SIMBA : Baada ta BOCCO : OKWI MKUDE

Simba tayari imeanza mchakato wa kuhuisha mikataba ya wachezaji wake ambayo inamalizika mwishoni mwa msimu

Baada ya kumalizana na nahodha John Bocco, inaelezwa mshambuliaji Emmanuel Okwi na Jonas Mkude wako katika mazungumzo na uongozi wa Simba ili kuhuisha mikataba yao

Wachezaji hao wanadaiwa kunyemelewa na timu nyingine hivyo kuulazimu uongozi wa Simba kuharakisha kuwapa mikataba mipya

Okwi amekuwa akihusishwa na timu kadhaa kutoka Afrika Kusini, ambapo mwezi Januari Kaizer Chiefs iliwasilisha ofa kwa klabu ya Simba lakini uongozi ‘ukaipiga chini’

Mkude anatajwa kuwaniwa na timu kadhaa kutoka Arabuni

Wachezaji wengine ambao wako katika mipango ya mwalimu na watasaini mikataba mipya pia

Aidha Simba huenda isifanye mabadiliko makubwa ya kikosi chake hasa kwa wachezaji wa ndani baada ya Aussems kuagiza waliopo waongezewe mikataba kwa kuwa nje ya Simba hakuna wachezaji wengi bora

Wachezaji wa ndani wanaotajwa kujiunga na Simba kwa ajili ya msimu ujao ni pamoja na Vitalis Mayanga kutoka Ndanda Fc.

Mayanga alisajiliwa kwa ajili ya michuano ya CAF lakini taarifa zake zikachelewa kutumwa

Wengine ni Ibrahim Ajib kutoka Yanga na Beno Kakolanya (huru)

SEVILLA – Kuwasili Dar Mei 21

Leo Jumamosi Sevilla inakamilisha mchezo wa mwisho ligi kuu ya Hispania , La Liga kwa kucheza na Athletic Club

Kama itashinda mchezo huo, Sevilla inayoshika nafasi ya sita kwenye msimamo wa La Liga , inaweza kukata tiketi ya kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa msimu ujao

Baada ya mchezo huo, kikosi cha Sevilla itaanza safari ya kuja nchini tayari kwa mchezo wa Kimataifa wa kirafiki dhidi ya mabingwa wa Tanzania Bara, Simba

Sevilla inatarajiwa kuwasili nchini Mei 21 kuelekea mchezo huo utakaopigwa Mei 23, uwanja wa Taifa kuanzia saa moja jioni

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, (TFF) limesema kuwa ujio wa timu ya Sevilla kutoka nchini Hispania chini ya SportPesa Tanzania utaongeza hamasa na maendeleo ya mpira wa miguu nchini.

TFF imewataka wachezaji wa Simba kutumia fursa ya mechi hiyo kuonyesha uwezo na vipaji vyao ili kujitangaza

Rais wa TFF, Wallace Karia amesema kuwa Sevilla FC ni timu kubwa yenye historia kubwa katika soka duniani na hivyo ujio wao utawavutia mashabiki wa soka hata wa nchi jirani ili kuja kushuhudia wachezaji nyota wa wanaocheza bara la Ulaya.

CASILLAS: Mlinda lango wa Kimataifa wa Hispania, Iker Casillas Ametangaza kustaafu Soka rasmi hii leo;

– Mlinda lango wa Kimataifa wa Hispania, Iker Casillas Ametangaza kustaafu Soka rasmi hii leo; hili limekuja siku chache Baada ya kuruhusiwa hospitali ambako alikimbizwa kufuatia kupata Shambulio La Moyo wakati akiwa katika Mazoezi ya Klabu yake ya FC Porto..
.
– Legendary huyo amefanikiwa kucheza jumla ya mechi 881 ngazi ya Vilabu na games 167 katika timu yake ya taifa ya Hispania na makombe aliyotwaa ni Kama..
• 1x World Cup 🏆
• 2x Euro Championship 🏆
• 3x Champions League 🏆 • 5x La Liga 🏆
• 2x Copa del Rey 🏆
• 1x Club World Cup 🏆
• 1x Primeira Liga 🏆
🙌🏽🐐 #Updates

RATIBA YA SOKA HII LEO JUMAMOSI:

