
Kocha akisaini mkataba mpya wa mwaka moja kuendelea kuitumikia @simbasctanzania Jee anastairi kupewa mkataba wa mwaka moja au aongezewe zaidi.? #nguvumoja
credit: @simba_view

Kocha akisaini mkataba mpya wa mwaka moja kuendelea kuitumikia @simbasctanzania Jee anastairi kupewa mkataba wa mwaka moja au aongezewe zaidi.? #nguvumoja
credit: @simba_view
Thanks for joining me!
Good company in a journey makes the way seem shorter. — Izaak Walton

Klabu ya Benfica imesema haitamuuza nyota wake Joao Felix chini ya dau la £105m msimu huu (Daily Mail) .
Felix anawaniwa na vilabu ya Man United pamoja na Man City
Klabu ya Simba Sc imeanza kuwania saini ya beki wa Lipuli Fc Willium Lucian “Galas” ili kuboresha kikosi chao kuelekea kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika msimu ujao. .
Taarifa za awali zinadai kuwa huenda ikaachana na beki wao Zana Coulibaly.
Lamine Moro beki raia wa Ghana ambaye awali aliwahi kufanya majaribio na kikosi cha Simba Sc ametua nchini kumalizana na Yanga Sc tayari kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania.
Kikosi cha Yanga leo kimeendelea na mazoezi kwenye uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo wa mwisho wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Azam Fc utakaopigwa Jumanne, May 28 dimba la Uhuru
Kocha Mkuu wa mabingwa hao wa kihistoria Mwinyi Zahera amesema baadhi ya wachezaji waliokuwa wagonjwa wameanza kurejea kikosini
“Paul Godfrey alikuwa mgonjwa lakini leo ameanza mazoezi. Dante, Abdul, Ngasa, Banka, Jaffar na Ajib bado wagonjwa,” amesema
Katika hatua nyingine Zahera amemuagiza Meneja wa Yanga Nadir Haroub kumsaka beki wa timu hiyo Kelvin Yondani ambaye haonekani mazoezini
Zahera amesema hana taarifa kama Yondani ni mgonjwa, amejaribu kumpigia simu bila ya mafanikio
“Sina taarifa za Yondani, nimejaribu kumpigia simu lakini hapokei, tumemtuma Meneja (Nadir) aende akamtafute kwake anipe mrejesho kabla sijafanya maamuzi,” Zahera aliiambia eFM
Aliyekuwa kiungo wa Azam FC Tafadzwa Kutinyu ambaye alikuwa akihusishwa na Yanga, amesajiliwa na klabu ya Horoya AC, mabingwa wa Guinea
Kutinyu ametua timu hiyo akiwa mchezaji huru baada ya mkataba wake na Azam Fc kumalizika
Kutinyu anaungana na Heritier Makambo ambaye anasubiri kujiunga na timu hiyo baada ya ligi kumalizika
Kutinyu yuko kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Zimbabwe kinachojiandaa na fainali za AFCON 2019 zitakazofanyika Misri
Kutinyu na Thabani Kamusoko ni wachezaji pekee kutoka Tanzania walioitwa timu ya Taifa ya Zimbabwe
Kiungo mkongwe Thabani Kamusoko yuko Zimbabwe na kikosi cha timu ya Taifa kinachojiandaa na fainali za AFCON 2019 zitakazofanyika mwezi ujao nchini Misri
Ni kama kiungo huyo hatarejea tena Yanga baada ya jana kuwaaga wachezaji wenzake wa kikosi cha Yanga
“Nimewakumbuka sana rafiki zangu, sina neno jingine la kusema zaidi kwani mlikua zaidi ya marafiki,” ameandika Kamusoko ukurasa wake wa Instagram

Kamusoko ni miongoni mwa wachezaji ambao mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu, hatma yake ikibaki mikononi mwa kocha Mwinyi Zahera
Keshokutwa Jumanne baada ya mchezo dhidi ya Azam Fc, Yanga itatangaza majina ya wachezaji ambao wameachwa pamoja na wale ambao tayari wamesajiliwa na timu hiyo
Zahera amesema kuna wachezaji nane ambayo tayari wamesajiliwa na timu hiyo, sita wa Kimataifa na wawili wazawa
Licha ya kuwa na taaluma ya ukocha Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amemuhakikishia kocha Mwinyi Zahera kuwa hatamuingilia kwenye majukumu yake
Dk Msolla ana taaluma ya ukocha na aliwahi kuinoa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’
“Nimezungumza na kocha kuhusu hili. Nimemuhakikishia awe huru kutekeleza majukumu yake,” amesema
“Nitajikita zaidi katika uongozi kuhakikisha yale niliyoyaahidi wakati wa kampeni tunayatekeleza”
“Tutampa Zahera ushirikiano wote atakaohitaji, na kama atahitaji ushauri wa kiufundi kutoka kwangu basi nitampatia”
Katika hatua nyingine Dk Msolla amesema wameanza mkakati wa kuongeza wanachama kwa kuanzisha matawi mapya
“Tunataka tuhamasishe sana uanzishwaji wa matawi mapya nchi nzima,” amesema
“Tutaigawa mikoa kwenye kanda ambapo kila kanda tutapeleka Mjumbe mmoja wa kamati ya utendaji, mchezaji mmoja wa zamani na mchezaji mmoja anayecheza sasa”
“Tutahakikisha wanapita kina kona ya nchi kushawishi mashabiki wawe wanachama”
Aidha Dk Msolla amesema wataongeza ushiriki wa wanachama katika kufanya maamuzi ya timu hiyo kupitia teknolojia kwa kuwashirikisha hukohuko waliko
Utaratibu wa sasa unawapa zaidi fursa wanachama wa jijini Dar es salaam
Baada ya mchezo wa Kimataifa wa kirafiki dhidi ya Sevilla, tukio la mshambuliaji wa Simba Adam Salamba kumuomba kiatu kiungo mahiri na nahodha wa Sevilla Ever Banega, liliibua mijadala kwenye mitandao ya kijamii
Baadhi ya mashabiki hawakuelewa maana ya tukio hilo ambalo ni la kawaida na hufanywa na wanasoka kama sehemu ya kuonyesha uungwana mchezoni

Salamba amesema ataweka kumbukumbu kiatu alichopewa na kiungo huyo wa Kimataifa wa Argentina
“Kiatu ambacho nimepewa na mchezaji wa kimataifa kutoka Sevilla, Ever Banega nitakichongea fremu iwe kumbukumbu daima,” amesema
Aidha Salamba amesema fursa ya kucheza na Sevilla imemuongezea shauku ya kutaka kwenda kucheza soka nje ya nchi
“Ndoto zangu ni kucheza nje ya Tanzania, baada ya kucheza na Sevilla juzi, imeniongezea ari ya kutaka kufikia malengo hayo”