SIMBA : Baada ta BOCCO : OKWI MKUDE

Simba tayari imeanza mchakato wa kuhuisha mikataba ya wachezaji wake ambayo inamalizika mwishoni mwa msimu

Baada ya kumalizana na nahodha John Bocco, inaelezwa mshambuliaji Emmanuel Okwi na Jonas Mkude wako katika mazungumzo na uongozi wa Simba ili kuhuisha mikataba yao

Wachezaji hao wanadaiwa kunyemelewa na timu nyingine hivyo kuulazimu uongozi wa Simba kuharakisha kuwapa mikataba mipya

Okwi amekuwa akihusishwa na timu kadhaa kutoka Afrika Kusini, ambapo mwezi Januari Kaizer Chiefs iliwasilisha ofa kwa klabu ya Simba lakini uongozi ‘ukaipiga chini’

Mkude anatajwa kuwaniwa na timu kadhaa kutoka Arabuni

Wachezaji wengine ambao wako katika mipango ya mwalimu na watasaini mikataba mipya pia

Aidha Simba huenda isifanye mabadiliko makubwa ya kikosi chake hasa kwa wachezaji wa ndani baada ya Aussems kuagiza waliopo waongezewe mikataba kwa kuwa nje ya Simba hakuna wachezaji wengi bora

Wachezaji wa ndani wanaotajwa kujiunga na Simba kwa ajili ya msimu ujao ni pamoja na Vitalis Mayanga kutoka Ndanda Fc.

Mayanga alisajiliwa kwa ajili ya michuano ya CAF lakini taarifa zake zikachelewa kutumwa

Wengine ni Ibrahim Ajib kutoka Yanga na Beno Kakolanya (huru)

SIMBA – TUZO ya Mshambuliaji Bora wa mwaka – MO SIMBA AWARDS

John Bocco, Meddie Kagere na Emmanuel Okwi wameteuliwa kuwania tuzo ya mshambuliaji bora wa mwaka

Bocco, Kagere na Okwi wameongoza vyema safu ya ushambuliaji ya Simba wakifunga mabao 50 kati ya 72 yaliyofungwa kwenye ligi

Kagere anaongoza mbio za kuwania kiatu cha dhahabu ligi kuu ya Tanzania Bara akiwa amefunga mabao 20

Mshambuliaji huyo pia ndiye kinara wa mabao wa kikosi cha Simba katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika ambayo Simba imetolewa hatua ya robo fainali amefunga mabao sita

Bocco na Okwi wamefunga mabao 15 kila mmoja kwenye ligi kuu ya Tanzania Bara

Kupiga kura tembelea tovuti rasmi ya MO SIMBA AWARDS kwa kubonyeza HAPA

SIMBA Yamalizana na Bocco

Klabu ya Simba inaendelea na mchakato wa kuhuisha mikataba ya wachezaji wake ambayo inamlizika na tayari imemalizana na nahodha wake John Bocco

Taarifa za uhakika ni kwamba Bocco amesaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kukipiga Msimbazi hadi mwaka 2021

Bocco aliyeifungia Simba mabao 15 kwenye ligi ya Tanzania Bara msimu huu, alikuwa akiwaniwa na timu yake ya zamani Azam FC

Azam Fc inadaiwa kuwashawishi Aishi Manula, Erasto Nyoni, John Bocco na Shomaria Kapombe wasaini kunako klabu hiyo waliyokuwa wakicheza kabla ya kusajiliwa na Simba mwaka juzi

Msimu uliopita Bocco aliibuka kuwa mchezaji bora wa Simba na msimu huu ameteuliwa kuwania tuzo hiyo sambamba na Meddie Kagere na Clatous Chama

Zoezi la kuchagua mchezaji bora wa msimu huu tayari limeanza, kura zinapigwa kupitia tovuti rasmi ya Mo Simba Awards

Bonyeza HAPA kumpigia kura Bocco kama unadhani anastahili kuwa mchezaji bora wa Simba msimu huu

SIMBA inamkumbuka Patrick Mafisango

Tarehe kama ya leo miaka saba iliyopita, May 17 2012 klabu ya Simba ilipatwa na majonzi makubwa baada ya kumpoteza kiungo wake Patrick Mafisango aliyefariki kwa ajali ya gari

Umauti ulimfika Mafisango kupitia ajali ambayo katika jitihada za kunusuru maisha ya mwendesha pikipiki, gari yake iliingia mtaroni na kusababisha apoteze maisha kutokana na majeraha aliyopata

Kabla ya kuja Tanzania Mafisango alichezea APR ya Rwanda na alipofika nchini alijiunga na Azam Fc kabla ya kusajiliwa na Simba

Mechi ya mwisho Mafisango kuichezea Simba ilikuwa dhidi ya Al Ahly Shandy nchini Sudan katika hatua ya 16 Bora ya Kombe la Shirikisho, ambayo Simba ilitolewa kwa penalti 9-8, kufuatia sare ya jumla ya 3-3.

