




Simba ilipowasili mkoani Mara jana, shamrashamra za mashabiki zilikuwa kubwa hali hiyo imeendelea mpaka leo ambapo mashabiki walianza kuingia uwanjani tangu saa tatu asubuhi

Mpaka kufika saa 10 jioni huenda mashabiki ambao watachelewa wakalazimika kurudi nyumbani kuushuhudia mchezo huo runingani kwani mpaka sasa uwanja wa Karume unaelekea kujaa
Mashabiki wana shauku ya kuishuhudia Simba ambayo imetua mkoani Mara kwa mara ya kwanza baada ya kupita miaka 15
Baada ya ushindi dhidi ya Alliance na KMC, Simba imeingia Mara ikiwa na shauku yas kupata alama nyingine tatu ili kujisogeza zaidi kileleni mwa msimamo wa ligi
Biashara United imeweka hadharani viingilio vya mchezo huo ambapo VIP ni Tsh 20,000/- Mzunguuko Tsh 5,000/- huku watoto wakiwekewa kiingilio cha Tsh 3,000/-
Mchezo utapigwa kuanzia saa kumi kamili jioni
Kila la kheri mabingwa wa nchi…!

Mchezo huo utapigwa kesho Jumamosi katika uwanja huo
Msafara wa Simba uliwasili mkoani Mara mapema leo na kupokewa na idadi kubwa ya mashabiki waliokuwa na shauku ya kuwaona mabingwa hao wa nchi







Mchezo huo utapigwa kesho Jumamosi, April 27 kwenye uwanja wa Karume
Idadi kubwa ya mashabiki wamejitokeza kwa wingi kuulaki msafara wa mabingwa hao watetezi wakati ukiingia Musoma

Simba tayari imeondoka Mwanza na leo jioni inatarajiwa kujifua kwenye uwanja huo
Hii itakuwa mara ya kwanza kwa Simba kucheza mkoani Mara baada ya kupita miaka 15
Biashara United inanolewa na beki wa zamani wa Simba Amri Said

Baada ya mchezo dhidi ya KMC jana, mashabiki wa Yanga walionekana kuisemea KMC kuwa imeonewa na waamuzi huku wachezaji wa timu yao wakigoma kufanya mazoezi wakidai mishahara
Tangu jana wachezaji wa Yanga hawafanyi mazoezi wakishinikiza walipwe madai yao ya mishahara ya miezi mitatu huku wengine wakiwa hawajalipwa fedha za usajili mpaka leo
“Badala ya kuhangaika jinsi ya kuwalipa mishahara wachezaji wenu mnahangaika na timu Bingwa inayowafunga kila siku. Kama nyie wananchi wachangieni hao wachezaji walipwe mishahara,” ameandika Manara kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram















Hata hivyo leo katika mchezo dhidi ya KMC, Bocco ameifungia Simba mkwaju muhimu wa penati ulioipandisha Simba hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1
Hata hivyo katika mchezo huo Meddie Kagere alikosa penati ya kwanza iliyotolewa na mwamuzi
Matukio haya yanadhihirisha kuwa hakuna sababu ya kuwalaumu wachezaji pale wanapokosa mikwaju ya penati kwani hakuna mchezaji mwenye uhakika wa kufunga penati kwa asilimia 100
Katika kikosi cha Simba Bocco ndiye mwenye rekodi nzuri ya kufunga mikwaju ya penati.
Kwenye ligi Bocco amefunga mikwaju yote mitano aliyopiga msimu huu