Mbabane Swallos yaigwaya SIMBA

Baada ya kupangwa kuanza na mabingwa wa Tanzania Bara, Simba kwenye mchezo wa hatua ya awali michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, Mbabane Swallows imeonyesha ‘mchecheto’ kuelekea mchezo huo.

Ujumbe ulioandikwa kwenye ukurasa wa mtandao wa Facebook wa timu hiyo unaonyesha kuihofia Simba hasa baada ya kubaini ina wachezaji 10 wanaocheza timu za Taifa

“Tumepangwa na timu kutoka nchini Tanzania, Simba kwenye mchezo wa awali wa michuano ya ligi ya mabingwa,” umesema ujumbe huo.

“Sio ratiba mbaya na lengo letu ni kama msimu uliopita, kufuzu kwa hatua ya makundi”

“Hata hivyo Simba sio timu ya kubeza, ina wachezaji nane kwenye timu ya Taifa. Wanacheza mchezo mzuri na ina washambuliaji wa pembeni wenye kasi”

Mbabane Swallows inayoshika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu ya Swaziland, itakuja nchini kati ya Novemba 27-28 kuivaa Simba kwenye uwanja wa Taifa kabla ya mchezo wa marudiano wiki moja baadae huko Uswazi.

Simba inaendelea na maandalizi kuelekea mchezo huo ambapo Ijumaa wiki hii itacheza na mabingwa wa Malawi, Big Bullets kwenye mchezo wa Kimataifa wa kirafiki.

Singida United Yajitosa kumwania KAHEZA, RASHID Simba sc

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems ametoa ruhusa kwa wachezaji wake wawili, Marcel Kaheza na Mohammed Rashid kutolewa kwa mkopo dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa mwishoni mwa wiki hii.

Wachezaji hao wamekuwa hawapati nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha Simba kutokana na uwepo wa ushindani mkali wa namba unaosababishwa na ubora wa wachezaji kikosini.

Klabu ya Singida Unuted imeonyesha nia ya kutaka kuwachukua wachezaji wote wawili ili kuongeza nguvu kwenye kikosi chao ambacho kimekimbiwa na wachezaji wengi kutokana na ‘ukata’

Tanzania Prisons ilikuwa timu ya kwanza kujitokeza ikimtaka mshambuliaji wao wa zamani Mo Rashidi aliyeifungia timu hiyo mabao 10 msimu uliopita

Simba imedhamiria kuimarisha kikosi chake wakati wa dirisha dogo la usajili huku ikipanga kuwatoa kwa mkopo baadhi ya wachezaji waliokosa namba ili kulinda viwango vyao

WAWA Ampa jeuri Kocha Simba sc

Beki kisiki wa Simba, Paschal Wawa amempa jeuri kocha Mkuu Patrick Aussems ya kutokuwa na presha ya kusajili mabeki kwenye usajili wa dirisha dogo kwa kuwa anafanya kazi yeke ipasavyo.

Aussems amesema kuwa kwa sasa hafikirii kuongeza beki wa kati ndani ya kikosi chake kwa kuwa wale waliopo wanatosha na wanafanya kile ambacho anawaelekeza hali inyompa amani.

“Nafasi ya beki wa kati sifikiri kama nitaongeza mchezaji . Hawa waliopo wakiongozwa na Wawa ni wazuri na wanaonyesha uwezo mkubwa katika mechi zetu wanazocheza,” Aussems amenukuliwa na GPL

Mabeki wa kati wa Simba Erasto Nyoni, Juuko Murshid na Paul Bukaba wameonyesha viwangi vizuri katika michezo waliyocheza kwani wameruhusu mabao manne tu katika mechi 11 za ligi.

Pia yupo beki chipukizi Yusufu Mlipili ambaye licha ya kutopata namba msimu huu, anaweza kuisaidia Simba pale atakapohitajika na kocha Aussems

RATIBA ya KLABU BINGWA AFRICA

Droo ya ratiba ya awali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika msimu wa 2018/19 ilifanyika nchini Morocco Novemba 03, 2018 lakini haikuwa imetangazwa rasmi na Shirikisho la soka Barani Afrika CAF.

Ratiba hiyo imetangazwa rasmi leo ambapo Simba sasa itachuana na Mbabane Swallows, mabingwa wa ligi kuu ya Swaziland.

