




Timu ya Sevilla imewasili nchini usiku wa kuamkia leo tayari kwa mchezo wa Kimataifa wa kirafiki dhidi ya Simba utakaopigwa kesho Alhamisi, saa moja jioni katika uwanja wa Taifa
Katika Mkutano na Waandishi wa habari leo, Rais wa Sevilla Jose Castro ameeleza kufurahia ujio wao hapa nchini hasa ikizingatiwa wao wanakuwa timu ya kwanza kutoka Hispania kucheza Tanzania
Aidha ameipongeza Simba kwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Tanzania Bara
“Niwapongeze sana Simba ya Tanzania kwa kuchukua ubingwa wa ligi Kuu, tumekuja kucheza na timu bora. Ni heshima sana kuja Tanzania na bila shaka tutakua ni timu ya kwanza ya Laliga kuja Tanzania,” amesema
Wakati Sevilla ikiwa tayari imewasili, wapinzani wao Simba nao watatua leo kutoka mkoani Dodoma baada ya kufanikiwa kutetea ubingwa wa ligi kuu kwa msimu wa pili mfululizo
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Klabu ya Simba, Mohammed Dewji leo Jumatano Mei 22, 2019 saa 8:00 mchana ataongea na waandishi wa habari kwenye ofisi za MeTL Group zilizopo jengo la Golden Jubilee Towers, ghorofa ya 20
Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera amemwambia nahodha na mshambuliaji wa klabu hiyo Ibrahim Ajibu kufikilia mara mbili kuhusu kuihama klabu hiyo mwisho wa msimu huu. Imeelezwa.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa Zahera amedai Ajibu ni kiongozi wa wenzake na hapaswi kuwa na mawazo ya kuondoka Yanga na kuwaacha wenzake.
Mkataba wa Ajibu na Yanga unaisha mwisho wa msimu huu na inadaiwa kuwa atajiunga na klabu ya Simba baada ya mkataba wake kuisha na Yanga.
Taarifa za Ajibu kuondoka Yanga zimeanza muda mrefu uliopita na kuleta sintofahamu kwa wapenzi na mashabiki wa timu hiyo kutokana na namna mwenendo wa klabu ulivyo.
Zahera amemuomba Ajibu afikirie zaidi ya mara moja kuhusiana na kuondoka kwake kwa manufaa ya Yanga maana anaheshimu mchango wake.
TP Mazembe itamsajili kiungo wa Yanga Ibrahim Ajib Migomba akitarajiwa kujiunga na timu hiyo Julai 01 2019
TP Mazembe imeiandikia barua Yanga kuitaarifu juu ya nia ya kutaka kumsajili kiungo huyo.
Mazembe itamsajili Ajib baada ya kumaliza mkataba na Yanga
Aidha TP Mazembe imeiomba Yanga impe ruhusa ya siku tatu wiki hii ili aweze kwenda Congo kukamilisha taratibu za usajili
Hii ni habari njema kwa Ajib ambaye msimu huu umekuwa mzuri sana kwake
Ajib ameifungia Yanga mabao sita na kutengeneza mabao 17 kwenye ligi kuu ya Tanzania Bara inayoelekea ukingoni

Kikosi cha Sevilla kimewasili jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo tayari kwa mchezo wa Kimataifa wa kirafiki dhidi ya mabingwa wa Tanzania Bara Simba
Sevilla ilikaribishwa nchini kwa burudani ya Msanii maarufu Mrisho Mpoto ‘Mjomba’ aliyetumbuiza uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakati timu hiyo ilipowasili

Wapinzani wao Simba wanatarajiwa kurejea leo Dar kutoka mkoani Singida ambako jana walitwaa ubingwa wa ligi kuu kwa msimu wa pili mfululizo baada ya kuifunga Singida United mabao 2-0
Baada ya mchezo jana, Simba ilielekea mkoani Dodoma ambako leo inatarajiwa kuunganisha kwa usafiri wa Ndege kurudi jijini Dar es salaam
Nahodha wa Klabu ya Yanga SC, Ibrahim Ajib anatarajia kujiunga na Mabingwa wa DR Congo, Miamba wa Lubumbashi Klabu ya TP Mazembe kwa uhamisho huru Baada ya Mkataba wake na Klabu yake ya Jangwani kufikia tamati mwishoni mwa mwezi Ujao.. 👏👏👏.
#transfers
.


Klabu ya TP Mazembe imeiandikia barua Yanga kuwaeleza kuwa wamefanya makubaliano ya kuingia mkataba na Ibrahim Ajibu utakaoanza rasmi Julai 1.
Hiyo ni baada ya Mazembe kujiridhisha kuwa mkataba wa mchezaji huyo na Yanga unaisha Juni 30.
Taarifa hii inaua matumaini ya Wanajangwani hao kuendelea kuwa na fundi huyo wa mpira msimu ujao huku ikizima tetesi za kurejea Simba.
#TransferUpdates
– Christian Pulisic ametua London tayari kuanza kuitumikia Klabu yake ya Chelsea Baada ya kucheza nusu msimu kwa mkopo akiwa na Borussia Dortmund; Ikumbukwe Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Marekani alisajiliwa na The blues mwezi January na kuachwa kwa mkopo BvB.
#transfers