HOROYA AC Yamuwahi kuntinyu

Aliyekuwa kiungo wa Azam FC Tafadzwa Kutinyu ambaye alikuwa akihusishwa na Yanga, amesajiliwa na klabu ya Horoya AC, mabingwa wa Guinea

Kutinyu ametua timu hiyo akiwa mchezaji huru baada ya mkataba wake na Azam Fc kumalizika

Kutinyu anaungana na Heritier Makambo ambaye anasubiri kujiunga na timu hiyo baada ya ligi kumalizika

Kutinyu yuko kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Zimbabwe kinachojiandaa na fainali za AFCON 2019 zitakazofanyika Misri

Kutinyu na Thabani Kamusoko ni wachezaji pekee kutoka Tanzania walioitwa timu ya Taifa ya Zimbabwe

KAMUSOKO -:Aaga wachezajinyanga

Kiungo mkongwe Thabani Kamusoko yuko Zimbabwe na kikosi cha timu ya Taifa kinachojiandaa na fainali za AFCON 2019 zitakazofanyika mwezi ujao nchini Misri

Ni kama kiungo huyo hatarejea tena Yanga baada ya jana kuwaaga wachezaji wenzake wa kikosi cha Yanga

“Nimewakumbuka sana rafiki zangu, sina neno jingine la kusema zaidi kwani mlikua zaidi ya marafiki,” ameandika Kamusoko ukurasa wake wa Instagram

Kamusoko ni miongoni mwa wachezaji ambao mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu, hatma yake ikibaki mikononi mwa kocha Mwinyi Zahera

Keshokutwa Jumanne baada ya mchezo dhidi ya Azam Fc, Yanga itatangaza majina ya wachezaji ambao wameachwa pamoja na wale ambao tayari wamesajiliwa na timu hiyo

Zahera amesema kuna wachezaji nane ambayo tayari wamesajiliwa na timu hiyo, sita wa Kimataifa na wawili wazawa

Sitaingilia Majukumu ya Zahera – Dk Msolla

Licha ya kuwa na taaluma ya ukocha Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amemuhakikishia kocha Mwinyi Zahera kuwa hatamuingilia kwenye majukumu yake

Dk Msolla ana taaluma ya ukocha na aliwahi kuinoa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’

“Nimezungumza na kocha kuhusu hili. Nimemuhakikishia awe huru kutekeleza majukumu yake,” amesema

“Nitajikita zaidi katika uongozi kuhakikisha yale niliyoyaahidi wakati wa kampeni tunayatekeleza”

“Tutampa Zahera ushirikiano wote atakaohitaji, na kama atahitaji ushauri wa kiufundi kutoka kwangu basi nitampatia”

Katika hatua nyingine Dk Msolla amesema wameanza mkakati wa kuongeza wanachama kwa kuanzisha matawi mapya

“Tunataka tuhamasishe sana uanzishwaji wa matawi mapya nchi nzima,” amesema

“Tutaigawa mikoa kwenye kanda ambapo kila kanda tutapeleka Mjumbe mmoja wa kamati ya utendaji, mchezaji mmoja wa zamani na mchezaji mmoja anayecheza sasa”

“Tutahakikisha wanapita kina kona ya nchi kushawishi mashabiki wawe wanachama”

Aidha Dk Msolla amesema wataongeza ushiriki wa wanachama katika kufanya maamuzi ya timu hiyo kupitia teknolojia kwa kuwashirikisha hukohuko waliko

Utaratibu wa sasa unawapa zaidi fursa wanachama wa jijini Dar es salaam

ADAM SALAMBA: Kuweka Kumbukumbu kiatu cha Banega

Baada ya mchezo wa Kimataifa wa kirafiki dhidi ya Sevilla, tukio la mshambuliaji wa Simba Adam Salamba kumuomba kiatu kiungo mahiri na nahodha wa Sevilla Ever Banega, liliibua mijadala kwenye mitandao ya kijamii

Baadhi ya mashabiki hawakuelewa maana ya tukio hilo ambalo ni la kawaida na hufanywa na wanasoka kama sehemu ya kuonyesha uungwana mchezoni

Salamba amesema ataweka kumbukumbu kiatu alichopewa na kiungo huyo wa Kimataifa wa Argentina

“Kiatu ambacho nimepewa na mchezaji wa kimataifa kutoka Sevilla, Ever Banega nitakichongea fremu iwe kumbukumbu daima,” amesema

Aidha Salamba amesema fursa ya kucheza na Sevilla imemuongezea shauku ya kutaka kwenda kucheza soka nje ya nchi

“Ndoto zangu ni kucheza nje ya Tanzania, baada ya kucheza na Sevilla juzi, imeniongezea ari ya kutaka kufikia malengo hayo”

Francis Kahata amegoma kuongeza mkataba katika klabu hiyo huku akihusishwa kusajiliwa na Simba mkataba wake utakapomalizika mwezi wa saba

Kiungo fundi wa Gor Mahia Francis Kahata amegoma kuongeza mkataba katika klabu hiyo huku akihusishwa kusajiliwa na Simba mkataba wake utakapomalizika mwezi wa saba

