Majanga ya msimu uliopita yaikumba tena Yanga

Wakati kikosi cha Yanga kikitarajiwa kuchuana na Azam Fc Jumatatu, April 29 katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara, kocha Mwinyi Zahera huenda akalazimika kutumia wachezaji wa kikosi cha pili kufuatia mgomo unaofanywa na wachezaji wa kikosi cha kwanza

Leo Zahera aliamua kutumia wachezaji wa Yanga B kujiandaa na mchezo dhidi ya Azam FC baada ya wachezaji wa kikosi cha kwanza kugoma tena kufanya mazoezi licha ya kufika mapema uwanja wa chuo cha Polisi Kurasini

Mwishoni mwa msimu uliopita Yanga ilikumbana na changamoto kama hii ya wachezaji kugoma wakishinikiza walipwe hali iliyopelekea kumalizia michezo ya mikaoni ikiwa na kikosi cha wachezaji 14

Huenda hali hiyo ikajirudia tena kwa michezo sita iliyobaki kama viongozi wa muda wa Yanga hawatachukua hatua za haraka kutatua mgogoro uliopo

Wachezaji wafika mazoezini kuendelea na maandalizi ya kuikabili Azam Fc

Wachezaji wote leo wamefika mazoezini kuendelea na maandalizi ya mchezo dhidi ya Azam Fc utakaopigwa Jumatatu, April 29 kwenye uwanja wa Uhuru

Jana wachezaji hao waligoma kufanya mazoezi wakishinikiza waonane na uongozi wa Yanga ili kujua hatma ya madai yao ya mishahara na fedha za usajili

Wagoma tena

Licha ya kufika mapema mazoezini, wachezaji wa kikosi cha kwanza, waligoma kufanya mazoezi wakiwasubiri viongozi wafanye nao kikao

Kocha Zahera alilazimika kutumia Yanga B kuendelea na program ya mazoezi kujiandaa na mchezo dhidi ya Azam

Penati hazina mwenyewe, tuwavumilie wachezaji wanapokosa

Katika mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa dhidi ya TP Mazembe, nahodha John Bocco alikosa mkwaju wa penati tukio ambalo lilimfanya ashushiwe lawama nyingi na mashabiki

Hata hivyo leo katika mchezo dhidi ya KMC, Bocco ameifungia Simba mkwaju muhimu wa penati ulioipandisha Simba hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1

Hata hivyo katika mchezo huo Meddie Kagere alikosa penati ya kwanza iliyotolewa na mwamuzi

Matukio haya yanadhihirisha kuwa hakuna sababu ya kuwalaumu wachezaji pale wanapokosa mikwaju ya penati kwani hakuna mchezaji mwenye uhakika wa kufunga penati kwa asilimia 100

Katika kikosi cha Simba Bocco ndiye mwenye rekodi nzuri ya kufunga mikwaju ya penati.

Kwenye ligi Bocco amefunga mikwaju yote mitano aliyopiga msimu huu

FT : KMC 1-2 Simba

Mabingwa watetezi ligi kuu ya Tanzania Bara, Simba wameendeleza wimbi la ushindi kwenye ligi hiyo baada ya kuichapa KMC mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa uwanja wa CCM Kirumba

Mshambuliaji Emmanuel Okwi ameendeleza rekodi ya kuzifumania nyavu katika ligi hiyo leo akiitanguliza Simba kwa bao safi alilofunga kwenye dakika ya 23

Okwi amefunga kwenye mchezo wa tatu mfululizo sasa akifikisha mabao 10

KMC iliyokuwa bora katika kipindi cha pili ilisawazisha bao hilo kupitia kwa Hassani Kabunda kwenye dakika ya 57 kabla nahodha John Bocco hajaihakikishia Simba alama tatu muhimu kwa kuifungia bao la ushindi kupitia mkwaju wa penati katika dakika ya 82

Hiyo ilikuwa penati ya pili kwa Simba kwenye mchezo huo. Meddie Kagere alikosa penati ya kwanza kwenye dakika ya 60

Ushindi huo umeipandisha Simba mpaka nafasi ya pili baada ya kufikisha alama 66 na kuwa sawa na Azam Fc

Hata hivyo Simba ina mtaji mkubwa wa mabao

Sasa zimebaki alama nane tu kuifikia Yanga kileleni, Simba ikihitaji kushinda michezo mitatu tu ili kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi

Kikosi cha Simba kinaelekea mkoani Mara kuikabili Biashara United, mchezo utapigwa keshokutwa Jumamosi, April 27 2019

Kiporo Kimeliwa Simba Waichapa KMC bao 2-1

Hayawi hayawi sasa yamekua ni katika muendelezo wa simba kula viporo ndani ya uwanja wa ccm kirumba mwanza leo timu ya simba ikiibuka na ushindi mnono wa bao mbili kwa moja huku.

