
credit: @sokawaytz…
✍🏻 Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholas Musonye amesisitiza kuwa mashindano ya Kombe la Kagame yatafanyika kama ilivyopangwa licha ya vilabu kujitoa kwa Sababu Mbalimbali; Mabingwa wa Tanzania, Simba SC, walikuwa wa kwanza kutangaza kujitoa katika Mashindano hayo wiki iliyopita, na leo Jumapili wapinzani wao, Yanga SC pia wamethibitisha kuwa hawatoshiriki katika mashindano hayo ya kikanda.. Jana Mabingwa wa Burundi, Agle Noir FC waliandika barua ya kujitoa.
.
– Mechi za Mashindano haya zinatarajiwa kufanyika jijini Kigali, Rwanda kuanzia Julai 7 mpaka Julai 21..
🗣 (Simba na Yanga) “Haishangazi hata wanapopigwa katika mashindano ya CAF, mara zote hupoteza kwa 5-0 au hata 6-0, hatufadhaiki wala haitukwamishi kwa kujitoa kwao”… Alisema Musonye ambapo Pia amesisitiza kuwa tayari wana timu kadhaa kutoka Kenya, Uganda, Rwanda na DR Congo ambazo zitakuja na kujaza nafasi hizo timu mbili za Tanzania.
🗣 “Mashindano hayawezi kushindwa kufanyika kwa sababu ya Yanga na Simba hawapo, na tayari tumezungumza na timu Mbalimbali kuja kushiriki badala yao, Lengo letu ni kuwa na mashindano ya timu 16 na tutasimamia yawe hivyo” Musonye amesema.
.
✍🏻 Zesco United ya Zambia, AS Vita Club na DC Motema Pembe za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wao tayari wamethibitisha ushiriki wao pamoja na Azam FC ya Tanzania… Mashindano huleta timu kutoka Kenya, Rwanda, Burundi, Djibouti, Eritrea, Sudan, Somalia, Sudan Kusini, Ethiopia, Uganda, Tanzania na Zanzibar… Mshindi wa mashindano haya atarejea nyumbani kwake na kitita cha pesa ya thamani ya US$30,000..
#Updates #kagameCup
@Sokawaytz




