RATIBA YA SOKA HII LEO JUMAMOSI:
– Serie A
16:00 Udinese
SPAL
19:00 Genoa
Cagliari
21:30 Sassuolo
Roma
.
– FA Cup FINAL!!
19:00 Manchester City
Watford
.
– Bundesliga
16:30 Bayern München
Eintracht Frankfurt
16:30 Borussia M’gladbach
Borussia Dortmund
16:30 Fortuna Düsseldorf
Hannover 96
16:30 Freiburg
Nürnberg
16:30 Hertha BSC
Bayer Leverkusen
16:30 Mainz 05
Hoffenheim
16:30 Schalke 04
Stuttgart
16:30 Werder Bremen
RB Leipzig
16:30 Wolfsburg
Augsburg
.
– Ligue 1
22:00 Bordeaux
Reims
22:00 Guingamp
Nîmes
22:00 Lille
Angers SCO
22:00 Monaco
Amiens SC
22:00 Montpellier
Nantes
22:00 Olympique Lyonnais
Caen
22:00 PSG
Dijon
22:00 Saint-Étienne
Nice
22:00 Strasbourg
Rennes
22:00 Toulouse
Olympique Marseille
.
– La Liga
14:00 Levante
Atlético Madrid
17:15 Espanyol
Real Sociedad
17:15 Getafe
Villarreal
17:15 Real Valladolid
Valencia
17:15 Sevilla
Athletic Club
21:45 Celta de Vigo
Rayo Vallecano
21:45 Deportivo Alavés
Girona
21:45 Huesca
Leganés
.
– UEFA Women’s Champions League – FINAL!!
19:00 Olympique Lyonnais
Barcelona
.
– Belgium – First Division A.
(EL play-off: group A)
21:00 KFCO Beerschot-Wilrijk
Oostende
21:00 Sporting Charleroi
Eupen
21:00 St.Truiden
Westerlo
.
– Ligi Kuu Bara.
16:00 African Lyon
Mbeya City FC
.
– Kenya – Premier League.
14:00 MT Kenya United
SoNy Sugar
15:00 Kariobangi Sharks
KCB
15:00 Nzoia Sugar FC
Sofapaka
16:15 Posta Rangers
Kakamega Homeboyz
.
– Morocco – Botola Pro
22:00 Difaa El Jadida
Hassania Agadir
22:00 Rapide Club Oued Zem
OCK Khouribga
.
– South Africa – Cup.
20:00 Kaizer Chiefs
TS Galaxy
:
MECHI ZA JANA
– Belgium – First Division A.
(EL play-off: group)
FT Kortrijk 4 – 0 Cercle Brugge
FT Royal Excel Mouscron 2 – 4 Waasland-Beveren
FT Zulte-Waregem 2 – 1 Union St.-Gilloise
#Updates @Sokawaytz

MAN U – Yaanza Mikakati ya Kusuka Kikosi Bora Msimu Ujao

✍🏼 Kujenga kikosi ndani ya Manchester United kumeanza, Miamba hao wa Old Trafford Rasmi imewasiliana na klabu ya Fulham mara moja juu ya kutaka kumsajili kinda wao, Ryan Sessegnon.
:
✍🏼 United itakutana na Upinzani kwani, Tottenham na Juventus pia wanavutiwa na kijana huyo, ambaye leo anatimiza umri wa miaka 19, lakini United ni timu pekee ambayo imetuma maombi yao kuwasiliana na Fulham hadi sasa.. Kwa mujibu wa chanzo makini @skysports.
:
✍🏼 Sessegnon inaeleweka kuwa hawezi kucheza msimu mwingine katika Championship kufuatia Fulham kushuka daraja ikiwa ni msimu mmoja tangu wapande Premier league, United wanataka kuongeza vipaji kwa kusajili wachezaji vijana katika kikosi cha kocha Ole Gunnar Solskjaer..
:
✍🏼 Fulham huenda wakakubali kufanya Biashara ya kumuuza Sessegnon kwa vilabu vinavyomtaka kwani kinda huyo kabakiza Mkataba wa Mwaka mmoja tu kuwatumikia watoto hao wa London..
#transfers #Updates #premierleague
@Sokawaytz