Bao la kwanza la Simba limepatikana kutoka kwa Emmanuel Okwi dakika ya 23 na kusawazisha na mchezaji mahiri kabisa kutoka KMC Hassan kabunda mnamo dakika ya 57 baaadae kabisa dakika za lala salama John Bocco ameipatia goli la ushindi kwa mkwaju wa pelnati dakika ya 82.

Ni moja ya mchezo ulio kua na mvutano mkubwa kutoka pande zote mbili huku AK 14 Meddie Kagere akikosa penalt

Kwa matokea haya sasa simba imemfikia azam fc kwa kuwa na point sawa

Azam Fc vs Yanga kupigwa uwanja wa Uhuru

Mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara kati ya Azam Fc dhidi ya Yanga ambao awali ulipangwa kupigwa uwanja wa Taifa, sasa umehamishiwa uwanja wa Uhuru

Mratibu wa Yanga Hafidh Saleh amesema wamepokea barua kutoka TFF inayowaelekeza sababu ya mchezo huo kuhamishiwa uwanja wa Uhuru ni kutoa nafasi kwa uwanja wa Taifa kufanyiwa ukarabati baada ya kumalizika mchezo wa fainali AFCON U17 utakaopigwa April 28 2019

Kikosi cha Yanga kinaendelea kujifua kwenye uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo huo utakaopigwa Jumatatu, April 29 2019 saa kumi kamili jioni

Uwanja wa Uhuru ulifanyiwa ukarabati kabla ya kuanza kwa michuano ya vijana ya AFCON ambapo nyasi bandia za uwanja huo zilibadilishwa

Waliochangia Milioni moja kualikwa tukio kubwa May 11 Dar

TAARIFA MUHIMU

Kutokana na umuhimu wa Kila Mwanayanga ambae anatoa pesa yake kwa ajili ya timu yetu TUIPENDAYO na yenye Thamani kubwa sana kwetu sote, Kamati imefikia uamuzi ufuatao ili kujenga wigo mpana wa kila mtu kuwa sehemu ya tukio hili muhimu linalohusu uchangiaji wa Klabu yetu.

Tukio Maalum la chakula cha jioni jijini Dar es salaam litafanyika siku ya Jumamosi tarehe 11/05/2019 Hotel ya Serena kuanzia saa kumi na mbili jioni.

Makundi ambayo yatakuwa yameshachangia shilingi milioni moja au zaidi yatapewa kadi ya mualiko na kumteua mtu mmoja ambaye ataliwakilisha kwa niaba na hatimaye aweze kushiriki kwenye Chakula Cha Jioni pamoja na kupokea CHETI MAALUMU cha Shukurani kwa niaba ya kundi lake.

Kamati imeona ni busara kupata uwakilishi huo wa mtu mmoja mmoja kutokana na eneo husika kubeba idadi isiyozidi watu mia tano.

Kwa mantiki hiyo tunaamini tutakuwa tumeweza kushirikisha kila kundi au mtu kwenye matukio haya muhimu kwa Klabu yetu.

TUENDELEE KUICHANGIA TIMU YETU ILI TUWE NA KIKOSI SHINDANI MSIMU UJAO

Timu ya Wananchi Wawekezaji ni Wananchi

Deo Mutta
KATIBU – KAMATI YA HAMASA
YANGA 23/04/2019

Yanga yajitathmini faini za kila mara

Uongozi wa Yanga umesema utachukua hatua ili ‘kujisahihisha’ kuepuka faini za Shirikisho la Soka nchini (TFF) kutokana na matukio yanayohusisha imani za kishirikina yanayojiri kwenye baadhi ya michezo yake

Matukio ya kutotumia mlango rasmi wa kuingia uwanjani yameigharimu sana Yanga msimu huu ambapo jana ilipigwa faini ya nne baada ya kufanya kosa hilo mkoani Mtwara ilipokwenda kucheza na Ndanda Fc

Yanga tayari imepigwa faini zilizoigharimu timu hiyo zaidi ya Tsh Milioni 10 kutokana na matukio hayo ya kuingia uwanjani kwa kutumia ‘njia za panya’

Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amesema matukio hayo yanachangiwa zaidi ya Wananchi ambao kimsingi ndio wenye timu na wanahusishwa kuisimamia timu inapokwenda kucheza

“Umefika wakati sasa tunapaswa kuwaelimisha watu wetu wafahamu athari tunazopata kutokana na kuendekeza imani hizi,” amesema

“Lazima ifahamike kila mchezo una kanuni na taratibu zake. Tukiendelea kuvunja kanuni kutokana na imani zetu, tutaendelea kuigharimu timu”