Msimu huu Kahata ameisaidia Gor Mahia kutwaa taji la ligi kuu ya Kenya pamoja na kuisaidia timu hiyo kufika hatua ya robo fainali kombe la Shirikisho Barani Afrika

Hata hivyo fundi huyo wa mpira anataka kuungana na Meddie Kagere mshambuliaji wa zamani wa Gor Mahia ambaye kwa sasa yuko Simba

Inaelezwa Kagere amemshawishi kiungo huyo ambaye walicheza nae katika klabu ya Gor Mahia

Gor Mahia inakabiliwa na hali ngumu ya kiuchumi na huenda ikawapoteza nyota wake muhimu wanaowania na timu kadhaa

Mshambuliaji tegemeo wa timu hiyo Jacques Tuyisenge yuko mbioni kukamilisha usajili kunako klabu ya Atletico De Luanda ya nchini Msumbiji

Baada ya kumkosa msimu uliopita, Simba ina nafasi nzuri ya kumsajili Kahata msimu huu

BOCCO Ataka Shangwe za Ubingwa zihamie Morogoro

Jana mashabiki wa Simba waliojitokeza uwanja wa Taifa kushuhudia ‘mnyama’ akikabidhiwa kombe baada ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu, hawakufurahia kuahirishwa kwa hafla hiyo

Licha ya mvua kunyesha, baadhi ya mashabiki walikubali ‘kulowana’ ili mradi tu washuhudie tukio hilo la kihistoria

Hata hivyo Bodi ya ligi iliahirisha hafla hiyo baada ya mgeni rasmi, Waziri wa Mambo ya Ndani Mh Kangi Lugola kupata udhuru

Mtendaji wa Bodi ya Ligi Boniface Wambura alisema sherehe hizo zimehamishiwa mkoani Morogoro, zitafanyika baada ya mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa keshokutwa Jumanne katika uwanja wa Jamhuri

Akingumza baada ya mchezo dhidi ya Biashara United uliomalizika kwa sare ya bao 1-1, nahodha wa Simba John Bocco aliwashukuru mashabiki waliojitokeza uwanja wa Taifa kuwaunga mkono licha ya hali ya mvua

Yawezekana na wewe ulikuwa na wasiwasi kuwa Thomas Tuchel angetimuliwa?

Yawezekana na wewe ulikuwa na wasiwasi kuwa Thomas Tuchel angetimuliwa?
:
Hapana. PSG wamemuongezea mkataba mpaka 2021. Licha ya matokeo dhaifu bado wana imani na uwezo wake. Labda nao wamechoshwa na tabia ya kutimua wakufunzi hovyo.
:
💉PSG walipoteza jumla ya mechi 4 ya Ligue 1 kwa misimu miwili 2017 & 2018
💉PSG wamepoteza jumla ya mechi 5 za Ligue 1 ndnai ya msimu mmoja tu 2019
::
✍️Takwimu zake kwa ujumla
– Mechi: 55
– Ushindi: 40
– Vipigo: 9
– Mataji: 2

Wizara ya Maliasili na Utalii imemteua Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta kuwa balozi wa hiari wa utalii.

Wizara ya Maliasili na Utalii imemteua Nahodha wa Taifa
Stars, Mbwana Samatta kuwa balozi wa hiari wa utalii.Katika majukumu yake, Waziri @hkigwangalla amesema,
Samatta atatakiwa kuzungumza Kiswahili mara kwa mara,
kuitaja #Tanzania na pia kutumia bendera ya nchi. . . … .. . . 👉 Samatta ambaye ni mchezaji wa timu ya
KRC Genk ya Ubelgij atashuka nchini
usiku wa saa 9 kwa ajili ya kujiunga na
Timu ya Taifa ambayo inakwenda
kushiki michuano ya Afcon nchini Misri
na inakwenda ikiwa ni baada ya miaka
39 kupita.

FT: Simba 1-1 Biashara United

Mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara kati ya Simba, mabingwa msimu huu na Biashara United umemalizika kwa timu hizo kutoka sare ya kufungana bao 1-1

Mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa Taifa, ulivurugwa na mvua zilizojaza maji katika sehemu ya kuchezea ya dimba la Mkapa

Biashara United ilitangulia kupata bao la kuongoza kupitia kwa Innocent Edwin kwenye dakika ya 14 na Simba ikasawazisha dakika tatu baadae kupitia kwa Clatous Chama

Mashabiki hawakujitokeza kwa wingi uwanjani kutokana na hali ya mvua inayoendelea kunyesha jijini Dar es salaam

Yatibua sherehe za ubingwa

Bodi ya Ligi imelazimika kuahirisha sherehe za kuwakabidhi Simba kombe kutokana na changamoto ya mvua

Aidha Mtendaji wa Bodi Boniface Wambura amesema mgeni Rasmi Mh Kangi Lugola naye alipata dharura

Simba sasa itakabidhiwa ubingwa mkoani Morogoro siku ya Jumanne, itakapochuana na Mtibwa Sugar katika mchezo wa kumaliza msimu

Uongozi wa Simba umewataka mashabiki wa timu hiyo mkoani Morogoro kujiandaa kuipokea timu na kuwa tayari kwa shamrashamra za kihistoria