Taarifa za awali kuwa Simba ingechuana na timu ya Ngozi inayomilikiwa na Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza hazikuwa sahihi na zilitokana na mkanganyiko wa ratiba hiyo

Mchezo wa kwanza utapigwa kwenye uwanja wa Taifa mwishoni mwa mwezi huu Novemba 27-28 huku mchezo wa marudiano ukitarajiwa kupigwa nchini Swaziland Disemba 04-05.

Mbabane Swallows sio timu ya kubeza. Timu hiyo ndiyo aliyotokea Asante Kwasi kabla ya kuja nchini na kiungo wa Yanga Papi Tshishimbi.

Misimu miwili iliyopita Swallows iliiondosha Azam Fc kwenye raundi ya pili ya michuano ya kombe la Shirikisho na yenyewe ikafanikiwa kutinga hatua ya makundi.

Aidha timu hiyo msimu uliopita ilifanikiwa kutinga hatua ya makundi michuano ya ligi ya mabingwa ikipangwa kundi moja na Etoile Du Sahel, Zesco United na 1st De Agosto

Ilimaliza nafasi ya mwisho ikiwa na alama nne katika kundi D ambalo timu ya 1st De Agosto ilifanikiwa kutinga nusu fainali ya michuano hiyo inayofikia tamati leo kwa mchezo wa marudiano wa fainali kati ya Esperance dhidi ya Al Ahly ambayo ilishinda kwa mabao 3-1 katika mchezo wa kwanza wiki iliyopita

Wawakilishi wengine wa Tanzania, kutoka upande wa Zanzibar, JKU wao wataanzia ugenini katika mchezo dhidi ya Al Hilal ya Sudan

Kama Simba itafuzu hatua ya awali, raundi ya kwanza ikachuana na mshindi kati ya UD Songo ya Msumbiji dhidi ya Nkana Fc ya Zambia

Simba Sc: Kumsajili Thomas ULIMWENGU

#TetesiZaUsajili Imeripotiwa kuwa klabu ya Simba Sc ipo kwenye mchakato mzito kuhakikisha inamsajili nyota wa zamani wa Tp Mazembe Thomas Ulimwengu (25) kuelekea kwenye dirisha dogo la usajili litakalofunguliwa mapema wiki ijayo November 15.

Habari za chini chini zilizotufikia zimedai tayari uongozi wa klabu hiyo umepanga mkakati wa kuanza kuzungumza nae wiki hii ili kupata saini yake mara baada ya kuvunja mkataba na klabu yake ya Al Hilal ya Sudan

Ikumbukwe kabla ya kutua Al Hilal ziliwahi kuzagaa taarifa kuwa nyota huyo angesajiliwa Yanga kutokana na uongozi wa klabu hiyo kuonyesha nia ya kumhitaji #soka Updates

OKWII: Nikiachana Na SOKA nitakua Wakala Wa Wachezaji

Mshambuliaji wa Simba na timu ya taifa ya Uganda Emanuel Okwi amesema akiachana na soka anataka kuwa wakala wa wachezaji ili kuwasaidia wanufaike na vipaji vyao wasipite katika matatizo ambayo yeye na wachezaji wengine wegi wa sasa wanapitia.
:
“Baada ya kuacha mpira malengo yangu ni kuwa agent wa wachezaji wa baadaye kwa sababu nataka wafaidike na wafurahie mpira.”
:
“Nitapambana kuhakikisha wanapita katika njia sahihi ili wasipate matatizo ambayo sisi tumepata”.

OKWI: Aibuka Mchezaji Bora mwezi OCTOBER

Mshambuliaji wa Simba Emmanuel Okwi ametangazwa na Kamati ya Tuzo ya TFF kuwa mchezaji bora wa ligi kuu ya Tanzania Bara kwa mwezi wa 10.

Okwi ameshinda tuzo hiyo baada ya kuifungia Simba mabao saba katika mwezi huo.

Wakati huo huo Kamati ya Tuzo imemchagua Kocha wa Azam FC, Hans Pluijm kuwa Kocha Bora wa mwezi Oktoba akiwashinda Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems na Kocha Mkuu wa Mbeya City, Ramadhan Nsazwarimo