Hadi anafariki dunia, Mafisango alikuwa ni tegemeo Simba katika safu ya kiungo

Pamoja na kucheza kama kiungo, Mafisango pia anamudu kucheza nafasi ya beki wa kushoto na beki wa kati

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems ameeleza furaha yake baada ya timu hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 3-0

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems ameeleza furaha yake baada ya timu hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa Uhuru

Akizungumza na Wanahabari baada ya mchezo huo, Aussems amesema Simba ilitawala mchezo na ilistahili kuondoka na ushindi mnono

Aidha Aussems amesema ushindi umezidi kuisogeza Simba karibu na ubingwa wa pili mfululizo

“Tulitawala mchezo, tulitengeneza nafasi na tulifanikiwa kufunga. Jambo muhimu tumekaribia lengo letu,” amesema Aussems

BREAKING NEWS: MAKAMBO ATIMKA YANGA, AJIUNGA HOROYA AC

Mshambuliaji wa Yanga Heritier Makambo ametimkia Guinea kujiunga na klabu ya Horoya Fc

Taarifa za Makambo kusajiliwa na Horoya zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii mapema leo ambapo timu hiyo imemtambulisha rasmi
Makambo ndiye kinara wa mabao katika kikosi cha Yanga msimu huu akitupia kambani mabao 16

Kulingana na mtandao wa Kalonews, Makambo amesaini mkataba wa miaka mitatu

“Horoya AC imemsajili mshambuliaji kutoka DR Congo Heritier Makambo aliyekuwa akiichezea Young Africans ya Tanzania,” imesema taarifa ya mtandao huo

“Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25 aliyewahi kuichezea Motema Pembe, amefunga mabao 16 kwenye ligi ya Tanzania”
“Amesaini mkataba wa miaka mitatu”

Kuondoka kwa mshambuliaji huyo ni pigo kwa Yanga ambayo iko kwenye mchakato wa kukiimarisha kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao

https://play.app.goo.gl/?link=https://play.google.com/store/apps/details?id=com.chumbani.raha&ddl=1&pcampaignid=web_ddl_1

Yanga italazimika kuingia sokoni kusaka washambuliaji wengine wakali

Hata hivyo Yanga itanufaika na mauzo ya mshambuliaji huyo kwani mkataba wake na Yanga ulikuwa bado haujamalizika
Inaelezwa Makambo ameuzwa kwa dau linalokadiriwa kufikia Milioni 230 za Kitanzania




SIMBA YAIKUNG’UTA MTIBWA SUGAR BAO 3-0 UWANJA WA UHURU YATINGA KILELENI

Mabingwa watetezi ligi kuu ya Tanzania Bara Simba wameendelea kujiweka katika nafasi nzuri ya kutetea taji lao baada ya leo kuichapa Mtibwa Sugar mabao 3-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Uhuru

Simba iliingia kwenye mchezo huo ikiwa na shauku ya kuondoka na alama zote tatu baada ya kutopata ushindi katika michezo miwili iliyopita
Ilianza kuhesabu bao la kwanza kupitia kwa nahodha John Bocco kwenye dakika ya 32 akiunganisha krosi murua iliyochongwa na Meddie Kagere

Simba iliyotawala mchezo huo, ilikwenda mapumziko ikiwa inaongoza kwa bao 1-0

cut

Kasi waliyomaliza nayo kipindi cha kwanza, waliiendeleza kwenye kipindi cha pili na kufanikiwa kufunga mabao mengine mawili kupitia kwa Emmanuel Okwi(56′) na Clatous Chama (46′)
Mtibwa Sugar ilitumia zaidi mashambulizi ya kushitukiza na ilipoteza nafasi kadhaa kutokana na washambuliaji wake kutokuwa makini
Washambuliaji wa Simba wameendelea kuweka rekodi ya kuzifumania nyvu msimu huu, Simba ikifikisha mabao 72
Kagere, Bocco na Okwi wamefikisha mabao 50
Ushindi huo umeirejesha Simba kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 85
Simba sasa inahitaji alama nne tu kutoka mechi nne zilizobaki ili iweze kutetea ubingwa

Simba yaomba sapoti ya mashabiki mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar

Leo saa kumi jioni Simba itashuka uwanja wa Uhuru kuikabili Mtibwa Sugar katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara

Uongozi wa timu hiyo umewataka mashabiki wajitokeze kwa wingi kuwapa sapoti wachezaji katika mchezo huo ambao matokeo ya ushindi ni muhimu

Msemaji wa Simba Haji Manara amesema wachezaji wameahidi kupambana ili kupata matokeo lakini uwepo wa mashabiki wengi uwanjani itakuwa chachu ya wao kufanya juhudi zaidi

“Twendeni uwanjani kwa wingi kama ilivyo kawaida yetu. Tunahitaji alama nane tu tuweze kutwaa ubingwa, tujitokeze kwa wingi kwani kwa umoja wetu tutashinda”

Mchezo wa leo ni kwanza kwa Simba na Mtibwa Sugar kukutana msimu huu. Mchezo wa pili baina ya timu hizo utapigwa mkoani Morogoro, May 28

Simba yapania kuweka sawa hesabu za ubingwa leo

Mabingwa watetezi ligi kuu ya Tanzania Bara Simba leo wanashuka dimba la Uhuru kuwakabili Mtibwa Sugar katika mchezo ambao vijana wa Patrick Aussems wamepania kuchukua alama zote tatu

Baada ya kukosa ushindi katika michezo miwili iliyopita, Simba leo inahitaji ushindi ili kuweka sawa hesabu za ubingwa

Simba inahitaji alama saba kutoka michezo mitano iliyobaki kuweza kutetea ubingwa kwa msimu wa pili mfululizo

Kama itashinda leo, halafu ikashinda mchezo dhidi ya Ndanda Jumapili, sare au matokeo ya ushindi mchezo dhidi ya Singida United, yatatosha kuipa Simba ubingwa wa pili mfululizo

Meneja wa Simba Patrick Rweyemamu amesema wachezaji wa timu hiyo wako katika hali nzuri kuelekea mchezo huo ambao wamepania kuondoka na alama zote tatu